Staili ya kujifunza kujisikia MJINGA!
>> Wednesday, November 26, 2008
Wenye akili unawatambua KIRAHISI kwa kuwa wanajua utakachokujua ambacho hujui au unadhani ulitumia akili sana kukijua.
Labda huhitaji hata kujaribu kujifunza ili kujifunza.
Labda siku ya pili tokea kufa, utajikuta tu unajua angalau UJUZI wa jinsi ya kufa siku moja kwa sababu UMEKUFA KWA SIKU MOJA na wengine bado wako hai chooni.
Labda staili ya kujifunza kujisikia MJINGA itafudhu zaidi ukidhania kuwa wengine hawana ujinga.
Swali:
- Unajifunza nini?
- Unauhakika kuwa ufikiriacho unajifunza si kile ambacho hujajifunza bado?
Na ,''NINI'' usiyojifunza ,labda ni ujinga.
Lakini......
......Kufanya ujinga kunahitaji akili kama hujui jinsi ya kufanikisha ujinga ambao kuna wenye akili wadhaniao si ujinga.
Inawezekana kabisa unachojifunza si kile ufikiriacho unajifunza.
Labda ujifunzacho tayari unakifanya na unachofikiria unajifunza bado hujaanza kujifunza.
TUJIFUNZE UJINGA kama tunataka kuwa na uhakika na KUTOKUWA WAJINGA.
Nakutakia kila la kheri katika kujifunza UJINGA!
NAACHA!
Hebu tukumbushwe kidogo kuangalia UJINGA....YOU ARE DIRTY
Au ngojea Patrick ST Eloi atulize kwa Champagn'
Wadau wa bongo nawakumbuka!
Wote mnajijua natumaini!
Bila kuwasahau baadhi mlioko ndani ya picha zangu hizi za mchanganyiko ndani ya bongo kama...
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Lakini ujinga nao una faida zake, si unaoja jinsi wanavyichangana mara dada kuchafua chupi na kaka eti kapenda? labda ujinga ni muhimu ili wajinga wajue umuhimu wa ujinga. Pengine wajinga na ujinga hawapatani lakini hawajui kama ni wao ni ndugu wa damu. Mkuu hivi hawa watu wajinga na mjinga bora ujinga? ndiyo inawezekana nikiandikacho ni ujinga lakini ngoja kwanza...... mjinga na wajinga afadhali nini au ujinga na mjinga kipi bora
NAACHA MKUU kwaherii
@Markus:Haukuwezi kuwa na kinyume cha ujinga kama hakuna ujinga.
Post a Comment