Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Lugha! DUH!Lakini.........

>> Friday, June 15, 2007



Lugha kubwa atumiayo binadamu kuwasiliana na mwenziye haitumii sauti.Mara nyingi ujumbe unamfikia mtarajiwa kwa lugha ya mwili.

  • Jinsi unavyokaa na mdau tu , anapata ujumbe kuwa unamfikiriaje
  • Jinsi unavyo mtazama tu yule kisura au rijali, anajua kuwa unamuhusudu au sivyo.Hivi ni rijali au lijari? Lakini nahisi unajua na maanisha nini.
Nisikutishe !

Wakati mwingine tamaduni na makorokocho kibao yanaweza ya kaingilia haka kamchezo ka lugha na mawasiliano.
Kwani...
  • Nishawahi kuchanganyikiwa kwa kudhani waongeavyo Wanaijeria wengi na Wasomali kuwa wanagombana kutokana na sauti ya maongezi yao mpaka wakicheka ndio nagundua kuwa , kumbe jamaa wanataniana
  • Nishawahi kukutana na wadau wa ulaya mashariki nchi fulani, ambao wewe kama Mtanzania au Mkenya utikisavyo kichwa kukubali ndio wao watikisavyo kukataa.
Sasa kablasijaendelea mpate Clarissa Matota akupe ule wimbo wa Malaika akikuambia PESA ZASUZUA DUGUHUNYUNGU.




Lakini hivi unakumbuka jinsi Afrika Mashariki tunavyopenda kucheza na kuimba nyimbo tusizo zielewa maana yake?

  • Nakumbuka jinsi nilivyokuwa naimba nyimbo za Michael Jackson kwa kiswahili na kuzipatia kabisa.

  • Nakumbuka pia wadau walivyokuwa wanamfurahia nyimbo fulani za Kikongo pale katikaimba zao kulipotokea kakitu kasikikako kwa kiswahili kama wanasema Sehemu za Uke zinauma!
DUH!

Lugha ni kakitu ambako kana mambo mengi ndani yake!
Nimesikia kwa wengine kujua Kiingereza ni ujiko a wengine kujua Kifaransa ni ujiko, wengine sasa hivi hawapeleki mtoto chekechea kama hawafundishi kichina, halafu eti vilevile kuna wengine wanadai wanajua Kiswahili zaidi na...........

Duh!

Swali:
Lugha, dhumuni yake kubwa si ni mawasiliano?

Sasaaa.....
Ni kweli baada ya binadamu kusawazisha maswala ya msosi, mavazi na pakulala lazima atumie mpaka kaujuzi ka lugha kujisikia kamzidi mwenzie?

Hivi kwanini Raisi wa Ufaransa asipojua Kingereza ni sawa lakini Mimi nisipojua Kiingereza , unaanza kunistukia maswala?

Duh!
Nimekupataaaa!
Kwasababu mimi sio Rais!Lakini nani kasema Rais ni babu kubwa kuliko wengine? Au kwa sababu yeye kwa mtazamo wa jamii ame......
Duh!
Sasaa...!
Ngoja nimuache Koffi Olomide.......





Swali:
Hivi , wewe na mimi tukiongea tunaeleweka?


Ni kweli mara nyingi hatusikilizani wala kuelewana ingawatunaongea lugha moja. Sasa katika dunia yenye watu waongeao lugha tofauti , wewe na mimi huwa tunachukua muda kujaribu kuelewa mwingine anamaanisha nini akifungua mdomo? Au ndio tuna......

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Chemi Che-Mponda 6:07 pm  

Simon,

Ujue hata mimi wakati mwingine nikisikia waNigeria wakiongea nadhani wanagombana. Cha kuchekesha WaNigeria wanatucheka sisi East Africans na Swahili. Wanasema tunaongea 'soft' na kiswahili ni soft language.

Simon Kitururu 1:56 pm  

@Dada Chemi:Kweli kabisa wanamchezo si tu wakufikiria kiswahili ni soft ila pia kufikirikuwa ni wajanja na wagumu kuliko wa East Afrika

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP