SIKILIZA mahubiri upate starehe ya KUJISIKIA unaDHAMBI!
>> Friday, November 21, 2008
Si mpaka sheikh ahubiri ndio ustukie una dhambi!
Dhambi ipo tu hata kama huikumbuki sasa hivi wakati ukobize ukifanya dhambi ya kufikiria wengine wanadhambi.
Akuhubiriaye utubu anaweza akawa katikati ya kujua dhambi afanyayo hata kwa kutamani kidogo akukatazayo katika mahubiri ya kuonja nanihii.
Kumbuka...
.... unafikiria ngono wakati unahubiri kukataza ngono.
.....unafikiria wizi wakati unakataza wizi na labda katikati ya kukataza wizi utastukia kuwa uliiba kwa kuibia kuchungulia maeneo yakuleteayo dhambi ya uasherati
Labda ...
... ni kweli kuwa wakati unakataza watu wasifanye dhambi ,huifikirii dhambi kinamna ya kufanya dhambi au uelewavyo wewe maandiko yanavyosema kuhusu jinsi ya kutenda dhambi.
Uelewavyo wewe maandiko NA KUHUBIRI kuwa si dhambi , inawezekana MUHUBIRI MWINGINE akawa na uhakika unatenda dhambi, kwa kudai Yesu ni Mwana wa MUNGU na ndio njia pekee, wakati kuna WAYAHUDI wanaomsubiri mpaka leo NA PIA wale wenye uhakika na ALLAH.
Tunaweza kubishana na KUINGIA dhambi kwa kukataa hata uhalali wa HARE KRISHNA katika topiki kama hizi ambazo zinacheza na imani kuliko akili ya uchambuzi ,hasa kwa wakereketwa wa dini hata kama ni ya KIPAGANI.
Naacha, lakini....
.....Inawezekana unashtushwa na stori za dhambi ya kuua.
Lakini labda....
.... hutajisikia kutubu kama wewe ukovitani, unaua kutetea dini ikufundishayo kuua ni dhambi.
AU?
Swali:
- Hivi si bado Tanzania tunapiga wezi na kuua kwa nia ya kuwafunza adabu halafu wanakufa tukiwa bado tunashangilia ;'Piga MWIZI HUYO! '?
- Unafikiri Rais Kikwete kashaua mwaka huu kama Rais Nyerere, au George Bush kwa kusaini muuaji anyongwe?
Labda....
...unauhakika MSHAHARA wa dhambi ni MAUTI kama vile wasio na dhambi wanaishi MILELE ya mpaka kesho vile!
Lakini....
...Baada ya kumsikiliza akuhubiriye halafu hujisikii unadhambi, labda badilisha MUHUBIRI upate starehe ya kujisikia unadhambi ili utubu.
La sivyo unaweza USITUBU wewe, OOOHOOH!
NAACHA MKUU topiki imenishinda!
DUH! Nilishawahi kuhubiriwa hapa kijijini kwa bibi na babu...
Pata busara za Richard St. John akupe siri afikiriazo ni za KUFANIKIWA katika- Secrets of success: Passion, persistence, pushy mothers
Au USISIKILIZE MAHUBIRI haya ,labda unaweza kupata DHAMBI.....(natanguliza samahani kama utafanya DHAMBI ya kusikiliza busara zilizochanganyika na UJINGA wakati nimekuonya)...
Basi Dr Dre anadai-Been There Done That
(Tahadhari! Anatumia lugha chafu kwa wengine ,na unaweza kujikuta umeelewa kuliko ukimsikiliza KOffi Olomide uchezaye muziki wake bila kumuelewa
.....
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
i like this. hawa jamaa wa makanisani huwa waongoooo wanatufanya kujishitaki. mwisho wa yote unaambiwa kutokumrudishia ela zake mungu nizambi, harafua haooo wanatajirika ghafura
@Kamala:Kazi kwelikweli!:-(
Post a Comment