Labda huu ni UKWELI kuhusu MTU YOYOTE yule!:-(
>> Thursday, July 16, 2009
Ukimtafuta MTU mapungufu,....
.... utamkuta na MAPUNGUFU.
Na kwa mapungufu,.....
.... anaweza kukunyoshea weye kidole....
.... huku haoni YAKE mwenyewe MAPUNGUFU.
Na jihadhari na ajulikanaye kwa kukosa mapungufu,....
.... na kama ni yeye mwenyewe ajishabikiaye wako ole.....
....na utakoma mwenyewe ukistukia afichalo lake PUNGUFU.
Lakini kwanini mtu atafute la mwingine pungufu,...
....wakati maishani muda hautoshi hata kujinyoshea mwenyewe kidole....
....katika jitihada za kusawazisha hata lako mwenyewe PUNGUFU?
Swali:
- Hivi ni yako mangapi unafikiri hayana UPUNGUFU?
- Hivi huwezi kutafsiri mahangaiko ya binadamu katika kusawazisha mapungufu kuwa ndio yajulikanayo kama MAISHA?
NI wazo tu KIJEBA usitishike!
Ngojea tubadili hali ya hewa kwa kutoka kwa binadamu na kuangalia ya MAJINI...
Au ngojea tu ALPHA Blondy amuongelee- Fanta Diallo
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Imetulia.
@Malenga Fadhy: :-)
:-(
Ajabu kuna jamaa huwa wanaaamini hawakoseagi. Hawajapungua.
Kaka tuko wote. Darasa tamu
Post a Comment