Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo Nimehubiriwa Sana!Lakini naogopa Kukufuru!

>> Thursday, May 24, 2007

Nimepata bahati ya kuhubiriwa sana leo hii!
Hasa baada ya kukiri kuwa sina imani na dini ziendeshwazo katika mfumo.Mfumo na maanisha dini yenye kiongozi na mfuasi na .....
Nahisi umenipata!
Moja ya jambo nilikuwa na habarishwa, lilianzia kwenye jina langu Simon.Kwa sababu linaashiria kuwa ni Mkristo.Lakini hivi unajua Simon maana yake ni Jiwe tu?Hivyo nikilibadilisha kulifanya la kiswahili, mimi naitwa Jiwe.

Ngoja nikupe dondoo ya yaliyonikuta ili ufikirie mwenyewe. Mimi niko mawazoni tu hapa lakini, samahani kama utajisikia vibaya au uka........

Mimi sisemi kitu zaidi yakukupa dondoo zilizokuwepo mjadalani.

Kwanza kulikuwa na hivi vitu viwili vilivyosababisha baadhi ya watu waanze kusema Wakristo wamepoteza nguvu za kutetea dini yao .....

1.Jose Luis de Jesus



Nilishawahi kumuandika hapa


2.Halafu cheki kazi ya Javier Prato

3.Bila kusaha hoja hizi:
Nani zaidi?


Ukiniuliza mimi kuhusu maswala haya, nitakuambia kuwa sina la kusema!
Wewe tu na Mungu wako!

Au Tubu basi !
AU

Kama unamfuata Jose , yeye anasema huna dhambi!

Kama unafuata Voodoo au Bwiti au........sijui!



Duh!
Mimi ntakuambia ngojea tuendelee kumsikiliza
Santana hapa , akikupa kile kibao Soul Sacrifice kama alivyo kipiga Woodstock 1969

Haya tena , Kesho basi!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 7:25 am  

Huyo jamaa anayehubiri uislamu na sijui nini, simwelewi kabisa anasema nini. Ulevi ule aliosema Marx. Hivi anasema nini hasa?

Simon Kitururu 8:23 am  

@Hapa anajaribu kuelezea tofauti ya Yesu na Nabii Mohamad hasa nani ni zaidi.Inatokana na swala kuwa Yesu anatajwa mara nyingi kwa jina katika Kuruani kuliko Nabii Mohamad. Topic hii mara nyingi hunifanya nikae kimya tu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP