Kama mpaka MUNGU wa UPENDO ANACHUKI , usinidanganye kuwa una UPENDO tu MOYONI kwa kale KAKITU au YULE FALA!
>> Wednesday, October 15, 2008
Swali:
- Chuki ni nini?
- Unafikiri Mungu wa Upendo hana CHUKI?
Upendo wako LABDA unaashiria kuna kitu UNACHUKIA.
Upendo wako unaashiria kuna kitu chenye uhusiano na ukipendacho ambacho UNAKICHUKIA.
Upendo wako wa vita kama tu nyege yako ya kumfunza adabu NANIHIINO, kuna umlengaye na si kweli kuwa itaondolewa UKAME kwa kumpiga yeyote tu apitaye mbele yako.
KUNA umCHUKIAYE, kuna ukichukiacho ambaye au ambacho ndio kipele kikuwezeshacho kugundua siri ya utamu wa UKIPENDACHO.
Labda itabidi tu ufurahie chuki kwa kukuokoa kutoka katika maisha yakutojua Upendo ni nini.
Labda tushukuru kwa kuwa Binadamu kwa sababu UBINADAmu unatusaidia kushindwa kuelewa hata mapenzi ya MUNGU wa UPENDO awezaye yote aachiapo tuwapendao wateseke na tuwachukiao wawini MAISHA au hata sehemu za siri za tumtamaniye.
Mwenye chuki na MTU au hata CHUPI , ni rahisi kufananishwa na BINADAMU MBAYA.
Mtu mzuri anafananishwa na matendo mengi watu waaminiyo ni matendo mazuri kama vile UPENDO au UKARIMU hatakama matendo hayo yanaweza kukuzawadia UKIMWI.
Binadamu huongelea, husifia upendo na amani mpaka anaweza akasahau kuwa mara nyingi ni chuki na vita vilivyomgundulisha starehe moyoni.
Hakuna binadamu asiye na chuki na kitu fulani kama sio chuki kwa MLENDA au LISURA lako ambalo kuna baadhi ya binadamu au hata mbwa waonyeshao dalili ya kulipenda au walisifialo kuwa zuri.
Tusitake kujidanganya.....
Kwa wakristo watakustua kuwa Yesu wa upendo alikuwa anachukia kama kwa Waislamu , Mtume Mohamedi alivyokuwa anachukia .
Wale Miungu wengine ambao baadhi wanasaidia mpaka akina NANIHINO kupaa na ungo pia nasikia wakichukia, hata mvua hazinyeshi pale kijijini kwetu.
Swali:
- Si ni kweli Mungu wa upendo alianza kuchukizwa na vitendo vya binadamu tokea ADAMU na HAWA?
Sasaaa.....
Unauhakika gani kuwa unajua UPENDO ikiwa tafsiri ya UPENDO wa kibinadamu labda wala haifanani na Mungu amaanishavyo kwa neno UPENDO?
SWali:
- Unauelewa upendo wa Mungu kama huelewi Mungu muweza yote kuachia uwepo wa chuki?
- Unauhakika unauelewa upendo wa MUNGU kama upendo wako mwenyewe unategemea CHUKI?
DUH!
Unauhakika hujachukia bado?
Acha hizo , nisije nikakuchukiza bure!
Naacha, topiki imenishinda!
Siku njema!
Lakini hebu tumcheki huyu jamaa akionyesha upendo kwa OBAMA
au labda tumcheki tu huyu Tembo akimuonyesha upendo Kifaru.
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Lakini nani ana hakika kuwa mungu anatupenda na kwa nini tunaamini ya kuwa mungu anatupenda? Je kuna mru alimsikia? Kwa sababu kama mimi nikisema nakupenda wewe inajulukana nakuona na wewe unaniona lakini sasa utakipendaje kitu/mtu usiyemwona? Ni fikra zangu tu?
@Yasinta:Ndio maana walokolo wakikuombea watakuambia KWA imani utatapona.
najua nguja nikuchekesha au nikupe hii ni rafiki mmoja aliniambia hivi mwamini yesu na mwambie akuponye. Yesu anaweza kuponya ukimwamini. nikamwambia siwezi kumwani yesu wakati sijamwona. alicheka sana
Yasinta habari za siku? Hongera kwa bidii unayoonyesha. Wewe unasimama kuwa mfano wa wnablogu wanaounganisha blogu moja mpaka nyingine kwa kuaca maoni. Hongera sana.
Kinachojitokeza katika mjadala ni suala la imani. Kwamba je, kuna maana yoyote kuamini kitu bila ushahidi? Je, ni kweli tunaishi kwa kutegemea ushahidi katika kila jambo?
Sababu ni kwamba, nionavyo mimi ni kwamba sehemu kubwa ya mwenendo wa maisha yetu inaongozwa na mambo ambayo hatuna ushahidi nayo. Mambo ambayo hatuna hakika kama yapo kama tunavyodhani. Mambo ambayo, pamoja na kufanyika kama sehemu kamili ya maisha yetu, bado hatuwezi kujua ilikuwaje tukayaamini. Kumbe nataka kusema nini?...Imani ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.
Kwamba ukuaji wa binadamu hauwezi kukamilika bila kuhusisha suala hili la kuamini pasipo ushahidi. Na Saikolojia inaenda mbali kwa kudai kwamba kutokuamini ni kilema kama vilema vingine.
Sasa kwamba Mungu ana chuki mimi sina jibu la moja kwa moja. Kwa sababu miungu wenyewe wapo wengi na wana tabia tofauti tofauti.
Ukisoma habari za mungu aitwaye alah utaona kuwa madai yake ni tofauti kabisa na pengine yana pingana na mungu Yehova. Sasa mwenye hasira ni yupi hapo sina jibu.
Niliwahi
Post a Comment