Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Udhaifu wa hotuba NZURI kama tu MAHUBIRI MAZURI!

>> Friday, July 24, 2009

Hotuba nzuri LABDA haina cha zaidi,....
.... kwa kuwa HAKUNA cha zaidi kikumbukwacho ZAIDI YA KUWA hotuba ilikuwa nzuri .

UNAWEZA kunibishia zaidi,....
...lakini YALIYOMO kwenye hotuba huwa hayakumbukwi hata kama mazuri.

NDIO!
Labda Hotuba ni maneno tu na hakuna cha zaidi,....
.....na kama kungekuwa na cha zaidi mbona HATUJIFUNZI hayo mazuri kutoka kwenye HIZO zidaiwazo NI hotuba NZURI?
Swali:
  • Pamoja na hotuba au mahubiri mabaya kudaiwa kuwa huwa hayakumbukwi, unafikiri ni nani anakumbuka hotuba nzuri?
  • Unafikiri huwa unakumbuka asilimia ngapi ya yaliyomo hata kwenye kitabu udaicho ni kizuri?
Kuna hawa WATU wako mawazoni mwangu leo na labda YALIYOMO katika waongeacho hakuna chochote cha zaidi ndio maana huwa hatukumbuki waliongea nini mara tu baada ya kudai tuliwasikia wakiongea!:-(

Hebu tuanze na Iddi Amini DADA....


Halafu huyu jamaa ajulikanaye kama Mwalimu Nyerere.....


Halafu kuna huyu MADIBA...


Halafu kuna huyu OBAMA....



IJUMAA na WIKIENDI njema MHESHIMIWA!

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 9:04 am  

Hata chakula kizuri huwa kinakumbukwa tu kuwa kilikuwa kizuri, lakini ukiuliza ladha yake, hakuna anaeikumbuka.

Simon Kitururu 9:08 am  

@Papaa Fadhy: Kweli kabisa usemacho!:-(

Yasinta Ngonyani 7:38 pm  

Mmmhh! Mi sina cha kusema leo:-(

Simon Kitururu 1:14 pm  

@Yasinta: :-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP