Wadogo leo , kesho ni....
>> Thursday, June 21, 2007
Wakubwa leo pamoja na mapungufu yao ,walikuwa wadogo kipindi fulani.
Kinachosikitisha ni kwamba, pamoja na ukweli wadogo leo ndio wakubwa wakesho, hakuna uhakika watakuwa wakubwa wa namna gani.
Kabla sijasema..
Msikilize Ziggy MarleyAkikuimbia Small People
Kila siku iendayo inamaanisha tumekua kiumri kwa siku moja. Lakini si kweli kuwa hiki kitu kukua kinagusa kila kitu sawasawa. Kuna maswala kama ya umaskini yanaweza kukua kinyume na mategemeo ya wengi, hasa wale watakao kufuta umaskini kama tuujuavyo.
Lakini hebu tuangalie baadhi ya madogo yakuayo.....
- Watoto leo , twategemea kama hawatadumaa basi ndio wakubwa wa kesho
- Njaa iaandamayo dunia leo yatarajiwa kukua ,hasa kutokana na binadamu kuzidi kuongezeka duniani
- Chakula kizalishwacho leo,wanasayansi wanasema kitaongezeka mara dufu kama teknolojia ya uzalishaji mazao itapewa kipaumbele.
- Ghana kama nchi yenye uchumi mdogo leo inapewa miaka si mingi kwa nchi hiyo kujitoa katika nchi za dunia ya tatu.Wataalamu wanadai kutokana na hali halisi ya uchumi na uongozi wa Ghana ,ukijumlisha na ukweli kuwa nchi hiyo itaanza rasmi kuzalisha mafuta., wataalamu wanafikiria haitachukuwa muda kugeuka kuwa kielelezo kuwa hata nchi ndogo leo yaweza kuwa kubwa kesho
- China inatarajiwa kuwa nchi yenye nguvu kuliko zote baada ya miaka kadhaa
- Udhaifu wa mabavu ya USA unatarajiwa kukua kwa jinsi miaka inavyokwenda
- Tanzania ina.........
- Nk
Katika hayo yote hapo juu, nilichotaka kusema ni kuwa, madogo leo yaweza kuwa makubwa kesho,lakini makubwa leo yaweza kuwa madogo kesho pia.
Ngoja tena Ziggy Marley....atuimbie....Black My Story
Duh!
Niko mawazoni tu usistuke sana!
Lakini........!
Tunavyolimbikiza maswala madogo madogo, tutegemee kuwa kesho yatakua makubwa.Inategemea tu na ni madogo yapi.Kama ni madeni madogo madogo leo, kesho yanaweza kukushinda kwa ukubwa.Kama ni akiba ndogo ndogo leo , kesho ya weza kuwa ni hazina kubwa itakayo kukwepesha njaa!
Basi wadau !
Alhamisi njema!
Hebu Msikilize Kidogo Mbilia Bell Akikuimbia kibao Senda
Tukopamoja!
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment