BUSARA za BINADAMU kuendeleza UTAIFA baada ya KUFA kwa waliogundua MFUMO wa UTAIFA!
>> Thursday, November 20, 2008
Binadamu wanajifanya WAJANJA halafu kuishi pekee bila kikundi hawawezi.
Kwa bahati mbaya...
...katika kundi la binadamu wajanja , KUNA MJANJA.
Lakini....
...yote ni kutapatapa kumfanyako binadamu aliyeko kwenye kibano kustukia staili ya kutatua tatizo, ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi kukabili tatizo .
Katika kuhangaikia matatizo ya kijiji kunaaliyewaza kutatua kwa kuwa na NCHI.
Ili kuwa na NCHI, lazima kuzaliwe wazo na tafsiri ya nchi ni nini.
UBOVU mkubwa wa fikira za binadamu ni kusahau kuwa hakuna kidumucho au kuganda.
Kila kitu kinabadilika na labda ukifanikiwa kurudi tena duniani baada ya KUFA na kufariki kwa miaka kadhaa, hata Mlima Kilimajaro unaweza ukawa umebakia kichuguu halafu KIGOMA ni bahari ya Pakistani.
Unaweza kubisha!
Kila kitu kinabadilika kama siokupotea na kuzaliwa upya.
Lugha uzijuazo baada ya miaka mia kadha zitakuwa tofauti na uzijuavyo sasa.
Na....
....Binadamu na tafsiri za mambo hubadilika baada ya kujua mambo.
Swali:
- Hivi si sikuhizi dunia haiko kama meza?
Sasaaa..
...Binadamu ni king'ang'anizi akizoea staili fulani kukubali jambo laweza kufanyika kwa staili nyingine kama ya ngwasuma.
Katika swala la mfumo mzima wa kuendesha jamii, kwa sababu tuna Mataifa basi tunayang'ang'ania kwa sababu ndio mfumo tuujuao.
Aliyebunia UTAIFA kafa!:-(
Aliyebunia UTAIFA angekuwa hai leo hii na kushuhudia jinsi watu wanavyopigana vita kwa sababu za UTAIFA angeweza kuwa na busara za kuwastua watu kuwa TAIFA umaana wake uko kwenye kurahisisha mahusiano ya watu kushughulikia matatuzi ya kuishi hapa duniani na sio kuongezea MATATIZO.
Waliobunia mfumo wa UTAIFA WAMEKUFA!:-(
Waliobunia, wangeshuhudia mpaka leo kuna nchi kama Tanzania ambayo inahangaikia swala la UTANGANYIKA au UZANZIBARI, labda wangeshangaa ya ULAYA ya NCHI kama UBELIGIJI isumbuliwayo na kama igawanyike ,WAFLEMISHi wajitawale tofauti na Wabeligiji Wafaransa.
Inawezekana ni kweli binadamu anahitaji kuunganishwa chini ya jina moja kama jina WASENGE ili kujitambua. Lakini labda hata chini ya jina WAKONGO bado inashindikana kujitambua kuwa ni Taifa moja kama kunaajisikiaye ni Mtutsi ndani ya KONGO.
Katika kutatua ya leo kama binadamu tunang'ang'ania tafsiri na mifumo tuijuayo leo ingawa mifumo yenyewe ndio hiyo mingine isababishayo Nchi kama ICELAND kuchacha kwa kufuata kanuni wakati NCHI kama TANZANIA kujisifia kwa kufuata HIZOHIZO kanuni.
Tatizo ni...
...waliogundua mfumo wamekufa na sisitumenogewa na mifumo hata kama mfumo sio lazima uwe aina moja katika kutatua matatizo ya jamiii iunganishwayo na neno TAIFA, kama sio tamaduni za walio ndani ya eneo liitwalo TAIFA.
Utaifa starehe.....
......hukawii kujikuta unapepea bendera kwa furaha kushangilia TAIFA!
Na usipoangalia utakosa raha kama huna kwenu kitu kisababishacho upende taifa lenu.
Swali:
- Si kuna mataifa yalikuwa shamba la MTU au kampuni fulani tu?
- Unakumbuka kunakipindi hakukua na neno AFRIKA wakati kulikuwa na watu AFRIKA?
Naoungamkono jitihada za kukumbuka kwanini kulizaliwa mataifa na fikira zakuendeleza amani katika MATAIFA!
Kama Taifa ndio tatuzi , lilinde taifa!
NAACHA MKUU!
TAIFA lako libarikiwe mpaka litakapo badilika maana!
Ngojea tu twende kutembelea TAIFA la Zimbabwe kwa OLIVER MTUKUDZI alete za Pss Pss HALLO...
AU VYBZ KARTEL aongelee ya masikini katika EMERGENCY
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
"Don't worry about the pretty things you hear them say, don't trust no enemy can trust no friend" Alisema Nasio kwenye wimbo wake Dangerous. Ndilo nionalo kwenye haya usemayo. Hakuna la ziada
@Mubelwa Bandio:Si Utani Mzee wa Changamoto!
Post a Comment