Busara nyuma ya JINSI ya KUVUA NGUO au AKILI za WADHANIAO wengine WAKO UCHI!
>> Wednesday, October 29, 2008
LABDA aliyeko uchi ndio Mwenye akili na busara,ingawa wengi watadai aliyevaa nguo ndio mwenye busara na hekima na labda ndio mwenye kujiheshimu.
Cha ajabu ni kwamba , amchekaye au kumdharau aliye uchi anaweza akawa hajawahi kujiuliza ni nini busara za avaavyo na je ni akili kuweka umuhimu wa herufi kubwa mpaka umfanye avae avaavyo.
Lakini.....
Aliyeko uchi anaweza akakuvutia au kukutisha kutokana na tafsiri za ubongo wako.
Kuna mpaka WAAFRIKA na hata WADUNIA bwelele wadaio wakiona hasa akina dada hawajafunika vichochoro fulani vya mwili hudai kuwa si utamaduni wa AFRIKA.
Swali:
- Ushawahi kufuatilia utamaduni wa kiafrika wa kukaa uchi?
- Unafikiri ni kwanini Wachungaji/mapadri wa makanisa fulani wanavaa magauni/majoho?
- Unauhakika na spidi yako ya kuvaa ukihisi unapigiwa chabo?
- Unakumbuka ukubwa wa AFRIKA na tamaduni za uvaaji za kiafrika?
Tamaduni kibao zimetuletea nini cha kuvaa na jinsi ya kuvaa.
Tamaduni karibu zote duniani zinakubaliana katika kuvalisha sehemu za faragha tu au VIJIUKE na VIJIUUME tu.
Mambo ya kuficha kwingine , ni wajanja wameamua na jamii karibu zote zinatofautiana katika umuhimu wakuvalisha nguo matako au hata miguu ,kitu kitakacho kufanya ukose starehe ya kuwa na magaga miguuni.
Maridadi mengine yote yakuficha SEHEMU nyeti kama mikono na hataMATITIya WANAUME yametokana na tafsiri za jamii zenyewe kwa kusaidiwa na hali ya hewa na hamu zao za kibinadamu kama sio imani ambazo mara nyingine hazina ukweli.
Lakini.......
Kama unakumbuka siku ulioanza kufikiria kuwa UNAHITAJI kuvaa nguo, wewe BOMBA la mtu.
Lakini ....
Baada ya kuzaliwa tu kuna walioanza kufikiria kukuvalisha nguo.
Na labda....
Mpaka sasa hivi unapendeza sana tu kama shetani!
Swali:
- Unafikiri kwa nini kuna baadhi ya binadamu wanataka kupendeza?
- Unapovaa nguo unafikiri zinasaidia zaidi kuficha ulivyo mbaya uchi au ni kweli unazihitaji kama kisitiri utu?
Kitendo cha kuvalishwa nguo au kufunikwa tokea uzaliwe ,kinaweza kuwa ndio chanzo chako cha kufikiri nguo zinaumuhimu hata usiokuwepo.
Tatizo ni...
Labda bado unavalishwa nguo kwanamna maradufu bado, ingawa unadai hutaki kuchunguliwa ukivaa hilo linguo lako usingizialo kuwa linakusitiri na labda ni kweli linakusitiri ingawa tunaona nanihii kwa mbaaaali!
Tatizo ni....
binadamu mwenye akili bado anaweza kuvalishwa ligwaguro ingawa kanzu haikuhitaji chupi na joto hili.
Pamoja na nguo kuweza kukusitiri au kuficha nanihii, makende au hata kibiongo, inaweza ikawa inatumika kukuficha tu kujua kuwa matumizi yako ya nguo kufunika kila mahali ni matumizi mabaya ya vitambaa.
Swali:
- Ushawahi kufikiria kwanini unafikiria unavyofikiria ukiona aliyeuchi?
- Hivi kweli kukaa nusu uchi si utamaduni wa KIAFRIKA?
- Hivi unakumbuka kuwa vichaa asilimia kubwa hawatembei UCHI?
Inawezekana ni ujinga kutumia akili kutetea kitu chochote kiitwacho utamaduni , mila au desturi zifanyazo ukose uhuru kwa kitu cha mpito kama tu staili za kufunika utupu wa binadamu aliyezaliwa uchi.
Labda kidumucho katika vazi la binadamu ni kuwa uchi.
NAACHA MKUU na nakutakia kila la heri katika BUSARA zako za kuvaa na kuvua!
NAWAZA TU HAPA mkuu USIGUNE basi!!
Ngojea basi tujifunze kutoka katika BUSARA za tamaduni au kutoka kwa MAKAKA tumbo moja wawezao na kujua utamu wa kuoa mke mmoja au FRATERNAL POLYANDRY.
Au labda AMY SEDARIS afundishe kuhusu uoshaji wa uke au labda anatania.
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
nafurahi umerudi kwani ulikuwa kimya kidogo asante kwa mafundisho. kazi njema
@Yasinta:Asante pia kwa kuzidi kunitembelea!
Post a Comment