Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nitakuua Kwa Heshima wewee!

>> Wednesday, June 13, 2007


Kabla sijasema .....

Kuna kawimbo ka Fado ka huyu mwanadada aliyezaliwa Mozambiki aitwaye Mariza kamenikaa kichwani.....


Nikirudi kwenye kamshawasha ka kuua kwa heshima.......

Naweza kusema kwa uhakika kuwa:

  • Tamaduni inaweza kuwa utumwa.
  • Heshima inaweza ikawa ujinga.
  • Dini yaweza kuwa.....
Kutokana na heshima kama zitafsiriwavyo kutokana na misingi ya tamaduni fulani, imefikia kuwa kuna watu huuawa ilikutunza heshima ya familia. Mwanadada anauawa kwa kosa la kupenda mtu wa kabila jingine, dini nyingine au hata famili isiyopatana na familia yake ili kutunza heshima. Mwanakaka anauawa kwa kisa kakufuru kutokana na tamaduni fulani au dini fulani.
Swali:
Hivi dini nyingi sizinasema kuwa ukitenda dhambi utakwenda motoni na kuchomwa milele au utazaliwa tena kama kamnyama fulani ambako kwa akili za binadamu wanaamini ni kabaya......au utaadhibika kisawasawa...nk?


Cheki kidogo haka ka habari kazungumziako kati ya mengi, mwanadada aliyeuawa atokaye kwenye dini ya Yazidi, kwa kosa la kumuhusudu mwanakaka muislamu wa Suni
...


Kuna kabusara Buddha aliwahi kukasema, hebu kacheki:

  • "Do not believe in anything simply because you have heard it.
-Usiamini katika kitu chochote kwa sababu umekisikia tu.


  • Do not believe in anything simply because it is spoken and rumoured by many.
-Usiamini chochote kile kwa sababu kinasemwa na zushwa na wengi.

  • Do not believe in anything simply because it is found written in your religious books.
-Usiamini chochote kwa sababu tu kimeandikwa kwenye kitabu chako cha dini.


  • Do not believe in anything merely on the authority of your teachers and elders.
-Usiamini katika chochote kile kwa sababu tu kimepewa uzito na mwalimu wako pamoja na wakubwa zako.

  • Do not believe in traditions because they have been handed down for many generations.
-Usiamini katika tamaduni kwa sababu zimekuwepo katika vizazi vingi vilivyopita.

  • But after observation and analysis, when you find that anything agrees with reason and is conducive to the good and benefit of one and all, then accept it and live up to it."
-Amini tu baada ya kuangalia na kuchanganua, ukikuta kitu kikubalianacho na uhalisi wa mambo na kinasaidia mazuri na ni kwa manufaa ya mmoja na wengi, hapo kikubali na ishi kwa kukifuata.


Buddha
The "Enlightened One"


Duh!
Unaweza kumkatalia lakini!

Sasa nimestukia nakuchosha!
Lakini....

Swali:
  • Sasa kama hawa wenye heshima, tamaduni na dini, wanajua utachomwa na kusoteshwa na MWENYEZI MUNGU WA UPENDO baada ya kufa kwanini binadamu anajihangaisha kukuua na kukutesa hapa duniani?

  • Hivi kwa kufikiria kwako unafikiri binadamu na MWENYEZI MUNGU WA UPENDO nani anajua kutoa adhabu za kikatili zaidi?


Wapate OSIBISA walainishe siku basi!


Swali:
Ulempango vipi, wakutaka ku........kwa heshima?
BAAADAYE BASI
!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 7:52 am  

Mzee Simon nakubaliana na wewe,pata kitabu cha DANCI CODE.

luihamu 7:53 am  

Mzee Simon nakubaliana na wewe,pata kitabu cha DANCI CODE.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP