Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mie MKULIMA lakini sijui nijiite WHITE FARMER kama wakulima wa ZIMBABWE ndio nionekane mjanja BONGO a.k.a BAB K?

>> Friday, September 25, 2009

[Tahadhari: Hili ni wazo holela!.-(]

Ukulima ni kitu bomba,....
.....ingawa BONGO kuna wachanganyao UKULIMA na USHAMBA!:-(

Swali:
  • Hivi unauhakika ushamba ni kitu KIBAYA?

Haki ya nani tena, Masela na Masista DU dukinaa, hata ukiwa fundi bomba,...
.... ukichemka au kuingia kichwa-kichwa kabla hawajakutoa nishai WE WAKUJA wanaweza kukukejeli katika staili ya tusi '''WEWE MKULIMA NINI!'' utafikiri wanajua ulivyokuwa mtundu hata gizani ukiwa SHAMBA:-(

Na usishangae kama wewe ni mbongo ukiwakuta WABONGO wadhaniao KIMTOKO wako bomba,...
....wakimshangaa Robert Mugabe na wenzake huko ZIMBABWE wanavyong'ang'ania mashamba wawe WAKULIMA baada ya kumstukia MKULIMA a.k.a WHITE FARMER kuwa ni mjanja kwa kuwa na SHAMBA.

Sasa Sista Du makalio mtikiso SINGIDA-DODOMA uninyimaye nafasi ya kukuomba,...
......kwa kuwa umestukia mie MKULIMA, sijui nikijiita WHITE FARMER Bongo utaniniruhusu angalau nikung'ate sikio katika kujaribu KUMWAGA KAULI NIKUELEZE ningependa katika mambo mpwito basi MWENZIO NIMEJIFIA na ningependa IKIBIDI kimbinde twende SAMBAMBA kwa staili matata za PENDO KIBONGE nilizojifunzia SHAMBA?


Samahani NASITISHA WAZO!:-(
Swali:
  • Hustukii kuwa ni kweli kuna Masista DU na Masela MZANI TANI ambao hawakuchekei wakistukia wewe MKULIMA?
  • Hivi unaamini kilimo cha mkono na hata kile cha trekta vyote vinastaili kuwa na jina moja kuwa eti vyote ni KILIMO?
  • Unakumbuka kutishika kama unajua Tanzania huita kilimo ni UTI WA MGONGO wakati ukifuata takwimu na tafiti za C.I .A zilizomo katika C.I.A World FACTBOOK ardhi inayolimika katika Tanzania ni asilimia NNE tu a.k.a 4%?
  • Unauhakika UTI WA MGONGO ni muhimu kuliko KINYEO?


NIMEACHA wazo Mheshimiwa!

Na hebu tufuatilie tena UKIMWI kwa msaada wa CNN idaiwe -HIV vaccine brings new hope


Au tukumbushane tena kuhusu saratani ya nyonyo kwa tangazo hili[Tahadhari zaidi:Tangao hili halikuhusu kama mtoto au unamchezo wa kukwazika au kufadhaika kirahisi!:-(]

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP