Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MATATIZO ya kuwa huru wakati umeshazoea kuishi JELA!

>> Wednesday, August 19, 2009

Kuna wazoeao kuishi kijelajela na uhuru kwao ni ....

.....PRESHA!

Na kuwa huru kuna presha za kufikirishwa ufanye nini na uhuru ambao labda hata ukitaka kula WAWEZASTUKIA ghafla mpishi ni wewe na utajikuta tu unalazimika mpaka....

.....KUJIPIKILISHA!:-(



Na unaweza MPAKA kututangazia MAMBO kwa kuwa uko huru , ila kasheshe ni katika kutekeleza LA sivyo yatakushinda kama yalivyowashinda WATANZANIA hata baada yakututangazia wanuiayo kwenye lao .....

...... AZIMIO LA ARUSHA!:-(


Uhuru kitu cha ajabu kwa maana usipoangalia eti kwa kuwa tu uko huru waweza kujikuta kwa uhuru umeamua hata kidonda chako mwenyewe kwa kukosa vyakufanya kujazia uhuru....

....UMEKITONESHA!:-(

DUH!
Ni wazo tu MHESHIMIWA ingawa labda kuna ukweli kwenye hii HOJA!:-(
Swali:
  • Uko huru?
  • Unauhakika kuna aliye huru?

Hebu twende Gabon kidogo tupate Patience Dabany


Au tubaki tu Gabon tukutane na VIBRATION walete kitu -Mone Bone

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:53 am  

Huru;-(

Masangu Matondo Nzuzullima 3:30 pm  

Uhuru wa kimwili au kisaikolojia? Waweza kuwa huru kimwili lakini ukawa bado uko jela kisaikolojia.

Walikuwa sahihi waliosema MENS SANA IN CORPORE SANO "A healthy mind in a health body?"

Kwa maoni yangu Health body (uhuru wa kimwili) ni rahisi zaidi kuliko healthy mind (uhuru wa kisaikolojia). Itazame Afrika na utaona!

chib 4:15 pm  

Kumbe tafsiri ya huru , zipo nyingi eh!!

Simon Kitururu 10:04 pm  

@Dada Yasinta: Ndio, Huru/Uhuru ndio swala lenyewe!:-(

@Profesa Masangu: Yani hapo sikubishii hata kidogo!


@Mkuu CHIB: SI utani!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP