Tatizo la kudai MWALIMU ni MZURI kwakuwa ANARAHISISHA kuelewa!
>> Friday, July 24, 2009
Binadamu ni mvivu ndio maana asilimia kubwa ya yamzungukayo HAYAELEWI
Na ukimpa nafasi atakuelezea kwanini HAELEWI.
Utasikia eti kitabu ni kibaya kwa kuwa HATUKIELEWI.
AU tu Mwalimu ni MBAYA kwa kuwa HATUMUELEWI.
Labda tukumbuke tu LABDA ni MWANAFUNZI ndio MBOVU kama HAELEWI.
Na tukumbuke tu kuwa WENGI wajuao sana ndio ambao kirahisi HATUWAELEWI.
Na kama unampenda Mwalimu kwa kurahisisha SOMO usishangae kujikuta mengi magumu HUYAELEWI.
NI wazo tu KINGUNGE na wala HUU sio MSAAFU!
Hebu tuulizwe- NAni ni Mwalimu wa MAPENZI....
Au tupate wimbo wa Omar Kopa -UNYAGO
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Sasa kama mwalimu harahisishi uelewa wangu nimpende wa kazi gani? Kila mutu ya bantu napenda mambo rahisi rahisi.
Kazi kwelikweli Duh!!
@Papaa Fadhy: :-)
@Dada Yasinta: :-(
Nakubaliana na wewe kihivi: Mwalimu mzuri harahisishi, anakufanya utumie akili vizuri.
Kama una mwalimu anayekurahisishia, hiyo ni hasara kwa sababu utaendelea kuwa mjinga wa yaliyo magumu.
Tafakari nzuri Mkodao.
Post a Comment