Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MTAZAMO wa maendeleo ya TANZANIA kwa kutembelea CHOO au VYOO ndani ya TANZANIA!

>> Tuesday, October 07, 2008

Sehemu za kutunzia kinyesi au kupunguzia LITA au kwa JINA maarufu ``CHOO´´, chaweza kukunong'oneza kitu kuhusu watumiaji wa faragha hizo hata kama watumiaji hutumia sehemu za kuheshimika hizi kwa matumizi ya kujamba tu. (Samahani kwa kutumia lugha chafu kama neno kujamba, ninamaanisha kutoa hewa inayonuka.)


Lakini.....

Sehemu babu kubwa yenye choo kichafu , hakina maji au hata makokoneo, kinaweza kuwakilisha nini wamiliki wa sehemu au waendao sehemu wanaona ni muhimu.Ingawa ni kweli kinaweza kuonyesha tu hali halisi ya ugumu au uhadimu wa kupatikana vitu fulani kama maji ya kutawadhia, debe la kutupia takataka au majivu ya kusaidia mambo fulani katika choo cha shimo, wakati Kitimoto, Bia fulani, Konyagi, Bavaria,Festival,Savanna, John Walkers......... mpaka Shampeni zipo kwenye shelfu kwa sababu ndio biashara yenyewe.

Sibishi !
Tanzania inaendelea!

(Mimi na wewe si ndio Watanzania wenyewe)


Lakini bado Tanzania kuwa na kitambi , kwa mtazamo wa wengi ni mali na sio tatizo la kiafya !
Kwa haraka haraka, nina maana .....

  • Bado KULA au KUWA NA CHAKULA ni ujanja na sio kitu cha uhakika
  • Bado tunatishana kwa muonekano.
  • Bado ukiendesha Benzi na hauna kitu benki au hata pesa ya mafuta, unaweza kuopoa ngoma kuliko ukiwa na pesa ya benzi na unapakia Bajaji.
  • Bado wewe unavutia kwa muonekano wa vazi la nje ingawa chupi chafu halafu imechanika kidooooogo.
Swali:
  • Hivi mimi na wewe tumeendelea?
Samahani kidogo!
Hebu nikuwekee baadhi ya picha za Mabloga wa Kibongo niliokutananao hivi karibuni.....
Photobucket
Mzee wa Rundugai Samaki Samaki -Mlimani City
Photobucket
Araway Kikaho Kwa Mama Perina -Morogoro

Photobucket
Photobucket
Rasta Luihamu na Mzee wa Rundugai Samaki Samaki -Mlimani CITY
Photobucket
michuzi Ofisini
Photobucket
Nikiwa na Mkuu wa Wilaya- Breakpoint katikati ya Muji

Photobucket

Rasta eeh! Nakusikiliza. Mlimani City
DUH!

Tuendelee....

Lakini sitaniii!

Matumizi ya SIFA za nguvu za akili , busara, ufanyajikazi bora, tabia nzuri, mpenda amani , sio mwizi nk, unaweza kuyashinda kwa Matumizi ya SIFA zitokanazo na unavaa nguo gani , unaendesha gari gani, unapesa bila mtu kujua unazipataje na unawatishia watu maisha kwa staili za amri zako uzitumiavyo kujihakikishia unastahili heshima.

SAMAHANI KIDOGO!
Hebu tuwacheki kidogo hawa simba niliowafumania maeneo walivyo kuwa na uhakika.Hawahitaji kukutisha ili uwaheshimu.



Photobucket

Photobucket


Sasaaaa........

Swala la chumba kipi kiwe kisafi zaidi katika nyumba chaweza kukusababishia ukasafisha zaidi chumba chakulia chakula zaidi kuliko jikoni chakula kipikiwako kwa sababu unaamini wageni hawafiki huko.

Lakini.....


Labda ni UKWELI ukiwa na njaa, cha muhimu ni chakula tu .
Maswala ya utaenda choo wapi huwa ni mbele kwa mbele au ni mambo ya baada ya kula.
Labda hata pale nyuma ya mlango wa nyumba ya jirani kama kuna giza, panaweza kufaa katika matumizi ya kushusha kilo au hata lita ukidhani hutashikwa chupi haijasitiri.

Lakini nisikuzingue!.............

KWA kifupi sehemu nyingi ziitwazo BAABU KUBWA Bongo, bado zinatimiza haja za mwenye njaa na hazijafikia kujali Mwenye Njaa akishakula atakwenda haja wapi.

Unaweza kunibishia , lakini naamini asilimia kubwa ya waitwao matajiri Bongo , bado wana tabia za wenye njaa. Mwenye njaa asiye nauhakika na tajiri mwenye uhakika unaweza usiwatofautishe kutokana na kufanana kwao kisaikolojia. Utakuta tajiri mzima naye hajiamini, aliyeelimika(tajiri wa elimu) naye hajiamini. Atataka kukutisha akijua unatishika na hakuna kujiamini ambako kunaweza kumfanya asione sababu ya kukutisha kwa sababu anajua hauwezi kumfanya kitu kwa sababu wewe huna. Mwenye nacho anaweza akawa anashindana na wewe usiyenacho ili tu ajisikie kuwa anacho badala ya kwenda hatua ya mbele itakayo mfungulia yeye mambo mengine na kukusaidia usiyenacho kuvuta hatua mbele badala ya kupiga makitaimu.

Mimi na ogopa utajiri wa GARI KUBWA, SEBULE SAFI chooo KICHAFU!:-(
Swali:
  • Kama matajiri bongo wanatabia za wenye njaa unafikiri masikini wenye njaa wawe na tabia gani?
  • Au mwenzangu unaweza kutofautisha tabia za tajiri mwenye njaa lakini anauhakika na kula na masikini mwenye njaa na asiye na uhakika na kula ndani ya bongo ,ukiwakuta wanawania ubwabwa?

Samahani turudi kwenye Choo....

Kirahisi sehemu ambazo tokea maili kumi zinaonyesha kuwa Mafisadi hawaendi hapo, basi uwe na uhakika kuwa unaweza kupata matatizo ya uchambie nini au hata utumie staili gani ya kupunguza kilo kama sio lita . Na ukitoka huko msalani ,sina uhakika utanukia a pafyumu gani kwenye vazi au puani.

Swali:
  • Ushastukia kuwa harufu mbaya inaweza kukuganda puani tu mpaka ukafikiri unanuka kichoochoo mwili mzima na kumbe bado unanukia manukato?
  • Hivi akinadada wastaarabu waendao sehemu babu kubwa walioko kwenye hedhi mnakumbukwa hata huko katika vyoo vya sehemu baabu kubwa sehemusehemu za kuhifadhi mambo ya kikubwa ya kike baada ya kubadilisha?(Naamini sehemu nyingi meneja ni mwanamume ambaye labda hajawahi hata kuona chupi ya dada yake imeanikwa)
Swali jingine ngojea nimuulize George W Bush

DUH!

Tuendelee.........au tuanze upya.......


Kama umezoea choo cha kukaa ukienda cha shimo, unaweza ukawa na matatizo ya kulengesha nanihii! Na labda miguu itakuuma.

Kwa Mtanzania Mweusi kama MIE, kama umezoea kuwa wengine ndio wanavyo, wanajua na wanastahili, hutashangaa kujikuta unashuhudia tu wenzako nyumba ya jirani wanavyojinoma katika mambo wewe uhisiyo kuwa hustahili kwa sababu zako fulani kama vile sehemu yenyewe ni kwaajili ya wenyenazo na labda hata Watanzania Wazungu au Wazungu Wazungu, hapo ikiwa kama umeshawazoeaWatanzania Wahindi,Wahindi , Watanzania Waarabu,Waarabu au WatanzaniaWachina, Wachina , ambao kuna maeneo mengi ndio wanaaminika kuwa wanavyo, wanaweza, au hata kustahili.

Utasikia kuwa bongo ni Tambarare kwa watu fulani!
NI KWELI HIYO!

Lakini muonekano wa utambarare wa bongo unastaili zake.
Bado kwa mengi ambayo utayaita ni tambarare , yuko atakayeona ni sawa tu na kuona hoteli nzuri lakini choo kichafu na hakuna maji! Hasa kutokana na mapungufu ambayo yanatatulika kama watu watakuwa makini kukuna muwasho kwenye kipele.

Tatizo ni kwamba ni MIMI na WEWE tunaohitajika katika kutatua na wala sioYULE
:-(


KAZI IPO!
USICHUKIE!Mimi nawaza tu hapa MKUU, kinamna!

Pata kidogo picha nyingine zangu na wadau kinamna kama hujali .
Samahani lakini!
AU?

Photobucket
Papa manento

Photobucket

Photobucket
Rose Garden hapa. FJ unakitenga kijiwe hiki lakini!

Photobucket

Photobucket
Maisha Club na Muzee Tiba...

Photobucket
Rasta Haji -Rock Garden
Photobucket
Mimi na Kaka zangu

Photobucket
Merinyo- Africa Sana

Photobucket
Bro Davie na Luta


Baadaye Basi!

Twende South Africa kidogo tujikumbushe mambo na Mzimbabwe/Mzambia/Msauzi DOROTHY MASUKA katika tamutamu ya zilipendwa iitwayo..Kwa Nhingirikiri

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Egidio Ndabagoye 4:53 pm  

Dah naona watu wanazidi kunenepa ile mbaya.Araway kaka ingia gym sasa.
Simon,hiyo ni safari ya mbuyu au msonge?

luihamu 7:19 am  

AMANI KAKA.

chemshabongo 6:12 pm  

ndambagoye wacha bwana mbona kawaida. alafu hata muda wa hiyo gim sitaupata kaka.

Simon Kitururu 12:19 am  

@Egidio: :-)
@Rasta: Amani iwe nawe pi
@Chemshabongo: Naona unajitetea:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP