Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati wewe UNASHINDANA na WEWE!

>> Friday, September 04, 2009

Kama unashindana na wewe labda hakuna ashindaye,....

.... na ukidhania unashinda labda huo ni ushindi wa mwisho!:-(


Na kama KATIKA YAKO mashindano, DHAMIRA inakugawa weye,....
... dhamira ikushawishiyo UDOKOE MBOGA ikishindwa na dhamira ikukatazayo KUDOKOA MBOGA.... au tu ikiwa ni mshindi wa pili, kumbuka bado DHAMIRA ILIYOKUSHAWISHI UFANYE bado imeshinda hata kama ITADAIWA ni DHAMIRA mshindi wa mwisho!:-(

Kumbuka mshindi wa mwisho ni mshindi hata kama huitwa wa mwisho NA bila wa mwisho adhaniaye ana USHINDI wa KWANZA NI NYOKO na ukweli labda mkitolewa BARUTI kutokea mbele, yeye YUKO mwisho.

Na tukiwa wawili na ukanishinda, kumbuka NINA haki za kushangilia ushindi wangu wa pili hata ukiitwa wa mwisho,KAMA unamaana kwangu ZINIPELEKAZO JUU hata kama NAENDA JUU huku niko hukohuko MWISHO.

Swali:

  • Unakumbuka mgambo wakitokea waanzao kupigwa virungu sio waliokuwa mwisho?
  • Hivi mtu akishinda na kuwa wa kwanza si maana yake inabidi aanze upya kwa kuwa kwa kifupi mchezo inabidi uanze upya na ushindi uliopita ushageuka NYOKO?
  • Unakumbuka mashindano ya binadamu yaliyo mengi KAMA SIO YOTE yako KICHWANI MWA Binadamu na wala HAYAKO KWA mtu kushindana na mtu au vifaranga wengine, kwa hiyo kwa kifupi ina maana ukishinda maana yake bado na kushindwa kumekung'ang'ani kipengele?

  • Unafikiri mshindi wa mwisho hajashinda?

  • Unakumbuka inasemekana mshindi wa mwisho ndio hujifunza kuliko mshindi wa kwanza?


NI wazo tu KIJEBA!

Hebu twende Tanzania Ras Nas alete kitu -River Nile...




Au tu tubakie hapa hapa Tanzania Jhikoman azungumzie-Mapenzi

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP