Ni starehe KUANGALIA video/picha za NYUCHI au taarifa za MJUMBE wa NYUMBA kumikumi kwenye INTERNET Tanzania?
>> Friday, October 10, 2008
Starehe ya kumuangalia MNENGUAJI wa SEBENE katika Video ni kuangalia ANAVYOPEKECHA mpaka moto unawaka na SIO kuangalia AKIPEKECHA NUSUNUSU kwa sababu video ina kwamakwama.
Kwa mtafuta elimu isemekayo hutafutwa zaidi na WATUMIA internet Bongo na DUNIANI, watumiao GOOGLE kutafuta busara kwa kuandika neno kama; 'MATAKO, uke(kwa jina lake maarufu) , Uume (kwa kale kajina kake) au hata kwa jina la kitundu kitoleacho mabaki ya chakula katika mwili wa binadamu, mbele ya neno SEARCH, nafikiri elimu inanoga zaidi kama unachotafuta KITAKUJA Haraka au MARA MOJA mbele ya macho yako ili ukitolee macho, kuliko ukae kukisubiria huku ukiwa na wasiwasi na mtu aliyekaa kwenye komputa ya pembeni yako, asije akastukia kuwa unasoma BIBLIA , KORANI na sio staili za MIKAO kwenye KAMASUTRA.
Nacho jaribu kusema ni kwamba........
- Internet Tanzania, kwa ujumla inakwenda mwendo wa KONOKONO(Very slow)
- Internet Tanzania, bado ni ghali sana kwa mtu wa kawaida.
Unaweza kubisha!
Lakini, watumiaji wazuri wa internet Tanzania, wanatumia katika maofisi walikoajiriwa au wanakofanyia kazi. Kwenye internet cafe, labda kama ndio ofisi yenyewe au kwa adoado sana.
Kama huna Laptop yako na unategemea Internet cafe ,basi uwe na bahati sana kupata sehemu ambayo uki ''CLICK'' tu e-mail yako inafunguka bila kusubiria sana au kuanza kuangaika labda FIREWALL ndio inazingua kwanini hii picha KITOVU tu ndio kinaonekana, lakini huoni mpaka kule chini NJIA PANDA.
DUH!
Kwa ujumla......
Tanzania inazidi kuwa nchi ya ajabu kwa jinsi matabaka yanavyojengeka.
Sasa hivi unaweza ukajisahau kuwa uko Tanzania upande mmoja wa barabara kwa kusikia watu wanalalamika jinsi walivyokula PIZZA mbaya , halafu ukivuka tu barabara ukakuta wanao lalamika hawajui watakula wapi.Kuna watakaokuambia kuwa ukitaka kuongea na watu watakaokuelewa , uende vijiwe fulani fulani siku hizi, hasa kama wewe ndio wale ambao moja ya tatizo lako, ni kujua nini kinaendelea New York , London au hata Beijing sasa hivi kama tu uangaikavyo kutafuta CIDER kwa sababu hupendi BIA Morogoro.
Unaweza kubisha!
Hasa wewe ambaye unanisoma hapa kwenye net hivi sasa hivi, lakini Internet bado si jambo linalojulikana na hata kutumiwa na asilimia kubwa ya watu Tanzania.
Unaweza kubisha!
Asilimia kubwa ya yaandikwayo kwenye net kuhusu Tanzania ni mambo ambayo hayawafikiii Watanzania walio wengi Tanzania.
Unaweza kubisha!
Kwa walalamikao kuwa wengi watumiao internet Tanzania hutumia kutafuta mambo ya sio kuwa na maana, ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya hao watu ni hao waitwao watu wa maana, wenye akili kama vile wanafunzi wa vyuo, walimu , maprofesa na wenye unafuu katika maisha . Na kama sikosei labda ni mimi na wewe ndio mabingwa wa kutaka kujua;'' hakuna picha za uchi za Rais kwenye net na wala sio hivi sera za Rais na Chama chake za kuendesha nchi zinatupeleka wapi. ''
Swali:
- Haujawahi kutafuta picha za uchi kwenye net?
- Hivi kutafuta maswala ya ngono kwenye net ni UJINGA?
- Ukiandika mtandaoni unafikiri ni nani anasoma?
DUH!
Naacha topiki basi!
Usinielewe vibaya!
Tanzania BOMBA!
Usije ukadhani nalalamika tu kwa sababu CHUNGU inazidi TAMUTAMU . Tamutamu ni nyingi kuliko chungu Tanzania. Na naamini ni mimi na wewe tunaotakiwa kuendeleza kuongeza TAMUTAMU Tanzania.
UKWELI ni kwamba maswala ya INTERNET hapa bongo bado yanazingua !:-(
AU?
Lakini pata MOTIVATION na TONY ROBBINS
Au pumzika na Henri Salvador akupe Jazz Méditerranée
Nakuacha na BAADHI ya picha za NDUGU na MARAFIKI kiduchu tena, ambao ni baadhi ya wanisaidiao katika Shida na Raha!
ASANTENI SANA!
Unaweza kuziangalia kama huzinguki!
Samahani lakini kama unazinguka!
Eli
Kusirie
Hassan na CO
Paul
Gayo na Katizu
FJ na Masandika
FJ na Nderima
Mrinde
Mr DJ
Master Marcus
Sisi
Irioko , Manento na KIKI
Adelino
Luta
Mchezo wa kuigiza Kale KAKUKU
Mimi , Maya , Davie na Mari
WIKIENDI NJEMA!
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
jamaa wewe ni mtaalamu wa sanaa ya kuandika vituko yaani visa kama mzee wangu Fred Macha. umenipatia kweli kweli. Lakini ukweli hata mimi naangalia sana wala hata mkisema ni ujinga au zinaathiri msinidanganye. tena kwa sasa nimekuwa nikijaribu kuuangali kupitia mtandao wa Google ta TZ ingawa bado haijakamilika katika progamu zake lakini nimeona picha nyingi tu tena za wabongo ambao wanablogu wanazungumza mahaba. lakini ukweli wanaosema kwamba hakuna mambo ya maana hao ndiyo watazamaji wakuu. mimi siacha tena nikima;liza hapa nabonyeza japo kuchungulia kidogo. msikasirike washkaji haya mawazo tu
hili ni bonge la mawazo mzee, kweli umefikiri haswa. lakini nadhani sababu kubwa ni kwamba wabongo huwa hatuna vijiwe maalum vyakuongelea mambo ya mahaba nangono kwa ujumla. tukiwa ktk wengi,hujifanya hatujui kumbe tukiingia kwenye net ndo kwanzaaaaa.
watoto hawaambiwi juu ya mambo haya na hivyo wakikua na kuwa huru, lazima wakimbilie ngono na hivyo wengi huwa addicted.
poa
@Markus: Tuko Pamoja
@Kamala:Nakubaliana na wewe kabisa.
ni kweli bana watu hawaongeleagi sana uso kwa uso hadi kwenye mtandao mi mwenyewe samtaim nachunguliaga kidogo.
amna bana ila sa si watu wanjifanya hawaongelei kumbe hasira zote kwenye mtandao
samtaim me mwenyewe nachunguliaga kiaina.
Huwa napiga Deo kimtindo.ila du!
Post a Comment