Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuhusu SWALA la uzito wa MOYO!

>> Wednesday, August 12, 2009

Mara nyingi KUHUSU UZITO wa MOYO,...

....huwa kinachozungumziwa ni UZITO wa kukubali HALIHALISI ajisikiayo MTU hata kama kwa hilo itasingiziwa mpaka ROHO!:-(


Na amini USIAMINI wengi waongeleao MAUMIVU YA MOYO,....

....hawaongelei unaodunda MOYO , kwa kuwa kama wanazotuziitazo dini katika maelezo yao watasingizia KWA HILO mpaka ROHO!:-(

Na wakati unaongelea MOYO,...

... kumbuka kwa binadamu humchukua muda kuelewa tokea akizaliwa kidundacho kifuani ni MOYO na hata baada ya kujua atachanganya katika kwake kuapia hata maswala yasiyo husiana na MOYO akaapia kwa moyo KUWA hata HAJAWAHI KUJINYEA wakati hata nia yako YAKUTAKA UKWELI ILIKUWA si YA kumtoa ROHO!:-(



Na usishangae kuwa bado kuna waongeleao ya ROHO wakiwa wanatoa stori za maumivu ya MOYO,....

...... kwa kuwa LABDA wanajua au hawajui kuwa hata wewe katika JEDWALI hujui nini tofauti ya YA MOYO na YA ROHO!:-(




DUH!
NIMEACHA MHESHIMIWA!

Swali:

  • Kwani ulikuwa na miaka mingapi ulipostukia una MOYO?
  • Hivi wewe UNA MOYO KWELI?

DUH!

Ngojea SANCHEZ abadili hali ya hewa kwa kitu -Love is POWER..




Au tu Toots & Maytals ft SHAGGY waongelee- BAM BAM

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 10:45 pm  

Mambo bam bam. Uliapotelea tuition kujifunza kutofautisha roho na moyo?

Simon Kitururu 1:59 am  

@Papaa Fadhy : Ulistukiaje?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP