Lewis Hamilton na ......
>> Saturday, June 16, 2007
Michezo ni kitu fulani ambacho watu weusi wanasifika sana ulimwenguni!Lakini ukweli ni kwamba hata katika michezo watu weusi wasifikaonayo leo , wameingia au kuruhusiwa kuingia katika michezo hiyo juzijuzi.
Mpya mwenye weusi ambaye amefungua njia katika mchezo tofauti ni
Lewis Hamilton
Swali:
Hivi lini tutakubalika katika maswala mengine zaidi ya burudani na michezo?
Duh!
Kunakale kawimbo ka Angelique Kidjo na Nile Rodgers
Je, ukiwaacha akina Mandela ,watu weusi kama akina Philip Amagweali walioko katika fani nyingine na akina......wataanza kuwa jina lililoko midomoni mwa wadunia lini?
Kwa wafuatiliaji wa michezo na wafuatiliaji wa maendeleo ya watu wa rangi wafunguao mipaka katika anga nyingine.
- Lewis Hamilton ndio dereva wa kwanza wa Formula one aaminikaye ambaye ni Mweusi.
- Jack Robinson, ambaye alifungua mlango kwenye baseball.
- Na wengine kadhaa waliofungua milango katika michezo mingine.
Duh!
Swali: Hivi mchezo wa nguti,kidali na mdako nani alianzisha?
Lakiniiiii......
Michezo mingi haijulikani nani kaanzisha.
Ila Basketiboli ambayo imewapa jina watu weusi hasa Marekani , ni miongoni mwamichezo mipya ambayo ni wazo la mtu mmoja.
Nishawahi kumuandika huyu James Naismith aliyebuni mchezo wa Basketball kipindi fulani.
Duh!
Ushawahi kubuni kamchezo hata kama ni kasiri?
Mimi mwenzio sijawahi!
Duh!
Noma!
Swali:
Hivi kwa nini Wazungu wanaamini yeyote mwenye tone hata moja la damu ya mtu mweusi ni Mweusi?
Wewe unafikiri Lewis Hamilton,Tiger Woods, Baraka Obama, Malcom X, Spike Lee, Jerry Rawlings, ........Maria Sarungi ........ni weusi?
Samahani lakini kama nakukwaza!
Wikimwisho njema!
Wapate Chic!
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment