Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati sehemu nyingine kuna njaa, ......HEBU wengine wachezee CHAKULA,!

>> Thursday, September 01, 2011

Hebu tudeku jamaa wakichezea kiungo cha KACHUMBARI!


7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:47 am  

Lakini hatuwezi kuwalaumu wao...mara nyingi pia nimekuwa nikiwaambia wanangu pia watu wengine wasichukue chakula kingi kwenye sahani japo wanajua hawatamaliza...maana mwisho wake kunaishia jalalani. Lakini mwisho nimeona si kosa lao....sijui kama naeleweka hapa...

sam 11:49 am  

Mtakatifu,sikuzote siyo ijumaa!!?.unapofurahi wewe mwenzio upande mwingine analia,anasikitika.hii ndo necha ya ulimengu/dunia.nikumshukuru mungu/au yeyote unaye mwamini,ukipata kula ya siku,kabia kidogo hata kaulanzi au mbege nk. kaka s.

Anonymous 11:55 am  

Da yasinta,katika makuzi yetu ,mara nyingi wazazi wetu walituambia,usitupe chakula.pia ndiyo maana kuna kitu kina itwa kipolo. waache watoto wale ila waeleweshe umuhimu wa kukithamini chakula.vipi sikukuu hakuna kilichobaki!!? kaka S.

Yasinta Ngonyani 12:00 pm  

Hii ndio maana ya kublog..kuelimisha/kuchauriana...nitafuata ushauri waka kaka Sam...Hakuna kipolo bwana:-)

Fadhy Mtanga 12:53 pm  

duuuuuuuuh!

Simon Kitururu 2:17 pm  

@Kapulya:Mie nakuelewa! Swala hilo Mama yangu pia alikuwa ananisisitizia sana ingawa kwa ujumla nilikuwa sio mlaji sana ila mchaguaji sana chakula na ilikuwa kama sihusudu chakula sili. Na kwa kuwa sipendi uji nilikuwa na uruka mpaka ikawa sababu mojawapo wakati fulani nilipelekwa boding wakidhania nitaacha kuchagua chakula na matokeo yake mpaka siku hizi huwa mara nyingi nasahau kula breakfast kwa kuwa mara nyingi sehemu nilizokuwepo ilikuwa ni kifungua kinywa!:-(

@Kaka S:Kweli kabisa usemalo!:-(

@Askofu Fadhy:Mmmmh!

@Wote ila kunajamaa kanitonya kwa pembeni kuwa eti wachezeacho hapo juu hao WASPENISHI ni NYANYA na sio CHAKULA!

Bado najiuliza:
Hivi NYANYA sio CHAKULA?

Na kutoka kwa mdau huyohuyo anadai kwao WASUKUMA eti hata wali kwa WATU sio CHAKULA ila CHAKULA ni UGALI , makande n.k


Kwa hiyo:
Hivi CHAKULA ni nini?

Yasinta Ngonyani 9:59 pm  

Simon kama ndio hivyo tupo wengi tusiopenda chakula cha asubuhi Basi tungepatana kweli ndani ya nyumba..hakuna kupika asubuhi:-) Mimi najua chakula ni chochote kile kimfanyacho mtu kushiba. Hii ndio sababu kubwa mimi sikuli tomato(Ketchup):-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP