Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chochote KIKUCHEKESHACHO kuna mtu KINAMLIZA

>> Friday, July 17, 2009

Kumbuka ,...
..... MAZINGIRA yakiruhusu na UJUACHO maishani kwenye picha ukikioanisha...

.... kuna KIMCHEKESHAYE hata kama kinakuliza WEWE.


Kumbuka,...
...AKITEREZA mtu na KUANGUKA...
..... labda atakayecheka ni WEWE.


Na LABDA kumbuka,...
.... kuna WACHEKAO akifa mtu hata kwa kisingizio ni adui...
.... hata kama sio WEWE.


Na vilevile kumbuka,...
... VICHEKESHO visivyowachekesha wengine...
... labda ndivyo vikuchekeshavyo WEWE.


Nuna basi kidogo labda utastukia na kukumbuka,...
... kuna mtu atakayechekelea akishuhudia umenuna...
...kama ambavyo uchekavyo HATAVISIVYOCHEKESHA kwa mwingine vikuchekeshavyo WEWE.


Labda tu pia kumbuka,...
...KULIA, kucheka, HUZUNI, furaha , mpaka hata KUTEKENYWA labda vyote unavijua....
.... kwa kuwa vyote ni kweli kiunganishi ni WEWE.


Swali:
  • Hivi bado unakumbuka katika SAKATA hili la maisha ajuaye vizuri kikuchekeshacho au kukuliza ni WEWE?

  • Na unakumbuka kuna mtu upishananaye mtaani kwako ambaye HATA SIKU MOJA hakuoni wala kukustukia upo hata tukiachana na swala kuwa unalia au kucheka?

  • Unabisha?
NAACHA UNYAMBISI!

Hebu tubadilishe ustaarabu kwa kusimuliwa ya YESU katika -YESU hakusema yeye ni MUNGU..


Baada ya mahubiri hebu Simba wa yuda - kwaya ya uinjilisti kijitonyama luthern church wazungumzie- Hakuna Mungu kama WEWE...


Baada ya kumaliza mahubiri ngojea Ngwair asimulie siku ilivyoendelea kwa mtu fulani katika kiba-MIKASI

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP