Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Baadhi ya sababu zimfanyazo BINADAMU atake KUHESHIMIWA!

>> Friday, August 28, 2009

UDHAIFU ndio sababu kubwa ya binadamu kufarijika AKIHESHIMIWA!


Unaruhusiwa kunibishia lakini!


Na katika BINADAMU kuhangaikia KUHESHIMIWA asilimia kubwa za awaheshimuo ni kwa vigezo vyao vya KINAFIKI vionyeshavyo UPANDE MMOJA WA YAO ili kuficha upande mwingine wa YAO au tu ili kulenga UDHANIE ni WAHESHIMIWA!

Ndio!

INASEMEKANA kila mtu anastahili HESHIMA kwa hiyo usiemjua LABDA sharti UMUHESHIMU kama hujui yake yaliyovulia nguo HESHIMA .


Ukifikiria zaidi labda ni busara kutowachunguza sana uwaheshimuo kama unataka KUWATUNZIA heshima!


Swali tena:

  • Hivi kwa kuwa heshima ni kitu cha bure hudhani inachangia HESHIMA kuheshimiwa kama vitu uvijuavyo vya BURE?
  • Hivi huwa unakumbuka kuheshimu vya bure?

  • Hivi si kuna uwezekano kama wewe si MDHAIFU basi huhitaji na hakikusumbui kujua ni nani AKUHESHIMUYE?



NALIKATIZIA HAPA HILI SWALA la heshima na labda ni la kijinga KIHESHIMA!

Twende tu BURUNDI kwa Khadija Nin alete kitu -Wale WAtu



Au tu ngojea tena Khadija Nin amzungumzie-Mama

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP