Hamu ya kuiba!
>> Wednesday, June 13, 2007
Unapozaliwa machale ya kutetea maisha yako unazaliwa nayo.
Unazaliwa unamachale ya kufukuzia nyonyo iko wapi. Ulimi wako unastukia ladha ambazo zinaashiria kitu kibaya au kizuri. Inasemekana hata maswala ya kunenepeana na kuota kitambi yanatokana na machale hayohayo yaliyojijenga katika mwili katika kipindi cha maelfu ya miaka ambapo binadamu alikuwa hana uhakika wa msosi wa baadaye, hivyo kujenga tabia ya kula zaidi ya atakiwavyo ili kuhakikisha kuwa hata kufa kabla ya kupata msosi mwingine.
Kwa hiyo machale mengine na vidubwana vingine unajifunza katika mazingira yako jinsi ukuavyo.
Duh!
Kuhusu hili swala la machale ya msosi.....
Siku hizi ambazo binadamu wengine wameweza kuwa na uhakika wa msosi ujao, halafu juu ya hapo anapata hii kitimoto, ndafu ,.... na sijui nini ile? ...... basi ukiongezea na kilaji hukawii kuongezea mzigo miguu yako!
Swali:
Hivi ushawahi kuona kiwango cha chakula ajiwekeacho mlalahoi?
Ushaona kaota kitambi?
Duh!
Kama mtoto anayekuwa sasa hivi katika mazingira ambayo kuiba ni ujanja, hongo na maswala kedekede,watu wamehalalisha kuwa ni moja ya funguo ya maisha, basi iko kazi!Unaweza ukakuta siku moja sifa ya mtoto itakuwa jinsi alivyoanza mapema kutapeli, kuhonga na kuiba. Hapo ndio utamsikia mzazi akijisifia, na mtoto genius!
Matatizo ya Afrika yamefikia kiasi ambacho inasikitisha, ingawa utasikia jinsi gani uchumi wa Afrika unaanzakukua. Hali ya Waafrika wengi si nzuri, kitu ambacho naamini kinakuza hamu ya kuiba.
Swali:
Hawa waliowengi waonapo wachache wanaiba hukuku vitendo vyao vikijulikana ,lakini bado wanaitwa waheshimiwa, unafikiri hawaingiwi hamu ya kuiba?
Tukizungumzia Afrika kwa ujumla.....
Naamini hamu ya kuiba inaongezeka na kitu kibaya ni ile hali ya watu kukubaliana na mshawasha huu.
Lakini.....
- Hivi kama waafrika uwaonao duniani, tarakimu zinakuambia katika kila waafrika wanne, mmoja ni Mnaijeria, na hali ya Naijeria na Wanaijeria ndio hivyo uionavyo, unafikiri ni lini Muafrika atakuwa kajikomboa?
- Tukiizungumzia nchi nyingine kubwa ichukuliwayo mifano kama South Afrika, ambayo bado chama kimoja kinanguvu kubwa kuliko vingine,kimfikiriacho hata Mzee Jacob Zuma(Mzee wa kuonja pekupeku) kugombea Uraisi.
- Tanzania nchi iitwayo ya amani lakini ipigayo makitaimu, hongo , wizi nje nje .....
Hebu msikilize Fela Kuti kidogo
Fela alikuwa anachukizwa na hali ya Naijeria.Mimi inanichukiza pia, kwani naamini nchi kubwa kama Naijeria ingeweza kuweka mambo yake sawa basi angalau picha fulani kubwa ya Afrika ingegeuka kirahisi zaidi ya hivi sasa.
Ila....
Najua kuwa unajua kuwa mti mmoja haufanyi msitu?
Hivyo bila miti kama Tanzania, Kenya , Eritrea, Togo, South Afrika........msitu uitwao Afrika hauwezi kushamiri.
Tatizo ni....
Bila miti iliyo safi ishikayo nyadhifa(kisehemu msituni)zishikwazo na akina Kikwete, Lowasa, ....na yule mjumbe wa nyumba kumikumi, msitu uitwao serikali hauwezi kushamiri.
Sasaaaa.....
Tukiacha kunyoshea wengine vidole.
Hawa wenye hamu ya kuiba ni mimi na wewe.
Swali:
Wazo lakutaka kuvuta chako mapema halikuingii saa nyingine ukistukia muheshimiwa anavyojichukulia?
Basi bwana wewe bingwa kama huingiwi majaribuni, kwa sababu hasa wakristo nasikia Bwana Yesu alifundisha mwenyewe sala ambayo, jamaa inabidi aombe kutoingizwa majaribuni.
Hii kitu majaribu weee!Acha tu!
Duh!
nakuacha na Fela Kuti tena.....
Lakini...
Naamini jinsi hali inavyokuwa ngumu ndio kaugonjwa ka hamu yakuiba kanaongezeka.Halafu si unakumbuka kunaviongozi wetu wengi baada ya kuiba tayari kaugonjwa kamekuwa kroniki, basi ndio wanaiba kama vile wakifa watanza na mapochopoacho waliojilundikia.
Swali:
Je , walio wengi wakishaingiwa na hamu ya kuiba tutafanyaje kugeuza mambo?
AU
Ndio wakikushinda jiunge nao?
Nisikufiche, nina imani na Tanzania na Afrika kwa ujumla, ila sijidanganyi, kazi tunayo!
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
FELA KUTI,HUYU BWANA NI POA SANA,FELA ALIWAHI KUSEMA KIFO NI TRANSITION KUTOKA SEHEMU FULANI KWENDA SEHEMU INGINE,NA NIKWELI KIFO NI AINA YA KITUO CHA BASI,UNAPANDA DALADALA UNASHUKA UNAENDELEA NA KAZI ZAKO.
NUFF NUFF RESPECT.
Post a Comment