Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hamu ya KUNOGEWA TENA kama mara ya kwanza ilikuwa TAMU!

>> Thursday, July 09, 2009

Utamu ULEULE kujirudia ni BAHATI NASIBU,..
... ingawa kwa kuwa MLENDA ushauonja mara ya kwanza wadhani wajua wake UTAMU.

Kama mara ya kwanza ilinoga na ukamsimulia NASIBU,..
.... haimaanishi katika SIMULIZI ZAKO za pili na ZA kumi za UTAMU kwa NASIBU huwa unaongelea uleule UTAMU.

Na haujirudii UTAMU wanasaikolojia WATAJIBU,...
.... kwa kuwa kisaikolojia au hata kihamu onjo la pili na la tisa hata la PEPSI huwa linatofautiana UTAMU.


Na kama mara ya kwanza ni chungu ILIKUSIBU,....
...kumbuka YA KWANZA CHUNGU inaweza ikawa SI CHUNGU ukirudia na KUPATIA jinsi ya kuonja UTAMU.



Swali:
  • AU?
  • Si unajua inadaiwa walioonja na kudondosha BIKIRA na walionja BIA na kudai chungu inasemekana baadaye chungu iligeuka TAMU?
Ni hilo tu na NI WAZO tu usitishike KATIBU WA MASWALA!

Ngojea Rose ROYCE walalamike katika -Love don't live here anymore

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 2:48 pm  

Ndiyo, ndiyo, ndiyo kabisa.
Mara ya kwanza inakuwa chungu (b.i.k.r.a) hadi watu wanasema hawarudii tena, then utamu unapowanogea wanasahau mara ya kwanza ilikuwa ccchungggu.
Lakini hamu bwana.! Hata ufanye nini,! Haiishi.

Simon Kitururu 8:10 am  

@Papaa Fadhy: Si utani :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP