Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

``SHIKAMOO MWAAAALIMU!´´,...

>> Wednesday, January 19, 2011

... labda kwa wengi ilikuwa ni kufuata UTARATIBU  na wala sio kusalimia kwa HESHIMA!

Ndio,...
.... labda kuna WANAFUNZI wengi waliokuwa wanatamka tu  ``SHIKAMOO MWALIMU´´ kwa kuwa  wanajua tu huo ni UTARATIBU uliobidi kufuatwa MWALIMU akiingia darasani.:-(

Swali:
  • Kwani ni mara ngapi unafikiri unatamka tu mambo kwa mazoea tu na wala sio kweli utamkalo latoka moyoni?
  • Hivi unaamini SALAMU haihitaji anayekusalimu ajisikie kuwa kuna mtu ANAMSALIMIA?

Ndio ,...
...kuna wengi husema mpaka sentensi mwanana ile ``I LOVE U!´´,...
.... ambao hawapendi mtu,...
.... na labda chasanasana wanasema tu hiyo sentensi kwa kufuata ushauri wa watu kuwa sentensi hiyo  huwa inaweza mpaka kulainisha kibano au tu kumrahisishia mtu  angalau kuvuliwa kificha nyeti hivihivi tu kwa kudhania anapenda!:-(

NI WAZO TU HILI!


Hebu tubadili kwa ku JAZZIFAI kijiwe hiki kwa msaada wa  Bobby Hutcherson  katika shughuli....



Bobby Hutcherson aendelee kwa - Teddy




Bobby Hutcherson adunge tu na - Montara



Au tu tupate tafsiri ya Madlib katika ndude hiihii - Montara

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:09 am  

Shikamoo ndu mwalimu!!!

emu-three 1:09 pm  

Mkuu umenikumbumbo, kuna kipindi hata hiyo `shikamoo' tuliambiwa ina tafsiri mbaya tuakaambiwa tuseme `cheichei mwalimu'
Nini maana ya salamu. Ni kutakiana amani, na kujuana hali, kwahiyo utakavyoitamka ni wewe mwenyewe, lakini nia iwe `amani iwe juu yako' na wewe utaitikia `na iwe kwako pia'
Hisia za tafsiri za salamu ziliwekwa kwa nia njema, kukubali `nafasi yako , na pili kutakiana amani. Lakini wanadamu wakaleta `madaluga'...ni hayo tu mkuu

Rachel Siwa 8:21 pm  

Ni kweli kwa wengine nikama utaratibu tuu.Naungana na emu-three, mtoto wangu anaposoma kuna Waswahili wengine hapo sasa tuwapelekapo au kuwachukua kuna tunasalimiana apo sasa mtoto wangu akisema shikamoo baadhi ya waswahili hawaitikii marahaba wanasema hujambo weee!!!!anasema siku nyingine wakiaanza kinuliza hujambo naweza jibu sijambo tuu?. Hapo sasa ngoma inogile!!

Simon Kitururu 2:40 pm  

@Yasinta: Marahabaaa Hujambo Mtoto Mzuri!

@M3:Nakubali kabisa ulonena Mkuu!

@Rachel:Naona kuna wakimbiao Ukubwa hapo! Lakini na mimi nakiri kuwa ni mzito sana kuitikia Marahaba tokea nianze kupewa Shikamoo enzi hizo.

Na bado nikiwa bongo nikiitwa Mr Kitururu huwa nafikiri mtu anajaribu kuongea na Baba yangu na sio mimi.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP