Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Uhusiano wa Uvutaji Bangi, Sigara na dini

>> Saturday, June 02, 2007


Je, unaungua kale kadude?

Unajua hapo muda fulani, mvutaji ndiye aliyekuwa anathaminika kidini kuliko asiye vuta?
Unajuatena hapo zamani za kaleeee!

Au?
Hivi ilikuwa zamani eeh?

Duh!
Uvutaji wa sigara
na ganja ukiufuatilia , utastukia ulikuwa unahusishwa na dini. Uvutaji ulikuwa unawasaidia waumini katika jitihada zao za kumuelewa muumba.

Swali:
Hivi Muumba, wewe unamuelewa?

Au unafikiri kwanini wa Hindu walikuwa wanamvutia bangi?
Hivi unafikiri kwanini kizazi hiki cha karibu cha Marasta kina mvutia bangi Muumba?

Au ulikuwa unafikiri kizazi cha marasta, kwasabbu kinasifika kwa kufyonza enzi zetu ndio maana yake kilianzisha?
Duh!
Nahisi unahitaji kusoma historia ya tabia mbaya mshikaji.
Duh!
Swali:
Hivi kuvuta ni tabia mbaya eeh?


Wahindi wekundu walikuwa wana mvutia sigara Muumba!
Duh!
Wewe unavutia nini?
Au ndio unamnywea mvinyo?

Duh!
Hivi ni kweli kuna watu wengine wekundu, wengine wanjano wengine......!?
Duh!


Lakini hawa wasemekananao kuwa ni wahindi wekundu walianzisha hii kitu ya kupuliza sigara, kabla hamjaifanya starehe!

Duh!
Ukienda Gabon wa Bwiti wana kamzizi kao.............Duh!

Hivi unafikiria hawa wote waliogundua kakitu wafikiriacho kinawasogeza karibu ya kumuelewa Muumba ni wajinga?

Nakuelewaaaaaaaaaaa!

Mimi sivuti sigara wala bangi wala.............
Duh!
umenikamata.....!

Ni kweli nilivuta majani ya mgomba ...........!:-)


Duh!
AU?


Hili jambo ni gumu kulihusisha na vizazi vya sasa ambavyo hata uhusiano wao na dini ni wamazoea tu zaidi ya imani.

Historia ya sigara inanizingua sana. Ukiifuatilia kutoka Kwa Wamaya, Aztec mpaka kuja katika kipindi cha kuikuta kila kona duniani utazimia mwenyewe. Ila kamchezo haka kakuvuta sigara naona kameenda mpaka kufikia katika kipindi cha watu kujistukia wenyewe kuwa kameenda mbali.

Kale kahistoria ka ganja ndio kalisha piganiwa mpaka vita tayari.Halafu hakana sifa nzuri hata kidogo ingawa ukifuatilia historia yake na sio kufuatia jinsi unavyo isikia leo kwanini mvuta bangi mbaya.....



Duh!
Unajua kutokana na kwamba sichani nywele nahusianishwa sana na mivuto!
Duh!



Hivi wewe unavuta eeeh?



Sawa, nakuelewa kuwa uvuti.Mimi pia.....! Ila unauhakika kuwa Bob Marley na Louis Armstrong na nani yule hivi...........?Unadhani ni wajinga?
Duh!
Kama humjui yule......basi tena......!


Ngoja nimuache Jimi Hendrix hapa.....



Lakini Juzi Uwanja wa ndege Tanzania wamekataza kuvuta sigara.

Duh!
Nahisi hata hospitali za Zanzibar wamekataza katika hiyo hiyo siku ya kuikomelea tumbaku....

Finland wamekataza siku hiyohiyo kuvuta katika klabu zote nchini hapo.
Hii inafuatia kukataza kuvuta ndani ya nyumba.


Sasa hawa wahindi wekundu walioanzisha kuvuta tumbaku wakitaka kuanza kutetea haki yao sijui itakuaje!

Si siku hizi muhimu kutetea mazingira na tamaduni za watu?


Duh!
Heri mimi sijasema!

Sasa............

Tupac
huyu..........


Lakini ukipata muda soma links nilizo unganisha hapa!
AU?


DUH!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 5:12 pm  

AU,

Sikiliza kibao cha Peter Tosh Bush Doctor,

Pata kibao cha Culture
i took up this morning the international herb,it makes i feel so good the international herb,even the doctor cant refuse it man the international herb,

Nuff Respect man.

Simon Kitururu 7:57 pm  

@Rasta :Lakini ukiongea na wahindi wekundundu, tumbaku ndio inauhusiano na Muumba hata kupita ganja, Hivi tumbaku na ganja ipi imempita mwenzie kwa kuwa international herb?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP