Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati NADOKOA maswala ya KITIMOTO yalipozaa swali la Prof. MBELE kuwa: Je, kuku wa kienyeji ni wa kienyeji kweli?

>> Saturday, January 29, 2011




KUKU wa kienyeji siku hizi TANZANIA kama hutaki kustukia labda inawezekana ni KUKU wa KIZUNGU  ,....
... labda inabidi  umdadavue KIVIPENGELE  BONYEBONYE KWELI ili ujue kwa kuwa  sio MUARABU labda NI KWELI   muonekano wake  ambao MPAKA  hana nywele za kipilipili  sura YA BINZARI  hata kama  sio MSOMALI,...

...labda  kibidii fulani za kutafuta atakavyo tumuone yeye kikwini  ni  bonge la  KINGI .:(




Na labda KUKU wa kienyeji KIAFRIKA siku hizi,...
.....labda ni yule ambaye hujui HATA nywele zake za kienyeji  ni zipi ,...

.....kwa kuwa LABDA  kachoma nywele au tu kaongezea nywele za MHINDI katika USUSI , .....


...na labda wakati ana nywele zisizo za KIZUNGU ,...
....bado kavalisha kichwa  WIGI.:-(


Na KUKU,...
...wa kienyeji  siku hizi,...
.... labda hata kumdaka  inahitaji usasa kwa kuwa  hata matembezi yake  UKIKAA KIENYEJI utakacho watu waelewe kuwa ni ``NAZITAKA  mbivu hizi´´,...

... kama wewe SIO mwenyeji  kwenye tobo LABDA  unawezakuta  KIGUNZI  na labda kweli ndicho katika kuzuia watamanio ``NDIZI MBIVU´´ gunzi kwenye tobo laweza kuwa katika kuzuia MENDE ASIINGIE ndio  ifanyayo kazi ya  KISIGI.:-(


Swali:

  • AU?


SAMAHANI  hebu tuanze TENA ni nini  kilichonipindisha mawazo kutoka kwa Prof. MBELE  katika  chombo cha ujumbe kiitwacho-`` KITIMOTO´´


......ambacho kipo HAPA








Au tupate tu mdadavuo uliofanya kutoka topiki yenye kichwa cha habari `` KITIMOTO´´ kimefanya mpaka nimefikia hapa,...

.....na kabla  ngojea niombe MSAMAHA kwa kumuhusisha mtu  bila kuomba ruhusa,...


SAMAHANI Profesa MBELE kwa  kuanza mbele bila ruksa na baadhi ya vitu nguli nilivyotoa kwako HAPA ambapo ni kijiwe nikihusudishacho sana tu!:-(

 ...ambavyo ni:




Blogger SIMON KITURURU said...

Naombea tu nyama zetu zisiingie magonjwa ya ajabu ajabu TANZANIA kwa maana tutapukutika sana tu!

Kwa maana kuna udhaifu sana katika kukagua usalama wake. Na kama magonjwa kama yale ya kichaa cha ng'ombe na mengineyo yakianza kutawala Tanzania cha moto tutakiona kwa kuwa sidhani kama kuna mzoga utatupwa na kuchomwa uteketee kama wafanyavyo wenzetu nchi tajiri.:-(

Na nasikia mpaka CHIPSI ni kawaida kabisa kutumia mafuta ya transformer za umeme kwenye vikao vingi tu.:-(

January 27, 2011 8:20 PM

Blogger emu-three said...

We acha tu, na watu wanavypenda kuila hii nyama ya nguruwe...kwanza ina mafuta mengi...halafu ...oh, ...na wengine sasa wanaila kwa `ushabiki'..tuangalieni na afya zetu kwanza, mafuta mengi ni hatari!

January 28, 2011 12:48 AM



Blogger SIMON KITURURU said...

Nakubali kuwa kuna mapungufu katika vyakula UGHAIBUNI kutokana na makemikali na nakadhalika lakini angalau wenzetu wanajinsi ya kufuatilia. Sisi kwetu mpaka uoteshaji wa mazao unageuka siku hizi.

Makemikali hata Tanzania yamebobea, mbolea za chumvichumvi nk. Kwa hiyo unaweza kukuta unakula kitu ambacho unazania ni freshi na hakina kemikali lakini kinazo.

Nakumbuka kwa mfano shamba letu la mahindi Songea kabla Baba yangu hajaliuza ilifikia bila mbolea za chumvi chumvi hupati kitu na pia hata kulima nyanya ilikuwa madawa kwa kwenda mbele.


Nachojaribu kusema ni kwamba Tanzania haina usimamizi wa afya za watu katika mazao na vyakula viuzwavyo. Magharibi pamoja na makemikali yao angalau wana institutions zinazofanya kazi kila siku kujaribu kukabili hali!

Ila mengine nakubali kabisa ulicho sema.


Narespond hivyo kwa comment hii hapa chini ambayo niliidaka hapo kabla halafu sasa siioni ambayo ni :


``Napenda kuwamegea kidogo uzoefu wangu, nikiwa mzoefu wa u-Swazi na mteja wa kuaminika wa kitimoto :-)

Mkaanga kitimoto ana wateja wengi ambao ni wateja wa kudumu, watu wa karibu yake, kuanzia marafiki, na pengine ndugu. Anawafahamu; anawapenda na kuwajali sana. Ana uchungu nao. Hawezi kuwafanyia jambo la kudhuru afya zao, labda iwe bahati mbaya au kutojua.

Yawezekana akatumia mafuta ya transfoma, kwa kutojua madhara yake. Lakini akielimishwa, naamini ataacha, maana hawezi kufanya kitu kwa makusudi cha kumdhuru ndugu yake, rafiki yake, au shangazi yake anayekuja kula kitimoto hapo.

Kama ni vyakula bomu, ughaibuni ndiko kwenyewe. Kuku wanalishwa kemikali wakue upesi. Matunda yanakaa "supermarket," hadi kupoteza thamani yake kwa afya ya binadamu. Lakini yanamwagiliwa maji ili yaonekane "fresh." Lakini ni matunda bomu. Na kadhalika.

Tofauti na kitimoto, wanaoandaa vyakula ughaibuni ni makampuni ya kibeparti ambayo lengo lao ni kuchuma pesa. Hawamjui mteja.

Na sasa hao mabepari wasiotujua wametua Bongo na "supermarket" zao zenye kuku kutoka Brazil, vikopo au vipaketi vya juisi ya machungwa vilivyofungashwa Dubai, na kadhalika.

Na wa-Tanzania walioenda shule sana utawakuta kwenye hizo "supermarket." Shule imewaharibu; wanaamini kuwa kwenda "supermarket" ndio maendeleo.

Mimi napendelea u-Swazi. Ukikatiza mtaa kama unavyoniona kwenye picha hapo juu, unakutana na mkokoteni umebeba maembe yaliyoteremka leo leo kutoka Morogoro, au unakumbana na genge panapouzwa machungwa yaliyoshuka asubuhi hii kutoka Msoga kwa Kikwete :-)´´

January 28, 2011 7:07 AM



Blogger Mbele said...

Lo, ndugu Kitururu, kumbe makala yangu uliiwahi hivyo, maana niliiondoa ili kurekebisha pale nilipotaja kitabu, lakini nimerejea tena nikaona umeshaniwahi. Sasa basi, sitaiweka tena, maana itakuwa ni kurudia hicho kipande ulichokinukuu.

January 28, 2011 7:20 AM



Blogger SIMON KITURURU said...

@Prof.Mbele: Mtandao unatisha! Yani uki press tu send kitu mtandaoni jua kuna mtu labda kashakidaka!:-(

January 28, 2011 8:06 AM




Blogger Mbele said...

Ndugu Kitururu, ni kweli unavyosema. Na wewe ni msomaji makini kuliko kawaida. Samahani kwa usumbufu niliosababisha kwa kuondoa makala na wewe ukakuta patupu :-(

Lakini mada yenyewe ni muhimu sana, na hayo unayosema, kwamba kemikali na matatizo mengine yameshaingia Bongo ni ukweli.

Inatisha, maana sasa suali linakuja: Je, kuku wa kienyeji ni wa kienyeji kweli? :-)




Na yote yalianzia kwenye shule  hii aliyokuwa anatoa Prof. J. MBELE  ,...

....kama kawaida yakeWAKATI anafundisha wale wafikiriao hawako DARASANI kama:...

Kitimoto

Neno kitimoto ni maarufu Tanzania. Kitimoto ni nyama ya nguruwe; inapendwa sana katika mabaa na sehemu zingine. Ubora wa kitimoto ni kivutio kwa wateja na neema kubwa kibiashara kwa wenye baa. Hapa kushoto ni sahani ya kitimoto ambayo niliinunua kwenye baa moja Sinza, hatua chache kutoka Lion Hotel.

Ninapokuwa katika miji kama Dar es Salaam, napatikana mitaa ya u-Swazi, kama inavyoonekana katika picha hii, iliyopigwa Sinza, bondeni ukifuata barabara inayopita mbele ya Lion Hotel. Kwa wale wasiojua, neno u-Swazi linamaanisha sehemu wanazoishi wananchi wa kawaida.

Hapo kushoto kuna baa na sehemu ya kitimoto ambapo nimeshakuwa mteja mara kadhaa. Picha hii inaonyesha jinsi mwenye kitimoto anayotangaza biashara yake. Tofauti na zamani, anaweza kuagiza nyama kutoka bucha kwa kutumia simu, na anaweza kuchukua oda za wateja kwa simu pia.


Pamoja na umaarufu wake, kuna hisia tofauti, michapo, na utani kuhusu kitimoto, mambo ambayo yanaweza kufanyiwa utafiti kama sehemu muhimu ya utamaduni wa leo wa m-Tanzania.













Sasaaaaa!....

...bado ,...
....SWALI alouliza Prof. J. MBELE :
  • Je wewe unafikiri ``Je, kuku wa kienyeji ni wa kienyeji kweli?´´:-(
  • Hivi kuna uwezekano KUKU wa KIZUNGU au angalau aitwaye ni wa KIZUNGUsio wa KIENYEJI  kisa kakua haraka, hana tako  au tu kimuonekano hajakomaa sana hata katika kukomalia SHUGHULI, - samahani hivi ni kweli kuna KUKU asiye wa KIENYEJI?



Hebu Roy Ayers na Erykah Badu walainishe katika kubadili matusi kwa - Searchin'







Au tu ZAP MAMA amalizie TU  na kinu NYAMANYAMA kilichobenjuka tayari  kiitwacho -RAFIKI

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mbele 10:56 pm  

Ndugu Kitururu, nafurahi umeifanyia kazi hii habari niliyoiweka kwenye kijiwe changu, na pia yale maongezi yetu kule, ukaja na ujumbe huu wenye kupanua uwanja wa fikra.

Naona wadau watakuwa na mengi ya kuwafikirisha, sio tu kuhusu kitimoto, kuku wa kienyeji, na ubepari bali vile vile suala la profesa mimi ambaye kuonekana kwangu, nikishamaliza shughuli za darasani na maktabani, ni u-Swazi.

Wakaaji wa u-Swazi wana mengi ya kunifundisha. Baada ya kuhitimu vyuoni hadi shahada za juu kabisa, nimegundua kuwa siwezi kujiita mtu aliyeelimika, hadi nianze kujielimisha upya. Ndio maana naonekana zaidi vijijini, u-Swazi, na kwenye kitimoto :-)

Wanablogu niliowahi kukutana nao, akina Mjengwa, Kamala, na Chacha, wanajua kuwa kama ni vikao, napenda vifanyike u-Swazi.

Ni kweli, hii dhana ya kuku wa kienyeji huenda imebakia jina tu, wakati uenyeji wenyewe unazidi kutoweka :-)

Simon Kitururu 2:42 pm  

@Prof. Mbele: MIE wewe karibu kila uandikacho kinafanya nafikiria sana.


Na ni matumaini yangu ni wengi mambo yako ni CHANGAMOTO hata kama huwa hawa-KOMENTI.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP