Lugha ya pesa!
>> Wednesday, May 02, 2007
Lugha ya pesa nafikiri ndio ielewekayo zaidi ya Kiingereza , Kimandarini(Kichina), .......na hata kuliko lugha hii tukufu ya Kiswahili!
Lugha hii ya pesa imetusaidia sana hapa duniani kuendeleza rushwa na mambo mengine kibao.
Lakini unastukia kuwa ingawa tunaisifia pesa, muda wa muda ukifika watu hujichukulia vyao.Halafu pesa yako inakuwa haina thamani.
Inasemekana wakati wa meli ya Titanic ilipoanza kuzama, matajiri walikuwa wanataka kuhonga kupata sehemu za maboti ya dharura.Hakuna mtu aliyekubali pesa hata mmoja!
Swali:
Lakini si niukweli hii pesa na mali hizi hatuzikwi nazo?
Inasemekana Zimbabwe sasa hivi ile lugha ya pesa inabidi uje na gunia kutokana na inflation.
Duh!
Kunajamaa aliimba kuwa pesa ni sabuni ya roho!
Najiuliza tu kuwa, tukishakufa si roho inautoka mwili? Sasa hii roho mbona inaiacha tu hapa kipengele(duniani) hii sabuni ya roho?
Hivi kuhusu hawa walionazo hizi pesa wanavyozidi kuongezewa, ni mpaka lini wasionazo wataendelea kukogesha roho kwa sabuni za mbunju?
Jumatano njema!
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mambo ya fweza! Kila mtu anaielewa lugha hii kiufasaha. Ila mhh! Pamoja na kwamba ni sabuni ya roho lkn huwa inaichafua roho na mwili pia.
true mtz
Nahisi inawezakuchafua mpaka akili
Post a Comment