Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SHENZI mwanawane SHENZI![sentensi hii imebaniwa pua na msichana mwenye mafua:-(]

>> Tuesday, August 18, 2009

[Tahadhari: sina uhakika na maudhui ya taralira hii!:-(]
SHENZI mwaniwani SHENZI!!

LABDA kwa furaha umefurahishwa ,...
.... na kabla huja- NISONYA kama bado unaamini katika furaha wakati sifurahi unaweza tu mpaka kunitukana hata kwa zaidi ya SHENZI!:-(

SHENZI mwanawane SHENZI!

.... Halafu mtoto mzuri kama MALAIKA na kama unajua nakufananisha na MALAIKA unafikiri wakati UNANICHEKEA nitasikia au kujali yako ya KISHENZI?


SHENZI totoz SHENZI!

.....Na labda hata wakati tunachekeana yote ni UNAFIKI kama hatulengi nia na ingawa unajua wote sie katika tafsiri ni WASTAARABU bado nia yetu inaweza kuwa ni tufanye yatafsiriwayo kuwa ni USHENZI.:-(


SHENZI sista du SHENZI!
....sasa NTAFANYAJE wakati unajua chakukifanya labda ni kweli kimekunasia na tukileta jeuri ya kukitungua na kukifanya inaweza ikawa ni DHAMBI hata tukifanya kiustaarabu nafasi ikijitokeza na sio kwa kutaka kuhakikishia WATU ukweli KUWA kitendo chenyewe kama kilishafanikisha kuzalisha mtu labda si cha KISHENZI.:-(


SHENZI binti mrembo SHENZI!
... tukana tu KWA KUWA hata kama hupendi kubinuka au hata kutoa ukilala chali , hata ukiipigia magoti kwa afikiriaye kifanyikacho ni USHENZI hata umsomee ALBADILI atafanya akifikiria kuna uwezekano kifanyikacho hata kama kimebarikiwa na MZEE WA KANISA a.k.a SHEHE, bado HATA KAMA SIO WEWE bado kuna watakao kihusianisha na USHENZI!:-(

NALIKATIZIA WAZO HAPA na labda kama umenisoma mpaka sentensi hii kuna uwezekano ulichosoma ni USHENZI!:-(

DUH!




Hebu twende Angola KIDUCHU tukakutane na ya -BONGA

Au tu tubakie mpakani mwa KONGO na ANGOLA Ricardo Lemvo asemetena ya -MAMBO YOYO

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:09 am  

Kazi kwelikweli

Yasinta Ngonyani 10:43 am  

Simon:-(

Simon Kitururu 7:06 am  

@Askofu Fadhy: Si utani!
@Dada Yasinta: :-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP