Kinyesi si ni Uchafu ?
>> Saturday, June 09, 2007
Pichani ni mtambo wa kutengeneza umeme uliotengenezwa na vijana wa Makambako wajiitao Tanzanite, waliotafuta jibu baada ya kuchungulia tatizo. Picha na Maggid Mjengwa
Inategemea na jinsi ufikiriavyo na jicho lako, wewe unapoona kinyesi mwingine anaona mbolea.
Wengine watakuambia kuwa matatizo ndio changamoto ya matatuzi.Ikiwa na maana wakiangalia tatizo wanaona jibu.
Dondoo:
Lakini wengi wetu matatizo ni matatizo tu, yanakutesa tu bila kukupa changamoto ya kukuwezesha kutatua maswala.
Duh!
Kabla sijaenda mbali, hebu wasikilize wanamama wa Kenya walioanzisha kijiji cha wanawake pekee kiitwacho umoja ,baada ya kuchoshwa na wanaume na mauvivu yao, uonezi wao, ubakaji wao nk.
Wakina mama hapo juu wamefikia hatua ya kuona wanaume kwao ni tatizo.
Si walaumu!
Na nawasifu kwa kuweza kufikia jawabu kuwa waanzishe kijiji chao na wameweza kufanya hivyo. Kwani naamini kuwa katika baadhi ya matatizo tuliyonayo mojawapo kubwa ni kugeuza wazo kuwa vitendo. Ni rahisi kufikiria jambo lakini kulifanya lionekane au kulitimiza si rahisi.
Lakini.....
Nafikiri kuwa kama dunia hii tutafikia jawabu la wanawake na wanaume kushindwa kuelewana na kufikia uamuzi wa kuishi vijiji , miji au nchi tofauti, itakuwa kasheshe zaidi. Kwa sababu bado mimi ni miongoni wa wale waaminio kuwa pamoja na tofauti tulizo nazo, bado kuna haja ya dunia hii kuwa na wanaume na wanawake wapatanao. Ila ni kweli wanawake bado wanateseka zaidi mikononi mwa wanaume kwa sababu bado dunia ni hapa mambo mengi yako chini ya wanaume. Nafikiri kuwa ingawa wapo wanaume wapewao kibano na wanawake kisawasawa, bado dunia inazinguliwa na wanaume zaidi.
Duh!
Uashastukia hili swala ni rahisi kujitoa na kunyooshea vidole wengine kuwa ndio linawahusu kuliko sisi wenyewe eeh?
Sasaaaa..................!
Swali:
Kinyesi si ni kinyesi tu?Au uonacho si maana yake kuwa ndivyo jambo lilivyo?
Swali:
Hivi yale matatuzi ya jambo tuliyofikia si ni mwanzo wa tatizo jingine?
Basi bwana!
Inawezekana kuwa katika kila tatuzi maharage kuna kanjegele ka tatizo jipya.
Na kila siku ni siku ya kuanza upya kutatua , kutazama kinyesi nk.
Lakini je ?
Tunaona mbolea wakati wa kutazama kinyesi au tunaziba pua na kusikia kinyaa halafu inakuwa imetoka?
Tuendeleze basi!Wikimwisho njema!
Mpate James Brown na Luciano Pavarotti
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
MKUU SIMON NAOMBA KURA YAK0.
Umoja ni nguvu...lakini...kinyesi si mtu hutazama kwenye sahani kabla tumbo halijashiba? Kuna jamaa mmoja alikuwa mlafi kweli kwake wageni hawakaribishwi mlo...mamake 'kamuuliza hivi "chakula kitu cha kubania..si kinyesi tu!"
Wanaume naona wanateseka pia ila tu hawtaki kuonekana wanyonge...mjadala wa siku nyingine huo.
James Brown...chaguo murwa kabisa.
Post a Comment