Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI tunasifia USHUJAA wa KIBANGA ampiga MKOLONI enzi hizo au tu MASHUJAA TU waliopita!:-(

>> Friday, January 28, 2011

Yaliyopita hata jana tu KIRAHISI watu huyajaji  kwa vipimo vya LEO,...
..... wakati labda VIPIMO VYA LEO  havifai kupima ya ZAMANI kwa kuwa,...


.... labda CHAKUKUMBUKA TU  hataubishe,....
....kuna TOFAUTI kati ya ya JANA na ya LEO,...


..... na ushujaa wa jana na yaliyofanya MTU huyohuyo kuwa shujaa JANA,....
...vinaweza kuwa na UHUSIANO na yaliyokuwepo tu JANA,...
...kwa kuwa KIBANGA aliyempiga mkoloni  HAPO ZAMANI   au tu MTU HUYOHUYO  wa JANA angekuwepo  LEO,...
.... yawezekana kwa mazingira YA SASA au  yaliyopo tu LEO  ,...

...labda HUYO SHUJAA asingefanya LEO YALE YASIFIWAYO kama USHUJAA asifikao nao LEO  ,...
... kwa kuwa LEO labda angetoka BONGE la baruti kwa kuwa leo  kuna kitu tofauti ambacho chaweza kusababisha MTU yuleyule ALIYEFANYA KITU JANA ,...
...asifanye kitu LEO kama JANA kutokana na yaleyale yaliyojitokeza JANA.:-(

Swali:
  • SI unajua mengi yaongelewayo kuhusu nyakati ZILIPENDWA ni yakufikirika ZAIDI YA UHALISIA  na ndio maana MAREHEMU kwa kawaida hukumbukwa alikuwa MTU MZURI na ya zamani yalikuwa DHAHABU kitu ambacho ukifanya utafiti waweza kustukia LABDA ni ALINACHA TU?


  • Na  si unajua kuna WAKATI  hata mtu mwenye aibu huingiwa ushujaa wa kunya HADHARANI au angalau PEMBENI YA  BASI    kutokana tu na MAZINGIRA ya  WAKATI HUO TU  ingawa hata umshikie kiboko SIKU NYINGINE majanini hanyi NG'O kwa kisingizio anaogopa siafu?

  • Na si si unajua kuna siku hata MBWA KOKO anakuwa SHUJAA kutokana na engo tu uliyombana na atakutoa baruti  ingawa  unamazoea ya kumkimbiza kila umuonapo kwa kujua ni MBWA KOKO huku ukimbwenga mawe ?



Ndio,...
... labda WAKATI na MAZINGIRA yanamchango wake katika ushujaa wa mtu,...
...... ndio maana  kuna aogopaye MUNGU ambaye kuna siku tu na MAZINGIRA  YAKIRUHUSU ambayo atajikuta KISHUJAA KATONGOZA mtu,...
.... na kwa bahati mbaya MAZINGIRA na WAKATI huo labda amtongozaye ambaye kwa kawaida NI BONGE LA MNYIMI  kilokole naye  akajikuta kaingia udhaifu kutokana na WAKATI na MAZINGIRA  na akakubali ,.....
....... na wote hao WAASHERATI wa wakati  mmoja halafu  kwa kiduchu tu ya CHAPUCHAPU   kufanya  WAWASTUKIAO siku hiyo  kubakia na sifa ya aina moja tu ya  KUHUSU  HAO kuwa,....
.... jamaa hao kwa uasherati WAMEFUDHU na kwa bahati mbaya hiyo kubakia ndio sifa yao ikumbukwayo na  JAMII.:-(





Swali:

  • AU?
Ndio,...
.... labda ni wakati tu na MAZINGIRA,....
... ndiyo yaliochangia NYERERE , Kibanga ampiga mkoloni, mpaka MANDELA kuonekana mashujaa,...


.... ingawa hatuwezi kuruka WAKATI huo na katika mazingira hayo ,....
...WALIKUWA WANAJUA NINI kuhusu wafanyalo VILICHANGIA ,.....


...... kwa kuwa ukifuatilia watu kama  MALCOM X mengi aliyokuwa anafanya MWANZO ambayo YALIKUWA YAKITAMBULIKA KAMA USHUJAA  baadaye aliyakana na kustukia ALIKOSEA ,...
..... au tu  kama tu MANDELA wa sasa hivi ambaye ni wakuunganisha watu NA MTU WA DIPLOMASIA   labda asingekuwa na USHUJAA ulioitwa UGAIDI wakati fulani kwa ajuayo LEO na kwa staili zake za kileo ambazo  baada ya kujua kitu zimekaa mkao wa KIDIPLOMASIA ZAIDI ya ule wa KIGAIDI.:-(.

Swali:

  • AU?

SASAAAA,...
.... usishangae siku moja wewe tukikuita SHUJAA kwa utakalofanya kwa kuwa UTATUTETEA siku hiyo kwa kuwa MAZINGIRA, ujuacho  na WAKATI vimejipanga mstari wa kukuwezesha kuruka BONGE la KICHWA ,....
.... hata kama siku hizi inajulikana kuwa kama  KASHESHE LIKIZUKA  weye  kwa kutoka baruti FILBERT BAYI na mbwa koko wote utawaacha nyuma kwa spidi za mbio  mpaka watu wanajikuta wanashangilia  tu -WEWEEE!:-(



NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na usikonde!!:-(


Hebu Mango Groove na The Sarafina Kids waje Live kwa -SPECIAL STAR




Mango Groove waendelee tu na-ULALE KANJANI



Au tu MANGO GROOVE watulize tu boli kifuani kwa-Right Time To Feel Fine

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP