Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

OBAMA kashinda URAISI lakini bado MIMI nina MATATIZO ya kubanwa MKOJO!

>> Friday, November 07, 2008

Ingekuwa poa kweli kama kufanikiwa kwa Kinjekitile kungehakikishia mafanikio ya Kadoda.

Tatizo ni...
Zubeda akila , Mwanahawa anabaki na njaa tu kama hana msosi.

Hali halisi haigandi, na kafuraha hata kakufurahia mazoezi ya kutengeneza mtoto, kana nukta baadaye kidogo.
Kafuraha ka mafanikio ya wengine kanaweza kasikusaidie wewe kufanikisha kutunga mimba na kanamaisha mafupi tu.

Lakini labda ni kweli kuwa mafanikio ya muislamu ni mafanikio ya mkristo kwa sababu wote ni binadamu, ingawa inawezekana pia kuwa ushindi wa Nyerere ndio kushindwa kwa Iddi Amini.

DUH!
........Maisha magumu mpaka unaweza ukajifariji kwa ushindi wa mwingine kupoza kiduchu.
Maisha magumu mpaka unaweza ukasikia raha kwa kumsifia umjuaye kwa umahiri wake usioujua utakao kujidanganya unaujua.
Swali:

  • Unafikiri nani anakujua vizuri wakati wewe mwenyewe saa nyingine unanuna bila kujua sababu zako za mnuno wakati uko peke yako chooni?
  • Unauhakika na ya kesho?

Maisha maguuuumu halafu tunakufa!:-(

Maisha magumu mpaka.....
  • KAMA mkristo wa jumapili, JUMAPILI inakukumbusha kwenda MSIKITINI!

  • UKIIONA Bidii, inaweza kukutia uvivu, kama jangwa likukumbushavyo msitu.

  • Kuna wajuao wewe ni MUISLAMU wa kusali ijumaa watakaoshangaa jumatatu inakukumbusha kwenda kanisani .

Unaweza ukadhani kuwa kitu kizuri wafanyacho ni kivutio cha wote kufanya vizuri.

Lakini bidii inatia uvivu hata kama ni ya kushusha kilo au kumwaga lita baada ya kumaliza kula na kunywa.

Bidii za wengine zinaweza kukukatisha tamaa kwa kustukia ugumu wa shughuli itakayo kulazimu kuvua kabla hata hujavaa.

Ni utundu lakini kuudanganya ubongo wako kuamini kuwa kwa sababu kapata na wewe utapata.
NI ushujaa kujitafutia kama chake kwa jasho lako bila kuingiwa hamu ya kumloga , kwa sababu alivyopata inakutia moyo labda nawewe utapata na huamini uchawi na sio mwizi ingawa tokea mdogo unatabia ya kudokoa sukari.

Tatizo ni....
...aliyepata anaweza akawa ameiba kile kidude.

Lakini.....
Inawezekana ni busara kuweza kuishi na kukosa na kuelewa kuwa walionavyo, vyao ni vyao na wala huvihitaji kama tu usivyoliihitaji limchumba lako au limtu ulilengalo kama bado halijakupata.
Swali:
  • Unauhakika wakati unahangaikia maswala ya kulenga wewe sio mlengwa?
Lakini.....
.....NI AFYA kufurahia mafanikio ya wengine.
Kwani ni lazima kila siku iwe wewe tu ndio unapata jamani?



Naacha basi MKUU!

Hebu tumsikilize MUNISHI akumbushie mitazamo ya Wakristo katika MANABII wa UONGO

Au labda nimuachie tu MAD COBRA asifie ngono katika FLEX.....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP