Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama HUNA PESA ,jinunulie Mji wa GEITA kwa Kutumia PESA za DHAHABU ya GEITA.

>> Wednesday, October 08, 2008

MAAJABU ya Musa!
Geita tajiri , watu Masikini!


Kwa mji unaotoa mabilioni ya dola kwa dhahabu yake, utashangaa kuwa kuna watu wanashindwa kuwasomesha hata shule ya msingi watoto wao, maji ya shida na sana sana ni ya visima, umeme unasura mbaya kama TANESCO na barabara yenyewe ya kufikia huko ndio hivyo tena..

Labda hilo ni jambo la kawaida Tanzania. Lakini ukawaida wake utakuzingua ukijua kuwa wahusika wafaidikao na dhahabu ambao sio watu wa Geita, wamefanikiwa kuwa na maji yasiyo katika kutoka Ziwa Viktoria, umeme usio katika na barabara zenu hawatumii kwa sababu ndege na helkopta zipo.

Samahani kidogo!
Ngoja niangalie kidogo Geita!


Photobucket
(Baadhi ya sehemu ya barabara nzuri kuelekea Geita)



Sasaaaa...
Swali:

  • Inakuwaje viongozi wetu wakubali watu waje kuchimba madini hata bila ya kufaidisha maeneo wanayochimba madini?
  • Inakuwaje waweze kupitisha bomba la maji kwenda migodini na kuvuka mji ambao unamatatizo ya maji bila maji?
  • Inakuwaje hata wanasiasa washindwe kuweka mshinikizo kuwa angalau hata kama dhahabu inachukuliwa bila sisi kuhusika angalau basi hata barabara au hospitali iwe ni moja ya faida kwa wananchi wanaoibiwa dhahabu yao?


Sasaaaa....

Chakusikitisha ni kwamba, matokeo ya kuwepo kwa migodi ya dhahabu Geita, unaambiwa asilimia 10 -15% ya watu wana vijidudu vya UKIMWI. Na hiyo ni idadi ya ambao wameenda kupima. Kama unavyojua kuwa asilimia kubwa ya waendao kupima mdudu ni wale wahisio kuwa hawana mdudu. Wanaojihisi labda wameukumba tayari , huwa hawapi UKIMWI.

Swali:
  • Umepima UKIMWI?
Lakini.......

Naweza kukiri kuwa Geita mji na ni wilaya poa!
Watu wake poa sana!
Nahisi ni kwa sababu ni Watanzania ambao cha ajabu tumefikia kujisifia wenyewe kuwa siye ni watu poa sana na nchi yetu ni poa sana kuliko nchi yao.
Swali:
  • Hivi sifa si inanoga ukisifiwa na sio ukijisifia?
  • Hivi Watanzania tunajisifu tuna amani eeh?
  • Hivi unauhakika na mtu ajisifiaye mwenyewe kuwa babu kubwa , mzuri, anaakili sana au MJINGA kidoooooooogo?
  • Unauhakika anayekusifia anakigezo gani ambacho anakulinganisha nacho ili kujua wewe zaidi kiduchu katika kufanya nanihii au katika kunanihii?
DUH!

Ngoja nisicheleweshe kukuna kipele!!!!!!!

Geita ni tajiri.

Kwa wataalamu niliokutana nao ,wanakuambia kuwa ardhi ya geita ni dhahabu.
Mpaka sasa hivi kwa makadiro ya mtaalamu mmoja niliyeongea naye kwa kina , anakuambia kuwa, akipatikana mwenye pesa ya maana , mji wa Geita unaweza kuhamishwa kwa sababu uko juu ya dhahabu.

Mpaka sasa kuna migodi ya aina mbili Geita.
Mgodi ambao unachimba juu kwa juu(hakuna mahandaki) na mgodi unaochimba chini kwa chini. Sasa unaambiwa unaoingia chini kwa chini lazima utaingia mpaka mjini Geita kwa chini, kitu ambacho kitasababisha Mji usijengeke kwa juu au baadhi ya nyumba kudidimia ardhini .

Swali:
  • Ushastuki sasa kuwa kugombea UBUNGE GEITA ni DILI ?
  • Unafikiri ni kwanini wajanja kutoka nchi kibao ambao wanamamilioni wanakwenda Geita maporini ?
  • Wewe na mimi tuko Mwanza mjini au Dar?

Chakusikitisha!

  • Ukifika Geita, huwezi kuamini ndiko dhahabu inatoka.
  • Ukifika Mererani Arusha, hutaamini kuwa ndiko Tanzanite inatoka.
Bado kidogo nami nianze kukatatamaa na kuanza kuamini kama wasemao:'AMA KWELI sehemu zenye utajiri HAZITAJIRIKI.'

Swali:
  • Hivi Tanzania ni nchi masikini eeh?
  • Unajua unaweza kuinunua Mererani kwa pesa za Tanzanite, kama vile unavyoweza kuinunua Tanzania kwa pesa ulizovuna Tanzania ,mbele ya macho ya Watanzania?
  • Hivi Watanzania ni wajanja kwa sababu wana Kiswahili Mingi?

Duh!
Basi Bwana!
MIMI na WEWE, na labdaYULE ndio WATANZANIA wenyewe, ambao labda ndio kwanza bado tunahangaikia chakula kwanza tushibe. Hatujavuka hata katika kutatua tatizo la kuwa na uhakika wa chakula mezani .

DUH!:-(

Usitishike lakini!
Naamini wewe ushastuka kama mimi!
Fanyiakazi basi kuondoa kiini macho.

AU?
Duh!

Ngoja nirudi Mwanza kwa shingo upande hivyo hivyo mikono mitupu au angalau kwa picha......:-(

Photobucket
Ndani ya Lake Victoria

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket
Hapa ndipo TEPANYAKI ndani ya TILAPIA ukitaka kula kijapani ndani ya Mwanza
Photobucket
Kiki ndani ya Tilapia

Photobucket

Photobucket
TILAPIA.( Picha kutoka katika Pool Bar ambako hukawii kugongana na wachukua Dhahabu za Geita ambao barabara zetu mbovu hawajawahi kuzitumia .)

Ngoja nimuache SEAL atupe kile kibao alicho kikarabati cha SAM COOKE A Change is Gonna Come

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Egidio Ndabagoye 5:07 pm  

Huwa nafikiri hawa watawala wetu akili zao zi wapi,wameshikiwa akili zao.Nenda Mererani kunatia huruma.

Nina swali,sisi wanyonywaji tufanye nini?

Mwanza panapendeza mandhari mazuri chakula safi,watu wema.Nasikia wadada wa kisukuma poa sana full adabu tatizo mahari yao kimbembe.

Egidio Ndabagoye 5:08 pm  
This comment has been removed by the author.
Simon Kitururu 12:17 am  

@Egidio: Kazi Ipo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP