Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

PEMBENI kidogo ya NANIHII!

>> Friday, November 28, 2008

Ukiwa pembeni kidogo , unaweza ukashuhudia vizuri!
Pembeni kidogo , labda huonji!:-(


Pembeni kidogo ya kishimo, si shimoni.

Na...
..... ni ujanja kujua ya ndani ya kishimo bila kudumbukia kishimoni.

Kipofu anaweza akakuandikia wimbo kuelezea uzuri wa ampendaye mpaka wewe unayeona unaweza kuwaza mara tatu na nusu; kajuaje MTOTO ana MASHAVU ya KUMIMINA na chunusi zinampendeza kama FENESI wakati haoni.

Kuelewa vizuri ya kwenye kishimo ,unachohitaji ni kujua kuna kishimo hata kama hujui kinaitwa kishimo.

Ukidumbukia shimoni, si kweli kuwa ,ujanja ni kutoka shimoni.

Shimo laweza kuwa ndio handaki ulikimbialo na usitalo kutoka.

Kama wote wanaamini kujitoa shimoni ndio ujanja, INAWEZEKANA ndio utapata faida zaidi kwa kubaki shimoni peke yako.

Swali:

  • Bado unajisikia kuanzisha kioski uuze ndala kwa sababu majirani wote wana kioski kiuzacho ndala?
Toka tu kishimoni kama wale , kama unafikiri faida ni kufanya kama wale.
Ukitaka kionekane vizuri au kirahisi, basi jaribu kisifanane na vile vya wengine.
Swali:
  • Unauhakikagani dunia ni ya duara wakati uko duniani?
Kumbuka...
...vitu vingine vikitolewa kishimoni Nyani hawiMJAMZITO!

DUH!
BAADAYE BASI, na usijali kama hunielewi!
NAWAZA tu hapa MKUU!

AU?


Twende kidogo Ethiopia kwa HELEN alete simulizi za YENE FIKER

Au ngoja turudi tu BONGO kwa KASSIM amlalamikie AWENA...

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:10 pm  

Mkuu pale pembeni kulikuwa na shimo moja hivi, lakini lilitengezwa ili liwe shimo. Lakini sijui kama linanuka au la kwani linavalishwa pazia ili watu wasijue kuna ninindani. Ngoja lipo hapo kweny kona ya kwenda nje karibu na mlango wa ndani, kulia kuna giza halafu utamkuta jamaa kashika chupa toka ILALA, lakini usidhani mapaka alale wala ukisimama tu unaona kila kitu hata kile kitamu usichokipata, leo kipo nenda kaone
KWAHERI

Simon Kitururu 12:41 am  

@Markus: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP