Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kitu TOFAUTI kwa kuwa ni TOFAUTI kuna kiwaingizao UOGA!:-(

>> Friday, January 28, 2011

Lakini,....



...kitu  tofauti  kinaweza kuwa ndio sababu  kuna MTU aliyekwenye ndoa,...
.... anavutiwa kuonja nje,...
... kwa kuwa kila akipigiapochabo anapandishwa ashki ya kujua  KAMA kitu tofauti ,...


.....NI KWELI NI TOFAUTI mpaka LADHA   au TAMUTAMU KUNOGA ni ileile tu  ya kuwa kwa kuwa ni BATA basi kwa vyovyote hata kama ni BATA MWINGINE  na HUYU NI MWEUPE basi ladha yake itabakia kuwa ya BATA TU ingawa bata huyu ni MWEUSI na mwenye matege kwa mbaali na MACHO ya kulegea.:-(


Swali:
  • Ushawahi kujiuliza ni kwanini KITU HICHO HICHO kimoja TOFAUTI kuna mwingine kinaweza kumtisha kwa kuwa ni TOFAUTI na mwingine kikamvutia kutaka kuonja kwakuwa ni TOFAUTI?


Ndio,...
.... labda uliyokutananayo MAISHANI  na  YALE ujuayo TU  yanakujengea misingi ya KUTISHWA , kuwa nyutro au tu KUVUTIWA  angalau kuonja au kuonjwa bila woga kisa ni KITU tofauti .:-(

Ndio,...
.... KITU tofauti na ULICHOZOEA pamoja na UTAMU WAKE kuna mtu anatishika nacho,...
... na labda ndio MAANA  kuna WATANZANIA hataufanyeje watakuambia ni HERI JINI LIKUJUALO halikuli  kidude mpaka KIGUNZI KIKAISHA kuliko JINI LISILO KUJUA ,...
... yote ikiwa ni kujaribu tu kuishi na WALIYOZOEA kwa kuwa YALE TOFAUTI yanatisha.:-(

Swali:
  • AU?
Ndio,..
... kwa kuogopa kitu TOFAUTI,....
.... kuna mpaka WAKRISTO ambao hawawezi kusikiliza ya WAISLAMU ,...
...... WAMASAI wala nyama ambao hawaonji ng'o SAMAKI kwa kuwa ni tofauti,    wa  BONGO FLEVA ambao kamwe wanaogopa kufuata MDUNDIKO,...
... na kwa ujumla kuna WARIDHIKAO TU na YALEYALE kisa wameyazoea VILEVILE ,...
... na hapa wala babu wee mie siongelei  KUWA WAMEZOEA staili zenu za chuma mboga na za KIMISHENARI ndio maana wameridhika nazo na kilichobakia inabidi watafute tamu kivingine  KWINGINE kabisa.:-(


Ni wazo tu hili MKUBWA na wala usipandishe jazba basi MHESHIMIWA !:-(



Hebu Earth, Wind & Fire wabadili kwa kuzibua sindimba kwa kibuyu -Devotion




Au tu Earth, Wind &Fire watulize tu boli pia kwa -Lets groove

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP