Bwiti!
>> Tuesday, May 22, 2007
Nashindwa kuelewa kwanini kutoka Afrika ni Vudu inayosikika kuliko dini nyingine yeyote kutoka Afrika.
Hivi Tanzania kwanini dini zetu za asili hazitambuliki kwa majina? Si maanishi kuwa ni lazima mtu aziamini hizi dini. Lakini kwanini majina yake nayo imekuwa mwiko kuyajua?
Utasikia jinsi zinavyolinganishwa na kuoanishwa na uchawi, lakini husikii sana zikitamkwa kwa majina yake. Utasikia tu jinsi gani karibu kila lugha izungumzwayo kwa mfano Tanzania, ina jina la Mungu au Miungu. Kinachoshangaza ni kwamba hatuzungumzii dini zilizokuwa nyuma ya majina haya ya Mungu na Miungu.
Pia hata hii dini ya Bwiti yenye asili ya Gabon, ni mara chache ukisikia watu wakiiongelea.Ingawa ni miongoni mwa dini chache za Kiafrika ambazo zinakubalika katika nchi zilipo kama dini. Wengine dini ni zile tu tulizoletewa.
Hebu cheki Wadau wa Bwiti wakikuimbia nyimbo za dini...
Ila inasemekana mizizi (ibogaine) waitumiayo wakati wa ibada imegundulika kusaidia kutibu watu waliokumbwa na tegemezi la kutumia madawa ya kilevi. Kwa hiyo hata kama huamini wasiyo amini angalau kakitu kutoka katika imani yao kuna watu kana wasidia.Au sikiliza hiki kitu...
Duh!Lakini haya mambo ya dini mmh!Mi chichemi!
Siku njema!
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment