Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nyuma na MBELE, usiposahau dunia ni MDUARA!

>> Friday, August 21, 2009

Nyuma ya MBELE labda haiko NYUMA,...

.... ingawa labda utapata mpaka mashahidi kuwa iko NYUMA.


Na mbele ya NYUMA,...
....kwa mtazamo au tu ukichukulia NYUMA kama vile uso wa tako,...
.... basi si utani ; Mbele ni NYUMA.

Lakini NYUMA ,...
..... hata ya MBELE YAKO kwa kuwa dunia ni mduara labda BADO iko mbele yako na si NYUMA.


Na kwa kuwa dunia ni mduara hata tukiwa tunatafakari ya NYUMA,...
....hata kwa AFIKIRIWAYE yuko MBELE kuna uwezekano katika MDUARA mara kibao ukweli ni kwamba kwa wenzie huwa anakuwa yuko NYUMA.

Swali:

  • Au?

  • Ushawahi kuangalia wanariadha wanakimbia uwanjani halafu ukachanganya wa mwisho ni yupi na wa kwanaza ni nani?

  • Kama uko mbele unafikiri tukigeuka sio wewe utakaye kuwa nyuma?
  • Unakumbuka aliyekukutangulia hata katika MDUARA HUU wa kuzaliwa na kuvalishwa nepi kwa utoto ndiye atakaye kuwa anajikojolea na kufungwa nepi hata kama tunamuita ni mzee lakini kuna mambo AFANYAYO hata UKIBISHA yata kukumbusha mtoto?

NI wazo tu na wala huhitaji kunielewa Mheshimiwa!


Ngojea Prince alainishe kwa kitu- Crimson and Clover


Au tu Osibisa warudie kitu -WOYAYA

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 7:21 pm  

Mmmmhhh:-(

Fadhy Mtanga 11:32 pm  

Sana tu Mtakatifu Simon, hata ukigeuza shingo, macho si yanakuwa nyuma na kisogo mbele?

Simon Kitururu 4:17 am  

@Yasinta: Mmmmmhhh!
@Askofu Fadhy: Nahisi hivyo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP