MAPENZI ya AKUPENDAYE yakifanana na jinsi aipendavyo yake CHUPI!:-(
>> Wednesday, September 09, 2009
Hata kama chupi ni nzuri na mpaka kama upendavyo ina maua ya DHAMBARAU,...
....ikichakaa HUTUPWA,....
.... na uliokuwa UJASIRI WAKE WOTE mpaka ule wa kutunza au tu kudili mpaka na NYETI wakati nyeti inanuka.....
...yote HUSAHAULIKA!
NA chupi ya zamani kwa kawaida bado ni tiifu na katika yake kazi haina DHARAU,...
....ingawa ITATUPWA,.....
... na hata kama mtu binafsi anaweza kumodifai KITENGE au BICHIKOMA LA KAKA liwe chupi, kwa aliyezoea chupi za kununua atataka tu chupi mpya anunue kwa kuwa anapesa na anajua SIKU HIZI ukitaka na unapesa duka la chupi limepanuka,....
...na chupi ZANUNULIKA!:-(
Tukiachana na chupi, kununua mtu kistaili kwaitwa KUTOA mahari hata kwa wenye DHARAU,....
... na kuna wenye dharau za KUTUPWA....
... waonao mtu ni KITU na kirahisi wanaamini MPANULIAJI MAHITAJI akipwaya katika HITAJI ,wapo wengine wapya na wamebobea kwenye hitaji,...
... kwa hiyo wazamani ni juu yake kugundua akianza KUSAHAULIKA.:-(
Swali:
- AU?
- Unauhakika hujanunuliwa?
- Unauhakika akupendaye hakupendi kama chupi huku akijua chupi ikichakaa mpya zanunulika?
- Unauhakika sio wewe umpendaye KIBONGE kama chupi iliyoanza kutoboka kiduuuchu eneo?
NALIKATIZIA WAZO HAPA!:-(
Kumbuka hili ni WAZO TU Kinjekitile au WEYE Mheshimiwa SHUGA DADA, na wala USITISHIKE!
Kumbuka hili ni WAZO TU Kinjekitile au WEYE Mheshimiwa SHUGA DADA, na wala USITISHIKE!
Ngojea Gregory Isaacs abembeleze tena katika- SOON FORWARD
AU tu TKZEE wadai-Palafala
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kazi kwelikweli:-(
Post a Comment