Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI unamkumbuka na KUMUOMBOLEZA Mwl Nyerere, UNAUHAKIKA hakuwa MJINGA?

>> Tuesday, October 14, 2008


Labda UNAKUFURU kwa kumsifia HAYATI Mwalimu NYERERE ukikumbuka sifa za Ubinadamu.
KWA KIBINADAMU ni vigumu kuona uwepo wa MTOTO bila mchango wa BABA na MAMA.
Lakini....

Labda kwa upeo WA KIBINADAMU, ni vigumu pia KUONA uwepo wa NCHI FULANI bila mchango wa MTU FULANI.
Lakini.....
Binadamu ni MSAHAULIFU na ndio maana stori za MAREHEMU WOTE DUNIANI zikumbukwazo kuhusu MAREHEMU ni NUSUNUSU.

Inawezekana unachokumbuka kuhusu MAREHEMU ni KILE UTAKACHO KUKUMBUKA.

Ubinadamu pia unaweza kuchangia ujue UPANDE MMOJA wa kitu kimhusucho MAREHEMU.
Pia inawezekana ujuacho kuhusu marehemu ni kile tu marehemu alichotaka ujue kuhusu yeye kwa kudhani ndio kitakacho kukusaidia au kukudhuru.
Inawezekana WAKUSIMULIAO kuhusu marehemu HAWATAKI ujue kitu fulani au kwa mapungufu ya kibinadamu hata wao hawakumuelewa marehemu na ni asilimia kiduchu tu waijuayo kuhusu marehemu.
Stori za wadaio kumjua marehemu zinaweza zikawa ni za ubunifu mzuri kutokana na WAPENDAVYO KUMKUMBUKA marehemu.

Swali:

  • Hujawahi kusikia watu au hata ndugu zako wakisimulia KW MOYO MKUNJUFU kitu kuhusu wewe , kitu ambacho unajua hakina uhusiano na wewe?
  • Unafikiri kuna mtu amjuaye mtu mwingine kwa uhakika?
  • Unakumbuka mambo asilimia ngapi kuhusu marehemu wa mwisho wewe kukutoka?
  • Unafikiri una muda kiasi gani cha kumjua mtu mwingine ?


SASAAAA....... ngoja niseme............

Aliyetutoka kwa kumuita MAREHEMU , twaweza kuwa tunakiri kuwa alikuwa BINADAMU.

Sifa mojawapo ya UBINADAMU ni MAPUNGUFU.
''Marehemu alikuwa MTU mzuri''; ni kauli maarufu MSIBANi au katika kumzungumzia KIPENZI aliyetutoka.

''Marehemu alikuwa MWANASIASA MBOVU''; ni sentensi inayoweza kuvumilika katika kumuongelea marehemu katika baadhi ya vikundi msibani kirahisi zaidi .
SIASA nzuri kwa wengine si lazima iwe ni nzuri kwako.

Kuna sifa ambazo akipewa binadamu , kwa wenye kuamini MUNGU wataanza kukosa maana ya UPEKEE wa UWEZO wa MUNGU kama binadamu pia kwa akili yake anatatua na kuona mbele na anastahili sifa kipekee kwa uwezo wake binafsi usiohitaji msaada wa msuli wa MUNGU.

Kuna mambo asifiwayo MAREHEMU ambayo hutokana na UPUNGUFU wa KIBINADAMU wakustukia au kuweza kuona halihalisi bila mchango ambao MAREHEMU AMETOA.

Labda mchango wa MAREHEMU kukupeleka shule ndio umechangia tatizo lako la KUDHANI UNAJUA SANA ambalo litachangia kwenda kwako MOTONI siku ya MWISHO.

Labda mchango wa siasa za MAREHEMU ndio unaoendeleza tatizo lako la kibinadamu la kuamini kuwa binadamu wote si sawa hapa duniani kwa sababu wengine wanatokea nchi ya KIGAGAGIGIKOKO wakati wewe unatokea nchi ya PEMBA.

Labda marehemu anazidi kukuaminisha kuwa nchi zinamipaka hapa duniani na kuwa nyie ni wakarimu halafu wao sio.

Labda marehemu anasababisha TATIZO lako la kuongea KISWAHILI na kuchangia watoto wako wasivyojua KIHAYA kitu ambacho kinahakikishia baada ya miaka kadhaa hakuna atakayejua kuongea KICHAGA.

SASAAAAAAAAAA...


Mwalimu Nyerere hatuwezi kukana mchango wake kwa TANZANIA.
Wote tunakiri kuwa alikuwa anaakili sana.
Lakini kuwa na akili hakuna maana kuwa alikuwa anajua yote.
Makosa yalifanyika kama yatakavyoendelea kufanyika na binadamu wote duniani.
Na ni kweli binadamu yeyote mwenye busara na akili atakubali kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa Mjinga tu kama WEWE na MIMI.
Swali Unafikiri kuna binadamu hata mmoja asiye MJINGA?

MUNGU amlaze mahali MEMA Mwalimu NYERERE!


Lakini.....

Labda tofauti kubwa kati yake Mwalimu Nyerere , MiMi na WeWe ni kwamba , wote tunajua alijitahidi kufanya kwa vitendo yale aliyoamini kuwa ni ya maana na ya msaada au MCHANGO mkubwa hapa duniani.

Lakini labda MIMI na wewe mchango wetu kwa nguvu ZETU zote kutokana na kaelimu kenyewe, kauwezo kenyewe na kaofisi kenyewe ka mabua tufanyiako kazi, ni kusaidia kuokota tu takataka pale mtaani naIKIWEZEKANA kujaribu KUUJAZA ulimwengu kwa kuzaa kwa mpango ,kujaribu kuelimisha taifa lijalo , watoto wetu au kumpa mimba mtoto wa tajiri ,ili angalau mtoto atokananaye na matendo yetu kwa kisingizio chochote kile AWE na afadhali katika maisha na awe mchango chanya katika DUNIA hii.

DUH!
Swali:
  • Nchi ni nini?
  • Tanzania ni NCHI au jina jipya lililotungwa na BINADAMU kuwakilisha sehemu fulani?
  • Watu wa sehemu fulani wana mchango gani katika maana ya neno NCHI?

Naacha!

Tulia kidogo na Muheshimiwa katika jamii , MAREHEMU Richard Pryor akupe maneno ya hekima(usiangalie lakini kama unatafusiri ya matusi kichwani).

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP