Nyumbani kwa Kitinda Mimba!
>> Thursday, May 10, 2007
Nilimuomba Mzee Maggid amtembelee Mama!
Asante kwa kufanya hivyo. Unajua haya maswala ya Ughaibuni nayaacha hivi karibuni. Mimi Kitinda mimba.... Narudi kwa mama hivi karibuni!
Kabla sijasema ngojea nimuache Richard Bona...
Sasa kabla sijaendelea , ngojea niache baadhi ya picha za chobisi Maggid
alizopiga.
Mtoni -Rock Garden
Chobisi ya mama ileeeeeee!
Hapa ni ileile chobisi ya mama kwa karibu kidogo....
Duh!
Napamisi , lakini.....
Ngoja Manu Dibango anisaidie..
Mjengwa alimkuta Shangazi yangu pia.......
Maggid Mjengwa eeh!Mama anakushukuru sana kwa kumtembelea.Ulichukua lakini tunda alilokua anakuchumia?Huyu ni mama yangu Mzazi. Nilimuaribu tumbo kwa sababu mimi ni Siziliani , kama unaelewa nacho sema.
Lakini....
namuachia Sizzla...
Kabla hujafika chobisi ukitokea kwa mkuu wa Mkoa lazima uvuke mgomba huu...
Hapa ni kutoka bustanini kwa mama ndio morogoro ionekanavyo.Umestukia Uwanja wa Jamuhuri pale chini?
Lakini unajua tena , pamoja nakupata faragha ya nyumbani , polisi wapo pia
Hebu Mpate KRS One
Mjengwa, nimefurahi sana!
Asante sana!
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Bwana Yesu hakusema tuuvae msalaba bro.Kwani si wahalifu si ndo waliosulubiwa, Yesu walimsulubisha ingawa hakuwa miongoni mwao.Msalaba ni ishara ya ukombozi wa roho.Tuamini tu,yatosha.Maandiko hayajatuagiza kuuvaa shingoni.
Bro ile hoja ya Mkaguzi mkuu wa serikali uliahidi kuchangia.Nakukumbusha.Wale wezi wananitia hasira kweli. Kweli nchi inaliwa na wenye meno.
Mzee Anony :usemayo kweli.Bwana Yesu hakuagiza kile kitu.Unajua tena, nawaza tu!Ile hoja sijaisahau!Nitaichangia.
Hiyo Morogoro imenivutia inavyonekana kijani, ni muda mrefu sijapita hapo, lakini na mimi ni karibuni nitakwenda huko.
Simon Raha ilioje kumuona Mama!.Kumbe wewe ni kitinda mimba?.Ngwala ulizopigwa ughaibuni zinatosha wahi fasta karithi uwanja huu.
Lakini sio uje upauze na kukimbilia darasalama...!!!
Simon,
lini "Mologolo" mtaleta wawekezaji wajenge bahari?
@Ndesanjo:-)
@Egdio:Raha kumuona mama.Dar esalaam kuna utamu wake lakini Morogoro ni jiji kasoro bahari tu.Na tushaanza mipango ya kujenga bahari ya mindu:-)
@Ndabuli: ni kweli ukijanni wake unavutia.Lakini wakati wa vumbi ni kasheshe pale
Post a Comment