Inasemekana picha moja huzidi maneno elfu nakadhalika tatu na nusu!
Labda ni kweli picha moja hufikisha ujumbe kirahisi kuliko maandishi elfu ziro.
Haki ya nani tena!;huhitaji kujua Kichina ukiona picha, kustukia labda wanaongelea swala la taaluma ya jinsi ya kukojoa porini.
SWALI:
Si umeshaona picha ya Yesu ingawa unajua hakukuwa na kamera wakati Mtume Mohamedi anaoa?
Lakini...... Labda wakati wote mnaangalia picha moja , kuna apataye ujumbe wa matiti wakati wewe unaelimika kwa ujumbe wa matako.
Labda wewe unaona jalala na kuhisi pananuka uvundo, wakati mwenzio anastukia kuwa bado kwenu hamjaishiwa chakula.
Labda wewe unaona picha nzuri wakati yeye anahisi unakamera nzuri!
Labda blogu za picha zimepiga ngwala blogu za maandishi, kwa sababu ni rahisi kuangalia picha za MUNGU katika blogu za video.
Swali:
Ushawahi kuona picha ya MUNGU alivyopendeza?
Unauhakika na tafsiri za ujumbe wa picha?
Basi tumcheki jamaa akikojoa...
Unauhakika umeona eeH?
Au tuangalie tu picha za uume au uke
UMEONA eeh?
Pumzika kidogo basi tuangalie picha ya Mungu wa watu fulani pale Duniani ,karibu kidogo na pale mijusi wafanyiapo mapenzi..... Labda picha , maandishi na hata sauti yako ingawa unanuka mdomo sasa hivi,vyote hufikisha ujumbe kuwa hakuna kinacho dumu.
Labda picha , maandishi na ukininongoneza, vyote vitabaini umebadilika , pamebadilika au cha moto utakiona kwa sababu ile kitu haiko pale tena.
Labda ujumbe uupatao kwa kirahisi kwenye picha kama ilivyo sababu yako yakutotaka kusoma maandishi ,hauna uzito wowote wa zaidi ya ujumbe: PICHA hii NZURI!
Naacha basi Mkuu! Topiki imenishinda!:-( NgojeaMUTABARUKAaghani shairi DIS POEM
Au ngojea tu Maxi Priest afikishe ujumbe kwa mwanamke kuwa anataka tena, katika ONE MORE CHANCE Read more...
Labda kweli kujinyea ni jambo kubwa kuliko kujikojolea, ila ukweli ni kwamba siku ya siku chumba chenye godoro likojolewalo kwa bidii, chanuka tu kama kilichonyewa.
Madogodogo yajirudiayo kila mara huzoeleka na hata kusahaulika jambo tufikirialo ni kubwa likitokea. Mambo madogo madogo ni rahisi kuyapuuzia.
Tatizo ni ...... labda hata kipimo kitumikacho kupima makubwa chaweza kuwa ni cha kupimia madogo.
Ukizoea kuwa makubwa ndio yalalamikiwe na kufanyiwa kazi, madogo huachiwa ya shamiri. Yafikiriwayo ni madogo hata kama mabaya, hayatiliwi maanani kwa kuwa kipimo kitumikacho hakituonyeshi matokeo ya mkusanyiko wa madogo.
Ukweli ni kwamba mengi makubwa mabaya tuyalalamikiayo chimbuko lake ni mkusanyiko wa madogo tuyadharauyo.
Hebu tujikumbushe.....
Mkusanyiko wa viharage ndio siri ya ujazo wa bakuli la maharage.
Umati wa punje za mchele, ndio siri ya wingi wa ubwabwa msibani hata kama ni wa jana na umechacha.
NA KADHALIKA kadhaa wa kadhaaa..
Nataka kusema....
Jambo dogo ni dogo kwa kubwa, lakinilabda jambo dogo ni kubwa kama hakuna kubwa. Ukizoea kudharau dogo kujifunza kuzoea kudharau kubwa si tatizo.
Nina maana... Kama waweza kuzoea kudokoa, waweza kuwa gwiji la kuiba.
Sasaaaaa.......
Inasikitisha kuwa karibu kila ninakopita Tanzania, naonajinsi Watanzania tunavyo dharau mchango wa madogo ambayo wengi wetu tunayaweza.
Chochote kidogo hakina heshima kutokana na mchango mdogo mdogo wa kuamini katika makubwa ulivyofanikiwa kukatisha watu tamaa katika kufanya madogo madogo tuyawezayo.
Siku hizi:
Ukiiba kidogo utafungwa, ukiiba makubwa unaonekana mjanja na ubunge unapewa.
Kutupa hata karatasi moja moja au chupa ya maji haionekani kwamba nimchango usababishao ukubwa wa jalala tuliitalo miji yetu.
Tunaamini katika mchango mkubwa wa serikali mpaka kutufyekea majani mbele ya nyumba zetu .
Ukiwa mfagizi unadharaulika na wathamio usafi wa ulipofagia.
Kusahau mchango uletwao na madogo ni kosa lifanywalo kwa waonao tu kuwa ni mpaka makubwa ya fanyike ndio mchango ufanikishao jambo.
Tatizo ni.... Tulio wengi hayo makubwa hatuna uwezo nayo.
Lakini.... Makubwa yasahaulishayo muonekano wa madogo yaweza kuwa SI msaada mkubwa kama tufikiriavyo.
Tukikumbuka kukumbushana kufanya madogo tuwezayo twaweza kutimiza makubwa.
Sikatai mchango wa makubwa, ila nachoamini ni kwamba tukijenga tena tabia ya kuthamini kufanya tuwezayo bila kusubiri hatutapiga makitaimu namna hii .
Cha kushangaza.....
Moyo wa kuchanga bado upo ingawa siku hizi unaelekezwa kwenye harusi kuliko hata elimu.
Ukiomba mchango wa kusomesha mtoto hupati lakini wa Kicheni pati na begi pati utapata.
Watu huangaika sana kutunza heshima na status zao kwa kujaribu kufanya wasiyoweza.
Labda kwa sababu tunatoka katika tamaduni za kudharau wadogo basi hata kama wanajua kuliko wakubwa hawatasikilizwa.
Sasaaa....
Naamini siri ya kutomzoea kikojozi tumjuaye hata kama leo kajinyea ni kukumbushana kuwa jamaa ni kikojozi. Naamini ndio maana mpaka leo KAMPUNI ya COCA COLA pamoja na kujua kuwa unajua COCA kola inautamu gani, hutumia pesa kibao kukuambia kuwa COCA COLA ni tamu.
TUSIKATE tamaa! Kama umenisoma mpaka hapa labda nimekukumbusha ufanye uwezacho. Siri ni katika vitendo. Uwezo wa kutenda ni binafsi ingawa watu hupenda kunyosheana vidole kuwa jamaa hafanyi bila kujua uwezo wake.
Swali:
Ukubwa au umuhimu wa jambo wa upima kwa kipimo gani?
Siri ya akili ya kutafsiri ukubwa wa jambo si umuhimu wa uchungu wa madogo?
Kama huogopi kufa unafikiri huna woga wa kuvunjika kiuno au nanihii?
Naacha topiki ingawa inaniuma kuwa kazi ipo katika kugeuza mtazamo wa binadamu ! Tukumbuke tu kuwa mchango wa madogo ni mkubwa! Mungu ibariki Tanzania! Mungu ibariki Afrika! TUTAFIKA! BAADAYE BASI!
Ngojea tubadilishe mawazo kutoka katika matatizo ya Tanzania na kwenda Marekani kumsikiliza John McCain akumbushe ya Marekani
Samahani kwa matumizi ya maneno na sentensi ziwezazo kumtia mtu fulani kinyaa kama tafsiri za akili zake humkumbusha chooni , mafinyofinyo au sehemu zinukazo kwa sababu tunasubiri halmashauri ya mji ije kusafisha!:-(Read more...
Kifurushi cha haja Kifuko cha hamu hamu ya kuua haja
Mwenye jungu la hamu ni mchaguzi wa haja
Haja kutenda cha haja matokeo hayati hamu ya haja
Haja ni kuamka kufa nusu ni kulala
Hatua ni kukaa, haja ikiwa kusimama.
Haja kama ni kutembea, ujanja hamu kutambaa.
Haja na hamu ni kukimbia mwenye busara kasimama.
Hamu na haja ni kusimama mchovu kakaa. Aliyepata.......... kalala! Asiyepata.................. kalala!
Kwa mchovu haja ni kulala, na kufa nusu ni kulala.
Hamu ya mkwepa kufa, siri ya muendekeza hamu ya haja.
Hayati mjaa haja na hamu Kifo si cha haja wala hamu. ---------------------------------------------------------------------------------- USITISHIKE usiponielewa ! Labda huna HAJA ya kujua ninaongelea nini ingawa una HAMU yakujua naongelea nini!:-(
IT´S TIME TO PAAAARTY!! YOU ARE ALL MOST WELCOME TO AFRO FIESTA HAPPENING. TAMPERE AFRO FIESTA HAPPENING WILL BE OFFERING VARIOUS MUSIC AND DANCE PERFORMANCES FROM DIFFERENT CORNER OF AFRICA,WITHOUT FORGETTING OUR SUPPER TALENTED DJ´S IN A HOUSE.THEM DJ´S WILL BE PROVIDING GREAT AND EXOTIC MUSIC SUCH AS REGGAE, HIP POP, AFRO BEAT, NDOMBOLO, SALSA, CARBBEAN BEAT, BONGO FLAVA AND MUCH MORE.THIS ISYOUR PARTY.SO PEOPLE!!!LETS THE PARTY GET STARTED!!! COME AND ENJOY THE AMAZING, EXCITING, ATMOSPHERE WITH FANTASTIC PEOPLE FROM ALL OVER THE WORLD.
LABDA aliyeko uchi ndio Mwenye akili na busara,ingawa wengi watadai aliyevaa nguo ndio mwenye busara na hekima na labda ndio mwenye kujiheshimu.
Cha ajabu ni kwamba , amchekaye au kumdharau aliye uchi anaweza akawa hajawahi kujiuliza ni nini busara za avaavyo na je ni akili kuweka umuhimu wa herufi kubwa mpaka umfanye avae avaavyo.
Lakini.....
Aliyeko uchi anaweza akakuvutia au kukutisha kutokana na tafsiri za ubongo wako. Kuna mpaka WAAFRIKA na hata WADUNIA bwelele wadaio wakiona hasa akina dada hawajafunika vichochoro fulani vya mwili hudai kuwa si utamaduni wa AFRIKA.
Swali:
Ushawahi kufuatilia utamaduni wa kiafrika wa kukaa uchi?
Unafikiri ni kwanini Wachungaji/mapadri wa makanisa fulani wanavaa magauni/majoho?
Unauhakika na spidi yako ya kuvaa ukihisi unapigiwa chabo?
Unakumbuka ukubwa wa AFRIKA na tamaduni za uvaaji za kiafrika?
Kuna mijadala kibao kuhusu KUVAA na KUVUA. Tamaduni kibao zimetuletea nini cha kuvaa na jinsi ya kuvaa.
Tamaduni karibu zote duniani zinakubaliana katika kuvalisha sehemu za faragha tu au VIJIUKE na VIJIUUME tu. Mambo ya kuficha kwingine , ni wajanja wameamua na jamii karibu zote zinatofautiana katika umuhimu wakuvalisha nguo matako au hata miguu ,kitu kitakacho kufanya ukose starehe ya kuwa na magaga miguuni.
Maridadi mengine yote yakuficha SEHEMU nyeti kama mikono na hataMATITIya WANAUME yametokana na tafsiri za jamii zenyewe kwa kusaidiwa na hali ya hewa na hamu zao za kibinadamu kama sio imani ambazo mara nyingine hazina ukweli.
Lakini....... Kama unakumbuka siku ulioanza kufikiria kuwa UNAHITAJI kuvaa nguo, wewe BOMBA la mtu. Lakini .... Baada ya kuzaliwa tu kuna walioanza kufikiria kukuvalisha nguo.
Na labda.... Mpaka sasa hivi unapendeza sana tu kama shetani! Swali:
Unafikiri kwa nini kuna baadhi ya binadamu wanataka kupendeza?
Unapovaa nguo unafikiri zinasaidia zaidi kuficha ulivyo mbaya uchi au ni kweli unazihitaji kama kisitiri utu?
Lakini..... Kitendo cha kuvalishwa nguo au kufunikwa tokea uzaliwe ,kinaweza kuwa ndio chanzo chako cha kufikiri nguo zinaumuhimu hata usiokuwepo.
Tatizo ni... Labda bado unavalishwa nguo kwanamna maradufu bado, ingawa unadai hutaki kuchunguliwa ukivaa hilo linguo lako usingizialo kuwa linakusitiri na labda ni kweli linakusitiri ingawa tunaona nanihii kwa mbaaaali!
Tatizo ni.... binadamu mwenye akili bado anaweza kuvalishwa ligwaguro ingawa kanzu haikuhitaji chupi na joto hili.
Pamoja na nguo kuweza kukusitiri au kuficha nanihii, makende au hata kibiongo, inaweza ikawa inatumika kukuficha tu kujua kuwa matumizi yako ya nguo kufunika kila mahali ni matumizi mabaya ya vitambaa.
Hivi kweli kukaa nusu uchi si utamaduni wa KIAFRIKA?
Hivi unakumbuka kuwa vichaa asilimia kubwa hawatembei UCHI?
Inawezekana kabisa binadamu mwenye akili ni yule aliyevaa kibwaya. Inawezekana ni ujinga kutumia akili kutetea kitu chochote kiitwacho utamaduni , mila au desturi zifanyazo ukose uhuru kwa kitu cha mpito kama tu staili za kufunika utupu wa binadamu aliyezaliwa uchi.
Labda kidumucho katika vazi la binadamu ni kuwa uchi.
NAACHA MKUU na nakutakia kila la heri katika BUSARA zako za kuvaa na kuvua! NAWAZA TU HAPA mkuu USIGUNE basi!!
Ngojea basi tujifunze kutoka katika BUSARA za tamaduni au kutoka kwa MAKAKA tumbo moja wawezao na kujua utamu wa kuoa mke mmoja au FRATERNAL POLYANDRY.
Wakati wa shida raha ipo tu ingawa imezidiwa na shida. Wakati wa shida ingekuwa ni bomba la ujanja kwa mjanja kustukia raha iliyoko chini kidogo ya kipele isubiriayo umalize kuteseka na shida.
Labda Kisaikolojia , inawezekana kuna shida unaipendelea .
Labda....
Ukiona mwenye maumivu anacheka, kuna visekunde kaondoa fikirani katika kiini cha maumivu.
Kuna kipindi masikini hakumbuki umasikini wake kama tajiri awezavyo kutostukia utajiri wake wakati anakufa na kastukia haondoki ng'o na ligari lake mkweche au lile jumba la fedha za wizi.
Kuna kipindi unaweza kucheka baada ya kuanguka kitu ambacho ni kinyume na matarajio ya washuhudiao jinsi ulivyoanguka pale sokoni.
Kuna kipindi unaweza ukamcheka mtu kaanguka kabla ya kustukia kuwa amekufa baada ya muanguko.
BAHATI mbaya......
Kila mtu anashida na labda shida yako ni kubwa kuliko yake kama YEYE aonavyo shida yake ni kubwa kuliko yako.
POLE kwa shida yako!Mwenzio chamoto nakiona na shida yangu!
Baadaye basi!
Tulia na Morgan Heritage wakukumbushe Jamaicakama unaweza kufananisha na hali yaTANZANIA katika wimbo KUNA KITU CHAKUKUFANYA UTABASAMU au Nothing To Smile About
MaDJ wakitanzania waliobobea katika fani ya upigaji muziki (U-DJ) watazindua rasmi kundi ambalo litakuwa linatoa kipaumbele suala zima la U-DJ nchini. Uzinduzi huu wa aina yake unatrajia kuleta mageuzi makubwa katika fani ya muziki na burudani nchini Tanzania. Kundi hili limejifunza na makosa ya baadhi ya makundi ya Ma-DJ nchini na kuunda umoja wa aina yake. Kundi hili la Ma-dj litakalojulikana kama C4 linaundwa na Ma-dj waliobobea na wenye ujuzi wa siku nyingi na wanapania kuuteka na kuleta mabadiliko nchini. Ma-dj hawa kuonyesha kuwa wanayodhamira ya kuuendeleza U-Dj na kuleta mabadiliko, wamenunua vifaa vya kisasa vinavyotumika kimataifa kama vile SERATO na VIRTUAL DJ MIXING SOFTWARE, NUMARK HDX TURNTABLES, Pioneer CDJ1000 MK3, Technics 1200 Turntables na Denon. Kundi hili pia lina maktaba ya muziki iliyosheheni muziki mbali mbali kwa ajili ya wateja wao.
Uzinduzi wa Ma-DJ wa C4 inatarajiwa kufanyika jumamosi 1 Novemba 2008 kwenye Ukumbi wa Little theatre kuanzia saa nne usiku.
Kutakuwa na burudani mbali mbali bila kusahau ma-dj wa C4 watadhihirisha uwezo wao wa kukamua santuri. Kiingilio katika shughuli hii ya kukata na shoka ni kwa 10,000/- tu Kwa maelezo zaidi wasiliana na C4 kwenye barua pepe c4unit@gmail.com. UONGOZI WA C4 DJs UNIT
Tanzania DJs set to launch a DJ Unit in Dar es Salaam
Tanzania is soon to experience the launch of the most versatile local DJs who will take Djing to another whole new level. This most anticipated launch will mark a turn in entertainment and DJ culture in Tanzania. This is the launch of C4 Entertainment Unit in Dar es Salaam. C4 Entertainment is a highly selective, hand-picked group of self-driven individuals yielding vastly specialized talent as DJs. C4 Entertainment diverse roster of outstanding DJs includes both established and emerging talent representing the whole spectrum of the club scene. C4 Entertainment aims to revolutionize Djing in Tanzania and has already acquired the latest DJ Equipment and software. For a start C4 boasts of SERATO and VIRTUAL DJ MIXING SOFTWARE, NUMARK HDX TURNTABLES, Pioneer CDJ1000 MK3, Technics 1200 Turntables and Denon. With a music library that cuts across all the genres, C4 are fully equipped and possess the expertise needed to successfully take over DJing in Tanzania.
The launch is scheduled for Saturday 1st November 2008
at the Little Theatre from 10:00pm.
There will be a Special DJ Showcase by C4 DJs and more entertainment.
All these for only 10,000/- per head For more information please contact C4 on Email:c4unit@gmail.com. C4 DJs UNIT MANAGEMENT
Sinauhakika na tofauti ya utamu wa MCHUMBA wa KUJITAFUTIA ulivyotofauti na MCHUMBA wakutafutiwa.
Labda uzuri wa umuitaye mchumba, ni ile tofauti isababishayo uweze kumtambulisha kirahisi kwa watu fulani kuliko mchumba hausigeli/hausiboi au lile tu limpenzi ambalo unanogewa nalo lakini nishai kuonekananalo mchana.
Swali:
Unafikiri kwa nini umuitaye mchumba anatambulishika kirahisi kwa WANOKO?
Unajua tofauti kweli ya mchumba wa kujitafutia na wakumtafuta mwenyewe?
Lakini... Utamu wa mchumba ni akusaidiavyo kisaikolojia kwa kukutuliza kirohochako kwa kuwa KAKUKUBALIA au UMEMKUBALIA.
Mchumba huyo huyo anaweza asiwe mtamu kama alivyokuwa mpenzi tu kwa kuwa unauhakika amekukubalia na labda hata uoga wa kujamba mbele yake hauna maana sana.
Mchumba wako unaweza hata kutomuonyesha sana yale mapenzi kwa sababu ushamvika pete au ushakuwa na ushaidi kutokana na alivyokupa mpaka siri yake ya kale kaugonjwa kake ka kifafa afanyako siri kwa wengine , na ni vigumu kukugeuka kama tu ulivyomsimulia kaugonjwa kako ka herpes.
Mpenzi wako hata bila kumtambulisha kwa maneno, unaweza kustukiwa na umati kwa jinsi ulivyokuwa huru kumfuta aliponyewa kidogo na bundi , karibu kidogo na pasipoguswa na marafiki wa kawaida ambapo umepagusa kwa uhuru kama wa RAIS KIKWETE kufanya ziara nchi za nje.
DUH!
Mchumba aliyetayari kutambulishwa kwa wakwe na marafiki NI MTAMU kwa sababu kwa kawaida hapendi kufanya kosa la kuaibishwa , kitu kimfanyacho awe MKARIMU ili usije kubadili mawazo.
Kisaikolojia, mtu yeyote aliyekubali uchumba anakaudhaifu ka kwamba amekubali na kwa muda mfupi ni vigumu kukageuza kaudhaifu kwa kukataa.
Swali:
Mchumba ni nini?
Unafurahi eeh ukiitwa mchumba?
Binadamu ni kiumbe cha ajabu! Tokea binadamu ajue kuongea anajaribu kutafutia vitu majina na kujifanya yeye anajina. Swali:
Unajua ingawa unajina lako na unatafutia vitu majina lakini ukiitwa mbwa unaweza kugeuka?
Naacha basi mkuu!Unajua na waza tu hapa!:-(
Wikiendi njema na kama tutajaliwa kinamna, basi tutakutana tena hapa baada ya siku kadhaa !
Kama unanafasi mpate kidogo mgombea umakamu wa rais Marekani, SARAH PALIN
Au rudi kidogo miaka ishirini iliyopita umpate MANU DIBANGO akiwa na binti yake GEORGIA wakikumbuka wimbo uitwao Qui est fou de qui? (Chouchou), waliourekodi wakati GEORGIA akiwa na miaka 7
Unaweza pia ukajikumbusha miaka ya 1950 na JIM Reeves akikuambia FLY AWAY
Basi mkuu ngojea turudi kwa LUCKY dubeatukumbushe BACK to my ROOTS!
Jumatatu basi MUNGU akipenda! Nakutakia kwenda msalani kwema!Read more...
Jambo lako binafsi zuri si lazima likae uchi kwa jamii kushuhudia , kwa jamii matunda yake kushuhudia.
Kitu ambacho hata hakijulikani, chaweza kuwa ni chanzo cha wewe kunichekea au hata kuwa na muda wa kunisaidia , kumsaidia ,kama sio kunionyesha chumba cha kujisaidia.
Tusichojua kikusumbuacho , chaweza kusababisha uwe mkali bila sababu katika kiwanja cha penzi .
Unawezaficha siri kwa kujifanya mzuri, lakini mficha siri hufanikiwa kuficha siri kwa yule tu ambaye si makini.
Siri yako ya KUBANA KIJAMBO, yaweza kujitokeza kwa utofauti wa staili yako ya mkao kwa akujuaye. Siri yako ya kubana mkojo , yaweza kujitokeza katika mwendo wako wakwenda msalani kwa akujuaye. Siri yako wakati unaongea na mpenzi wa siri , inaweza ikawa katika staili yako ya kunong'ona kwenye simu huku ukijichekesha katika visivyochekesha.
Siri yako wakati unadanganya , inaweza ikawa jinsi tu unavyosisitizia hoja kwa akujuaye.
Sasaaaaa.......!
Aina ya siri ni muhimu katika kugundua hata faida za ukubwa wa sehemu za siri.
Cha ajabu.....!
Tanzania mpaka yajulikanayo hunekana kama siri , ingawa wenyenavyo hawafanyi siri kutuonyesha ukubwa wa maeneo wayazungushiayo uwigo kuficha siri.
Pamoja na ustaarabu wa binadamu wengi katika ya faragha kuyaacha faraghani, huhitaji kuvua mtu nguo kugundua walio wengi hawana kificha sehemu za siri au hata imeshindikana kuvaa chupi nzuri.
Cha kutisha ni kwamba , kwa mwendo huu walio wengi watafikia kubakia na siri moja ambayo sio siri ,kwa sababu tayari unaona MATAJIRI na WANASIASA wanajijengea ngome ili wengi wasione kifichwacho kwa siri.
Na...... Wanasiasa wako makini , kutuibia mpaka maini Nasi kwa matumaini , twategemea matatizo yetu watakabili
Labda tuwakumbushe...
Kitu tusichokijua kwa mtu tusiyemjua tunayepishananaye , chaweza kuwa ndio kilichotuhakikishia usalama au kukabwa hata pale sehemu tunapopajua.
Na inajulikana.....
Matajiri wanaogopa masikini na wanahitaji kujua SIRI ya furaha ya MPWEKE apatayo kwa kuiangalia chupi yake yenye rangi nzuri hata kama haitashuhudiwa na kipenzi katika kibanda cha faragha.
Na inajulikana .......
Wanasiasa wanajua kuwa sasa hivi waliowengi wanastukia kuwa hawafaidiki na siasa zao ingawa bado wanadanganyika kirahisi kwa stori za danganya toto ambazo zinakubalika kutokana na kitu ambacho sio siri chenye uhusiano na elimu na umasikini huohuo.
Muhimu kukumbuka kuwa , wenyenavyo hawataweza kufaidi walivyo kuwa navyo kama WASIONAVYOwataendelea kusahauliwa na kuendelea kutembea na siri ya machungu ya kukosa na kuwa na uhakika kuwa wenyenavyo ndio tatizo.
Wanasiasa na matajiri kumbukeni kuwa mtafaidi sana kwa kuhakikisha angalau na wengine wanapata mpatavyo hata kama vyenu bado ni vya dhuluma.
Hakuna atakaye taka kukuvamia na kuhatarisha maisha yake ili akuibie TV yako ya inchi 120 kama angalau anako kaTV kake ka nchi 32.
Utafaidi kutembea na LIFERARRI lako ikiwa angalau na wengine wana vi RAV 4.
Hata pesa za EPA labda hakuna ambaye angefuatilia sana kama watu wangekuwa wamejazwa mapesa angalau ya kuwa na uhakika familia itakuwa poa tu kesho na kesho kutwa, na hata vijipesa vya kuongezea maisha kutokana na kale ka UKIMWI, zipo.
Labda....... Inategemea unaficha nini , kwa umahiri wako wa chaguo la ukubwa wa sehemu za siri kuwa mahiri. Kifichikacho leo , kucha yake yaweza kukiumbua kesho . Ikiwa huna ili, labda lile au kile chaweza kukahidi kuingia kwa ulaini katika pango hilo la siri.
Ukubwa wa jambo la siri waweza kugundulika SIKU ya KUFA kwa NYANI ambapo miti yote huteleza. Swali:
Hivi umevaa chupi nzuri ee?
Hivi unataka chupi yenye rangi nzuri kutokana na yule akusaidiaye kuivua atakavyokujaji kutokana na kificha faragha au pale uianikapo mbele ya macho ya jamii?
Binadamu wenye AKILI TIMAMU ni waoga na ukiwawezesha kuchagua wakuonea, wataonea VIBONDE.
Ni vigumu kwa mwenye akili MUKICHWA kukiri mbele ya NJEMBA afikirialo halitapenda lichukiwe kuwa analichukia. Hata iwe ni kale kabosi kako tu kenye umbo dogo na kwa kisiri unahisi ni kajinga lakini kanaweza kakakufukuza kazi ikupatiayo vipesa vya kutesea binadamu wenzako na kagari kako Mkweche , ikibidi itabidi ukasifie kuwa unakapenda kama sio kukahonga sehemu zako za haja ndogo.
Wapo ambao wanaweza kumtukania MUNGU kama tu wawezavyo kukutukana WEWE na MIMI. Wapo ambao tunaamini hata kumtukana binadamu mwenzako ni UJINGA.
Lakini wengi wapo ambao hata mapenzi ya MUNGU hatuyaelewi lakini hata kujiuliza sana kuhusu Mungu tunaogopa kukufuru.
DUH!
Basi bwana ,labda ni kweli UNAMPENDA MUNGU wako na ni kweli anakupenda ndio maana anakuacha uwe hai halafu MAISHA MAGUMUUUUUUUUUU!
DUH!
Swali:
Si kuwahai ni jambo la kushukuru na wote wajiuao Wajinga?
AU?
Unaweza kumuogopa na kumpenda mtu?
Nawaza tu MKUU na usichukie kama kweli unadai wewe ni MTU wa UPENDO hata kwetu wenye dhambi!
DUH! Naacha!
Ngoja Yvonne CHAKA CHAKA atusimulie jinsi jinsi anavyompenda DJ katika I am IN love with THE DJ Read more...
Upendo wako LABDA unaashiria kuna kitu UNACHUKIA. Upendo wako unaashiria kuna kitu chenye uhusiano na ukipendacho ambacho UNAKICHUKIA. Upendo wako wa vita kama tu nyege yako ya kumfunza adabu NANIHIINO, kuna umlengaye na si kweli kuwa itaondolewa UKAME kwa kumpiga yeyote tu apitaye mbele yako.
KUNA umCHUKIAYE, kuna ukichukiacho ambaye au ambacho ndio kipele kikuwezeshacho kugundua siri ya utamu wa UKIPENDACHO.
Labda itabidi tu ufurahie chuki kwa kukuokoa kutoka katika maisha yakutojua Upendo ni nini.
Labda tushukuru kwa kuwa Binadamu kwa sababu UBINADAmu unatusaidia kushindwa kuelewa hata mapenzi ya MUNGU wa UPENDO awezaye yote aachiapo tuwapendao wateseke na tuwachukiao wawini MAISHA au hata sehemu za siri za tumtamaniye.
Mwenye chuki na MTU au hata CHUPI , ni rahisi kufananishwa na BINADAMU MBAYA. Mtu mzuri anafananishwa na matendo mengi watu waaminiyo ni matendo mazuri kama vile UPENDO au UKARIMU hatakama matendo hayo yanaweza kukuzawadia UKIMWI.
Binadamu huongelea, husifia upendo na amani mpaka anaweza akasahau kuwa mara nyingi ni chuki na vita vilivyomgundulisha starehe moyoni.
Hakuna binadamu asiye na chuki na kitu fulani kama sio chuki kwa MLENDA au LISURA lako ambalo kuna baadhi ya binadamu au hata mbwa waonyeshao dalili ya kulipenda au walisifialo kuwa zuri.
Tusitake kujidanganya.....
Kwa wakristo watakustua kuwa Yesu wa upendo alikuwa anachukia kama kwa Waislamu , Mtume Mohamedi alivyokuwa anachukia .
Wale Miungu wengine ambao baadhi wanasaidia mpaka akina NANIHINO kupaa na ungo pia nasikia wakichukia, hata mvua hazinyeshi pale kijijini kwetu. Swali:
Si ni kweli Mungu wa upendo alianza kuchukizwa na vitendo vya binadamu tokea ADAMU na HAWA?
Sasaaa..... Unauhakika gani kuwa unajua UPENDO ikiwa tafsiri ya UPENDO wa kibinadamu labda wala haifanani na Mungu amaanishavyo kwa neno UPENDO?
SWali:
Unauelewa upendo wa Mungu kama huelewi Mungu muweza yote kuachia uwepo wa chuki?
Unauhakika unauelewa upendo wa MUNGU kama upendo wako mwenyewe unategemea CHUKI?
DUH! Unauhakika hujachukia bado? Acha hizo , nisije nikakuchukiza bure!
Naacha, topiki imenishinda!
Siku njema! Lakini hebu tumcheki huyu jamaa akionyesha upendo kwa OBAMA
au labda tumcheki tu huyu Tembo akimuonyesha upendo Kifaru. Read more...
Labda UNAKUFURU kwa kumsifia HAYATI Mwalimu NYERERE ukikumbuka sifa za Ubinadamu. KWA KIBINADAMU ni vigumu kuona uwepo wa MTOTO bila mchango wa BABA na MAMA. Lakini....
Labda kwa upeo WA KIBINADAMU, ni vigumu pia KUONA uwepo wa NCHI FULANI bila mchango wa MTU FULANI. Lakini..... Binadamu ni MSAHAULIFU na ndio maana stori za MAREHEMU WOTE DUNIANI zikumbukwazo kuhusu MAREHEMU ni NUSUNUSU.
Inawezekana unachokumbuka kuhusu MAREHEMU ni KILE UTAKACHO KUKUMBUKA.
Ubinadamu pia unaweza kuchangia ujue UPANDE MMOJA wa kitu kimhusucho MAREHEMU. Pia inawezekana ujuacho kuhusu marehemu ni kile tu marehemu alichotaka ujue kuhusu yeye kwa kudhani ndio kitakacho kukusaidia au kukudhuru. Inawezekana WAKUSIMULIAO kuhusu marehemu HAWATAKI ujue kitu fulani au kwa mapungufu ya kibinadamu hata wao hawakumuelewa marehemu na ni asilimia kiduchu tu waijuayo kuhusu marehemu. Stori za wadaio kumjua marehemu zinaweza zikawa ni za ubunifu mzuri kutokana na WAPENDAVYO KUMKUMBUKA marehemu.
Swali:
Hujawahi kusikia watu au hata ndugu zako wakisimulia KW MOYO MKUNJUFU kitu kuhusu wewe , kitu ambacho unajua hakina uhusiano na wewe?
Unafikiri kuna mtu amjuaye mtu mwingine kwa uhakika?
Unakumbuka mambo asilimia ngapi kuhusu marehemu wa mwisho wewe kukutoka?
Unafikiri una muda kiasi gani cha kumjua mtu mwingine ?
SASAAAA....... ngoja niseme............
Aliyetutoka kwa kumuita MAREHEMU , twaweza kuwa tunakiri kuwa alikuwa BINADAMU.
Sifa mojawapo ya UBINADAMU ni MAPUNGUFU. ''Marehemu alikuwa MTU mzuri''; ni kauli maarufu MSIBANi au katika kumzungumzia KIPENZI aliyetutoka.
''Marehemu alikuwa MWANASIASA MBOVU''; ni sentensi inayoweza kuvumilika katika kumuongelea marehemu katika baadhi ya vikundi msibani kirahisi zaidi . SIASA nzuri kwa wengine si lazima iwe ni nzuri kwako.
Kuna sifa ambazo akipewa binadamu , kwa wenye kuamini MUNGU wataanza kukosa maana ya UPEKEE wa UWEZO wa MUNGU kama binadamu pia kwa akili yake anatatua na kuona mbele na anastahili sifa kipekee kwa uwezo wake binafsi usiohitaji msaada wa msuli wa MUNGU.
Kuna mambo asifiwayo MAREHEMU ambayo hutokana na UPUNGUFU wa KIBINADAMU wakustukia au kuweza kuona halihalisi bila mchango ambao MAREHEMU AMETOA.
Labda mchango wa MAREHEMU kukupeleka shule ndio umechangia tatizo lako la KUDHANI UNAJUA SANA ambalo litachangia kwenda kwako MOTONI siku ya MWISHO.
Labda mchango wa siasa za MAREHEMU ndio unaoendeleza tatizo lako la kibinadamu la kuamini kuwa binadamu wote si sawa hapa duniani kwa sababu wengine wanatokea nchi ya KIGAGAGIGIKOKO wakati wewe unatokea nchi ya PEMBA.
Labda marehemu anazidi kukuaminisha kuwa nchi zinamipaka hapa duniani na kuwa nyie ni wakarimu halafu wao sio.
Labda marehemu anasababisha TATIZO lako la kuongea KISWAHILI na kuchangia watoto wako wasivyojua KIHAYA kitu ambacho kinahakikishia baada ya miaka kadhaa hakuna atakayejua kuongea KICHAGA.
SASAAAAAAAAAA...
Mwalimu Nyerere hatuwezi kukana mchango wake kwa TANZANIA. Wote tunakiri kuwa alikuwa anaakili sana. Lakini kuwa na akili hakuna maana kuwa alikuwa anajua yote. Makosa yalifanyika kama yatakavyoendelea kufanyika na binadamu wote duniani. Na ni kweli binadamu yeyote mwenye busara na akili atakubali kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa Mjinga tu kama WEWE na MIMI. Swali Unafikiri kuna binadamu hata mmoja asiye MJINGA?
MUNGU amlaze mahali MEMA Mwalimu NYERERE!
Lakini.....
Labda tofauti kubwa kati yake Mwalimu Nyerere , MiMi na WeWe ni kwamba , wote tunajua alijitahidi kufanya kwa vitendo yale aliyoamini kuwa ni ya maana na ya msaada au MCHANGO mkubwa hapa duniani.
Lakini labda MIMI na wewe mchango wetu kwa nguvu ZETU zote kutokana na kaelimu kenyewe, kauwezo kenyewe na kaofisi kenyewe ka mabua tufanyiako kazi, ni kusaidia kuokota tu takataka pale mtaani naIKIWEZEKANA kujaribu KUUJAZA ulimwengu kwa kuzaa kwa mpango ,kujaribu kuelimisha taifa lijalo , watoto wetu au kumpa mimba mtoto wa tajiri ,ili angalau mtoto atokananaye na matendo yetu kwa kisingizio chochote kile AWE na afadhali katika maisha na awe mchango chanya katika DUNIA hii.
DUH! Swali:
Nchi ni nini?
Tanzania ni NCHI au jina jipya lililotungwa na BINADAMU kuwakilisha sehemu fulani?
Watu wa sehemu fulani wana mchango gani katika maana ya neno NCHI?
Naacha!
Tulia kidogo na Muheshimiwa katika jamii , MAREHEMU Richard Pryor akupe maneno ya hekima(usiangalie lakini kama unatafusiri ya matusi kichwani). Read more...
Inasemekana kula UGALI na MAHARAGE kila siku hukinaisha kama tu ukila PILAU au MABIRINGANYA kila siku.
Inasemekana kuwa baada ya kuchoka kula kiporo cha wali na maharage yalioungwa na nazi ya jana uyapendayo,vyakula vyote vitakavyofuatia vitakuwa vitamu na vitakusaidia unogewe tena na wali na maharage ya jana yalioungwa na nazi hapo siku za baadaye.
Lakini... Ukiongelea chakula, labda ni tofauti na ukiongelea binadamu. Inasemekana mapenzi ya binadamu na chakula , yanalemea upande mmoja, kutokana na chakula kutokuwa na kauli kuhusu jinsi gani kinafikiria ukilavyo au ujilambavyo.
Swali:
Katika mapenzi yako , umpendaye ana kauli zaidi ya kudai leo hajisikii vizuri kunanihii?
Unatumia kigezo gani kupenda chakula ambacho hutumii kulipenda LIMTU lako?
Utamu waKIMADA au LILE TU JAMAA ambalo JAMII , DINI au KAUBONGO KAKO kanakukataza KUONJA , kutokana na kukaaminisha KAUBONGO KAKO kuwa JAMII , DINI au KAUBONGO KAKO ni kautamu KALIKOKATAZWA, ni UTAMU tu ambao UBONGO wako unatafsiri kuwa ni tofauti kidogo na kautamu upatako kwa mke au mume wako.
Lakini.....
Si kweli kuwa LIKIMADA lako au LILE LIMTU lalo la nje ni tamu kuliko LIMTU lako LA NDANI.
Lakini......
Limtu la nje linaweza likasababisha unogewe zaidi na LIMTU lako la ndani, kama tu liwezavyo kufanya ukawa unalipa limtu lako la ndani mgongo ukilala na kudai kuwa umechoka wakati unalifikiria na kuliota limtu lako la nje.
Swali:
Sasa utajuaje UTAMU kama hakuna UCHUNGU?
Udhaifu wa binadamu ni pamoja na kuumia roho, wivu na ubongo kujifunza kitu baada ya kugusa moto. Ukigusa moto ukaungua , utataka kuufunza ubongo kukukumbusha usiguse tena moto. Ukionja tamu, utataka uufunze ubongo jinsi ya kupata tamu ili urudierudie kuonja tamu.
Cha kushangaza ni kwamba , ladha chungu unaweza kuufunza ubongo ukaona ni tamu. Ndio maana kuna wadaio kuwa walipoonja BIA mara ya kwanza waliona ni chungu ingawa leo wanadai ni tamutamu kunoga. Labda ndio maana afurahiaye MAZOEZI ukamwambia kuwa anachofanya ni ADHABU , atadai anaumia na haoni tamutamu ya mazoezi.
Swali:
Unafikiri Utamu ni nini?
Unafikiri WAKUBWA wazima wangapi wanaweza kuona maziwa ya MAMA ni MATAMU kama toto lilozaliwa tu na bila aibu linajua CHUCHU inatoa nini?
DUH!
Kama toto lilozaliwa tu linajua maziwa ya mama ni matamu, labda utamu hauhitaji kitu chakufananishia.
Lakini .....
Labda penzi la MUME na MKE linatakiwa liongezewe vikorombwezo kama tu toto linyonyalo liongezewavyo aina nyingine ya chakula jinsi siku zinavyoenda .
Lakini.......
Labda jinsi uongezeavyo vikorombwezo kwenye penzi lako na limtu lako ni sawa tu na jinsi toto uliongezeavyo milo mingine lifanikiwavyo kuongeza UJAZO wa MAVI na harufu ya kinyesi.
Lakini....... Labda WEWE na Penzi lako na LIMTU lako ni tofauti na YULE na LIPENZI lake, na kama upendavyo kubadili vitumbua na kula maandazi siku mojamoja au tisatisa, ndivyo YULE aridhikavyo na UJI wa MIHOGO kila siku.
Lakini....... Labda huwezi kabisa kufananisha mapenzi ya mtu na mtu na mapenzi ya mtu na chakula kama tu ushindwavyo kula mihogo huku ukilazimisha kaubongo kadhanie unakula keki.
Swali:
Unafikiri kuna kitu mtoto anafananisha dunia nacho kimfanyacho akizaliwa tu aanze kulia?
Si inasemekana ukiwa unajichua mwenyewe, kujirutubisha mwenyewe au hata unafanya penzi na usiyempenda, unaweza kujenga akilini picha ya umpendaye kama wafanyavyo baadhi ya MALAYA na siku moja moja unaweza kudakwa kwa kukosea jina la limtu lako kwa kutaja jina la kipenzi chako UKIPENDACHO kikweli MOYONI, AKILINI na ROHONI?
Sasaaa...
KUMBUKA nawaza tu HAPA , halafu Topiki imenishinda!:-(
Naacha basi!
Nakutakia kila la heri ambaye unajua utamu wa aina moja tu!
Nakutakia kila lakheri ambaye unajua tamutamu mbalimbali lakini tamu uliyonayo unaamini itakuwa inanoga hivyo hivyo kubwa kuliko kesho au hata kesho ya mwaka kesho.
Nakutakia kila la kheri ULIYEACHA tamu ya zamani ukidhani TAMU MPYA ni tamu kubwa kuliko na kugundua kuwa tamu ya zamani ndio ILIKUWA tamu HASWA na haipatikani kwa utamu ule tena.KIBEBA TAMU kimeshastukia HUNA MPANGO!:-(
YOTE MAISHA ! SI ndio UBINADAMU AU? BAADAYE BASI!
Nakuacha na zilipendwa kutoka South AFRICA kutoka kwa CHICCO akikuambia WE CAN DANCE
Au ngojea tu Professor Jay akuambie HAPO SAWA. Read more...
Labda ni mapenzi ya Mungu mimi na wewe hatujui! Labda ni mapenzi ya Mungu kuwa hakuna asiyeugua! Labda ni mapenzi ya Mungu wewe na mimi hatuna kile na tuna hiki.
Lakini utamu waulichonacho INGAWA UPO , labda unapatikana zaidi pale ukijua uchungu wakutokuanacho.
Kwa akili za kibinadamu , labda Mbinguni kunavutia kwa sababu tu unaamini au hata kujua kuwa duniani kunatesa au KUNA MAPUNGUFU. Na labda kama unanogewa na ya dunia, unaweza usivumilie UCHUNGU wa mbinguni ambao kwa wengine ni UTAMU.
Inawezekana kabisa kwa upeo wangu na wako wa kibinadamu kwa matumizi ya huu huu ubongo UTAFSIRIO kuwa CHIPSI MAYAI ni tamu, MBINGUNI KUNABOA.
Au......
Labda wanasayansi wanasema kweli kuwa mwili wa binadamu bila kusahau UBONGO wa BIN ADAMU ndio unatafsiri sana jinsi unavyojinoma au kuumia hapa duniani. Kemikali na homoni zinasababisha upende, unogewe au hata utake zaidi kunanihiii, bila kusahau jinsi MISHIPA ya FAHAMU(nerves) iunganishavyo UJUMBE MWILINI, mpaka unaweza kujisau kuwa utamu wa ngono, kutekenywa au hata chakula UKO kwenye UBONGO na sio kwenye sehemu zako za faragha, kwenye kidongoloso au kwenye ULIMI wako uutumiao kulamba nanihii.
Sasaaa......
Tunachojua ni kwamba, MIMI na WEWE tukifa, MWILI pamoja na UBONGO utarudi kuwa UDONGO. Inamaana karibu kila utumiacho , kupapasa , kuonja kuibia, mpaka kikusaidiacho kutafsiri kuwa wewe KIBOKO na mambo yako kwa tafsiri yako ni MSWANO , kitageuka KUWA udongo na labda kitakuwa kinarutubisha tu mazao fulani kama tu MBOLEA ya MAVI YA KUKU.
Lakini.......
Tunachosikia ni kwamba, binadamu ana ROHO . Tusichojua ni jinsi gani roho inatafsiri UTAMU au UCHUNGU ikiachana na hilo LIMWILI LAKO au LANGU ambalotunalazimika tulichambe baada ya kwenda HAJA KUBWA.!
Swali:
Unafikiri roho ya binadamu inajua utamu wa BIA, Ngono au utamu wa kumpiga mwenzio?
Kama wewe ni mwanamume au mwanamke , unajua uhusiano wa kutaka kwako sehemu za siri za wenzio ufanyikavyo UBONGONI na UONGEZEKO wa mjao wa damu katika sehemusehemu zako za faragha?
Lakini tusiyojua anajua MUNGU!
Narudia kinamna.........
Mapenzi ya binadamu matamu na yanaweza kukusaidia kupata GONO.
Kama wewe ni mwanasayansi utadai kuwa unajua kuwa kemikani na homoni zako ndio zinazosababisha uhisi utamu au uchukie kutokana na tukio.
Kama wewe unaamini katika sayansi utadai kuwa ni kemikali na hormoni mwilini na ubongoni ndio visababishavyo uingie ukichaa wa KULIPENDA na KUENDELEA kukaa na LIMTU LAKO ambalo limesababisha uone ni kitu cha kawaida na ni USAFI kugusanisha VIKOJOLEO VYENU ingawa unadai MKOJO ni uchafu na harufu ya mkojo unaichukia kama tu HARUFU ya SAMAKI MAREHEMU mwenye mafinyofinyo.
lakini.....
Utafiti wa mambo ya ubongo unaonyesha kuwa wale binadamu waitwao wanaakili sana au Majiniasi, bado wanatumia sehemu ndogo sana ya ubongo.
Na inasemekana watumiao UBONGO wakipata jibu la swali, huacha kumlaumu Mungu kwa hilo. Malaria huacha kuonekana kuwa anayeumwa kalaaniwa , wanampa Kloroquini au hata Muarubaini CHAUMBEA na anapona. Inawezekana pia anayeumwa kichwa akapewa tu dawa na bila ya watu kukumbuka kuomba Mungu amponye. Hata yule kibibi mwenye macho mekundu asingiziwaye uchawi kwa sababu jirani yake ana ukoma, husamehewa chanzo cha kuwa kwake na macho mekundu kijulikanapo, chanzo cha UTASA kijulikanapo kuwa si kweli KALOGWA ndio maana HAPATI MIMBA, na ni lidume lake NDILO linafyatua risasi tupu.
Swali:
Si inasemekana Mungu ndiye aliyeruhusu Magonjwa duniani kutokana na upotofu wa binadamu?
Ukisha muombea mtu apone kwa Mungu halafu akafa ingawa hukutaka afe, sini mapenzi ya MUNGU?
Lakini tusiyojua anajua MUNGU!
Binadamu ni kiumbe cha ajabu na kigumu kukielewa ujenzi wake kama tu SISIMIZI au MENDE na ujuzi wao wakustukia ulipoacha kiporo tamu tamu ingawa huoni pua zao.
Sawa basi.......! Labda ni kweli binadamu ndio kiumbe BAABU KUBWA kuliko MENDE ,kwa mtazamo wa binadamu, ingawa hata ndege wanatushinda kwa ujuzi wa Jiografia ya dunia. (Si unakumbuka kuwa ndege wamekuwa wanasafiri kutoka bara moja mpaka jingine kwa miaka kibao kabla hata binadamu hawajajua kuwa Dunia imegawanyika katika mabara na ni ya mviringo?)
Lakini........
MUNGU ni MKUBWA! Labda ndio maana mambo yakitushinda siye binadamu , tunadai kuwa ni MAPENZI ya MUNGU!
Na ni kweli MAPUNGUFU ya binadamu ni makubwa kiasi kwamba , BINADAMU kumuelewa BINADAMU mwenzie IMESHINDIKANA.
AU?
Swali:
Kama unaamini MUNGU anajua yote na amepanga yote, UNAUHAKIKA gani hajapanga kuwa MIMI na WEWE tutaenda jehanamu, kama unaamini kuna jehanamu?
Unapozungumzia mapenzi ya MUNGU , UNAUHAKIKA unayajua mapenzi ya BINADAMU?
Lakini tusiyojua anajua MUNGU!
Ila kama wewe huamini MUNGU, labda tusiyojua tutajua kesho!
Tatizo ni......
Hatujui kama tuna kesho.
Kwa hiyo, labda ndio IMETOKA HIYO ,kama hujui na wala hujaonja.
Na labda kama hujui na hujaonja ndio imetoka hiyo, kwani hautakuwa na kitu cha kufananishia kautamu au kauchungu upatako.
Kama hujawai kuonja vitu viwili na hauna cha kufananisha, labda ni kitu kizuri kama uambiwavyo kuwa SUBIRI mpaka UOE ndio UONJE WAKUBWA waonjavyo KWA KISINGIZIO cha KUTAFUTA MTOTO au kiburudisho.
Swali:
SI kuna dini maarufu zishaurizo kuwa UKISHAOA hakuna kuliacha hilo LIMTU katika SHIDA na RAHA, na kama ni maandazi na chai ni mwiko kutaka kuonja togwa kwa vitumbua?
Lakini tusilo lijua , ANALIJUA MUNGU!
Na kama kuna mbinguni , labda tujuavyo VITAKUFA na LIUBONGO hili lisababishalo tufikiri tunajua.
DUH! Naacha hii topiki!
Ngoja nikakague Nyati kidogo.........(usishuke mbugani kama mimi nilivyofanya lakini)
Asanteni tena WADAU! Baadhi ni hawa katika picha zangu ambao hamkunitenga.....
Starehe ya kumuangalia MNENGUAJI wa SEBENE katika Video ni kuangalia ANAVYOPEKECHA mpaka moto unawaka na SIO kuangalia AKIPEKECHA NUSUNUSU kwa sababu video ina kwamakwama.
Kwa mtafuta elimu isemekayo hutafutwa zaidi na WATUMIA internet Bongo na DUNIANI, watumiao GOOGLE kutafuta busara kwa kuandika nenokama; 'MATAKO, uke(kwa jina lake maarufu) , Uume (kwa kale kajina kake) au hata kwa jina la kitundu kitoleacho mabaki ya chakula katika mwili wa binadamu, mbele ya neno SEARCH, nafikiri elimu inanoga zaidi kama unachotafuta KITAKUJA Haraka au MARA MOJA mbele ya macho yako ili ukitolee macho, kuliko ukae kukisubiria huku ukiwa na wasiwasi na mtu aliyekaa kwenye komputa ya pembeni yako, asije akastukia kuwa unasoma BIBLIA , KORANI na sio staili za MIKAO kwenye KAMASUTRA.
Nacho jaribu kusema ni kwamba........
Internet Tanzania, kwa ujumla inakwenda mwendo wa KONOKONO(Very slow)
Internet Tanzania, bado ni ghali sana kwa mtu wa kawaida.
Unaweza kubisha!
Lakini, watumiaji wazuri wa internet Tanzania, wanatumia katika maofisi walikoajiriwa au wanakofanyia kazi. Kwenye internet cafe, labda kama ndio ofisi yenyewe au kwa adoado sana.
Kama huna Laptop yako na unategemea Internet cafe ,basi uwe na bahati sana kupata sehemu ambayo uki ''CLICK'' tu e-mail yako inafunguka bila kusubiria sana au kuanza kuangaika labda FIREWALL ndio inazingua kwanini hii picha KITOVU tu ndio kinaonekana, lakini huoni mpaka kule chini NJIA PANDA.
DUH!
Kwa ujumla......
Tanzania inazidi kuwa nchi ya ajabu kwa jinsi matabaka yanavyojengeka.
Sasa hivi unaweza ukajisahau kuwa uko Tanzania upande mmoja wa barabara kwa kusikia watu wanalalamika jinsi walivyokula PIZZA mbaya , halafu ukivuka tu barabara ukakuta wanao lalamika hawajui watakula wapi.
Kuna watakaokuambia kuwa ukitaka kuongea na watu watakaokuelewa , uende vijiwe fulani fulani siku hizi, hasa kama wewe ndio wale ambao moja ya tatizo lako, ni kujua nini kinaendelea New York , London au hata Beijing sasa hivi kama tu uangaikavyo kutafuta CIDER kwa sababu hupendi BIA Morogoro.
Unaweza kubisha! Hasa wewe ambaye unanisoma hapa kwenye net hivi sasa hivi, lakini Internet bado si jambo linalojulikana na hata kutumiwa na asilimia kubwa ya watu Tanzania.
Unaweza kubisha! Asilimia kubwa ya yaandikwayo kwenye net kuhusu Tanzania ni mambo ambayo hayawafikiii Watanzania walio wengi Tanzania.
Unaweza kubisha!
Kwa walalamikao kuwa wengi watumiao internet Tanzania hutumia kutafuta mambo ya sio kuwa na maana, ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya hao watu ni hao waitwao watu wa maana, wenye akili kama vile wanafunzi wa vyuo, walimu , maprofesa na wenye unafuu katika maisha . Na kama sikosei labda ni mimi na wewe ndio mabingwa wa kutaka kujua;'' hakuna picha za uchi za Rais kwenye net na wala sio hivi sera za Rais na Chama chake za kuendesha nchi zinatupeleka wapi. ''
Swali:
Haujawahi kutafuta picha za uchi kwenye net?
Hivi kutafuta maswala ya ngono kwenye net ni UJINGA?
Ukiandika mtandaoni unafikiri ni nani anasoma?
DUH!
Naacha topiki basi!
Ingawa cha kusikitisha ni kwamba ,hapa huwa napenda kuunga video kutoka YOUTUBE na kwa mmtandao bongo , KUFUNGUKA KWAKE, KAZI IPO.
Usinielewe vibaya! Tanzania BOMBA!
Usije ukadhani nalalamika tu kwa sababu CHUNGU inazidi TAMUTAMU . Tamutamu ni nyingi kuliko chungu Tanzania. Na naamini ni mimi na wewe tunaotakiwa kuendeleza kuongeza TAMUTAMU Tanzania.
UKWELI ni kwamba maswala ya INTERNET hapa bongo bado yanazingua !:-(
Naamini binadamu hupenda asikilizwe na ikiwezekana aeleweke. Bahati mbaya si wote tumebarikiwa KUJUA KITU na kuweza kufikisha ujumbe ukaeleweka na kukubalika.Ndio maana tuko wengi tunajua kuwa TUNAMPENDA na KUMTAKA yule NANIHINO, lakini jinsi yakumtupia KAULI au hata kumsababisha aje nawe migombani kwa hiari kulionja TUNDA , inakuwa SHUGHULI.
Labda ndio maana utasikia fulani kwa KUTONGOZA au mwanadada yule KWA......KIBOKO , kutokana na kuwa wengine siye, KAULI ZETU hazifiki kwa tumlengae, au zikifika, hazisababishi MTU MZIMA na akili zake aamue kuwa atakuvulia nguo, mpaka KIFICHA MBILIMBI wewe BINADAMU mwenziye BILA HAYA.
LOOOOH!
Swali:
Unauhakika ujumbe wako unataka umfikie nani?
Wewe kama Bloga unafikiri UJUMBE wako unamfikia nani?
Katika pitapita zangu ndani ya BONGO, hasa katika siku ambazo Rais KIKWETE anaongea, nimefanikiwa kugundua kuwa kuna matabaka mawili yanayo sikia tofauti kauli za huyu Mheshimiwa.
Kuna kundi la waitwao WASOMI na Kuna WASIOTAJWA JINA liashiriyo uhusiano wao na shule au masomo ya shule ambayo sio Elimu Dunia. (Sina maana kuwa kuna UKUTA unaotenganisha makundi haya mawili)
Mara nyingi Kikwete akiongea, nimestukia kuwa kuna ambao watadai kitu kama 'HE DOESN'T SOUND PRESIDENTIAL' na ambao watasikia , ' Umemsikia Kikwete mwenyewe kakuambia KABLA HUJALA lazima ULIWE!'
Kuna kitu ambacho naamini kuwa hata kama humpendi Kikwete inabidi ukichukulie maanani. JARIBU.... Ujiulize kuwa;
' Hivi KIKWETE akiongea, anaongea na nani na anayemlenga anafikiria nini?'
Je, anafikisha ujumbe atakao kwa anaowalenga?
Kabla sijaendelea...... ' Kuna Rafiki yangu KWEBA pale UHOLANZI alishanikalia kooni kuhusu swala hili, kwa kudai kuwa tokea niko TANZANIA, nimegeuka CCM kutokana na mtazamo wangu kuhusu Kikwete akiongea.'
DUH! Tuendelee....
Mimi naamini Kikwete ni Rais wa pili Tanzania baada ya Nyerere ambaye anajua jinsi ya kufikisha ujumbe wake kwa anaowalenga. Lakini KUMBUKA ANAOWALENGA INAWEZA KUWA SIO WEWE.
Na naamini kama wewe ni mwanasiasa Tanzania au tu ni Mtongozaji , jifunze kitu kutoka kwa Kikwete , hasa katika kuchagua unamlenga nani na kujua ni kauli gani utumie ili upewe kifuko cha DHAMBARAU.
Simsifii Kikwete, lakini, asilimia kubwa ya watu kwa uchunguzi wangu ambao wanampigia kura Kikwete , Kikwete anajua jinsi ya kuongea nao na kuwafikishia kauli au hata ujumbe ambao kawaandalia.
Naamini kabisa pamoja na kuwa Kikwete yuko ndani ya Mashine Kubwa iitwayo CCM , ila bado ni mtu ambaye akikupania kuja kukukopa unaweza kumpa pesa yako ya kodi ya mwezi ujayo kwa kuamini kuwa baadaye kidogo atairudisha.
Asilimia kubwa ya niliokuwa nawatolea macho na kuwadadisi ambao ndio wapiga kura , watakuambia , hakuna mwanasiasa ambaye amebakiza Uraisi/Raisi au amelikuwa Raisi, ambaye yuko hai Tanzania, ambaye anaongea lugha yao na wanamuelewa kuliko Kikwete hivi sasa.
Profesa Lipumba na wengine wengi , kuna watu kibao niliokutana nao na kuwasikiliza kutoka vijiwe vya kila aina vya watu wa kawaida ambao ndio wapiga kura ,watakuambia husikika kama MWALIMU FULANI ambaye unasubiri tu kipindi chake kiishe anaongea na anachoongea hakikuingii MUKICHWA.
Ndio kuna watu kama Kabwe ambao wanajua kulistukia kundi walilengalo na wakajua nini na kwa staili gani watafikisha ujumbe, lakini staili ya Kabwe imekaamkao wa kunoga ukiwa nje ya Mfumo . Inaweza ikawa ngumu Kabwe akiwa Rais Kabwe au kama tu Mchungaji Mtikila baada ya kamuda fulani kuongezea maji juisi.
KUMBUKA sijasema FIKIRA za Raisi KIKWETE zidumu, lakini nafikiri kuwa unaweza kujifunza kitu hata kama wewe ni mtaalamu wa mambo ya siasa hapo Chuo kikuu kwa kumsoma tu Kikwete Hata kama ni kweli hukubaliani na aidia ya RAIS MSHIKAJI!
Sina uhakika lakini kuwa wanasiasa Tanzania huwa wanatumia WATAALAMU au UTAALAMU katika kujaribu kuangalia kundi walitakalo na jinsi ya kulifikishia UONGO au huwa wanabahatisha tu .
Naanza kuamini Mchungaji Mtikila hatumii utaalamu ndio maana kwa navyojua uwezo wake WAKUFIKISHA UJUMBE ulivyokuwa mkubwa , UJUMBE wake hata kama ule wa chuki kwa aliowaita jina ambalo laweza kuchukuliwa kama tusi ,'MAGABACHORI 'hauwafikii tena walengwa na makali yake kutokana na KUBAHATISHA KWINGI , kutegemea sana HISIA na kutokuwa na kundi maalumu lilengwalo.
Sawa, unaweza kusema kuwa ukiwa mwanasiasa Tanzania ,WALENGWA wako ni Watanzania wote.
Lakini jiulize kitu ......
Unafikiri Watanzania wote ni sawa?
Unafikiri Kikwete anaathirika nyie wasomi mkidai kuwa anapigaalinacha na anaongea kama mtoto wa kijiweni tu ?
Unafikiri Watanzania waliowengi wanaelewa hata kuwa Rais ni timu na sio mtu mmoja?
Unafikiri Watanzania wangapi wana DATA ambazo zinaweza kuwajulisha kuwa unawadanganya hata UKIWA unajulikana kama Mengi na unadai utawajaza MAPESA?
DUH!
Ngojea niache hii topiki.
BAADAYE BASI!
Lakini kama unanguvu kidogo ......
Katika pitapita nilikutana na hawa Taifa la kesho... Mitaa ya Sinza Huyu Dogo aliniua kwa jinsi alivyo zama kwenye kitabu. Mpaka msamaria mwema akamuomba aende akasome nyumbani maana atagongwa na magari.
Mitaa ya Mikocheni.
Ndio, nilikuwa na Bajaji kama kawa.......
Nilifika Bagamoyo kwaJHIKOMANpia. Mpate kidogo akiwa nyumbani na marafiki.
Ilibidi niguse bahari kwa upande waBagamoyokiduchu pia.....
Nilikutana naOgola .-Holiday Inn
Michuzi -kwa Wachina akiwa na LadyJAYDEE
Lady Machozi Band
Agapiti
Magusa
Machozi Band
Swali:
Hivi unauhakika Profesa unayemuita Profesa anajua nini?
Ushawahi kukutana na Profesa mjinga?
Nakuacha na Talib Kweli akikupa kitu Hostile Gospel