Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa Mpendwa Halufani!

>> Wednesday, May 16, 2007

Salamu nyingi zikufikie hapo chobisi ulipo!

Mimi huku sijambo ingawa ndio hivyo tena unajua hali ya dunia hii tuishio, kuna mengi bado yananizingua na mengi tu nimeshindwa kufanya .Sijakata tamaa lakini!Ingawa siachi kujiuliza maswali kuhusu dunia hii yetu kuwa;

Hivi Ni Kweli Dunia inatakiwa Kukosa Kasoro?

  • Ukizungumza na wataalamu wa mazingira, watakwambia jinsi gani binadamu anaharibu mazingira

  • Ukizungumza na wenye misimamo mikali ya dini ,utaambiwa jinsi gani shetani anavyozidi kumharibu binadamu

  • Ukiongea na wataalamu wa afya, watakwambia jinsi gani afya ya binadamu inavyotishiwa na hali ya dunia hivi sasa.

  • Ukiongea na wakubwa, watakuambia jinsi gani wadogo wanavyozidi kuharibika kitabia sasa hivi.

  • Ukiongea na mamilionea , watakuambia jinsi gani thamani ya shilingi milioni ilivyoshuka sasa, lakini jinsi gani waweza kupata vitu vingi sasa hivi kuliko zamani .

  • Ukiongea na masikini , watakuambia jinsi gani umasikini unavyozidisha makali hivi sasa.Na jinsi gani masikini anavyoshindwa kujisitiri hata kwenye mambo madogo.
Sasa .....
Ukifuatilia historia iliyonukuliwa tokea enzi za mababu na kabla ya mababu, si utakuta kuwa;


  • Kama ni hali ya hewa na mazingira, yalibadilika.Kukapita kipindi kisemekanacho kuwa dunia nzima iliganda na ikayeyuka , na mabara kugawanyika bila binadamu kuwa na mchango wowote katika hilo.Ma dainasoo wakapotea duniani ,tukabakiwa na Kifaru, mbu, skopioni na kadhalika wachache.
  • Kidini , kwa jicho la dini zenye sifa duniani siku hizi, nikimaanisha ukristo, uislamu, nk;si ni ukweli kuwa idadi ya waumini wazifuatazo ni wengi zaidi siku hizi, ukilinganisha na wakati Waijipti wanaamini Farao ni Mungu?
  • Ukizungumzia afya ya binadamu katika kipindi hiki cha sayansi na uharibifu;si inasemekani binadamu anaishi miaka mingi kuliko zamani?Lakini hapa si nukuu miaka ya kwenye biblia ambayo hukawii kusikia mtu alipofikisha miaka mia nane........!
  • Kuhusu tabia; si nasikia karibu kila kizazi huona kifuatacho kimeharibika?Halafu na miziki ya kizazi kipya ndio hata usiseme!Makelele tu, ukimuuliza Babu yangu!
Lakini mpendwa Halufani ,
Dhumuni la barua hii nikutaka kukujulia hali tu! Mimi bado niko vilevile. Kuna wakati na furaha, wakati mwingine na hasira, wakati mwingine na huzuni,wakati mwingine nafanikiwa, wakati mwingine nashindwa na wakati mwingine nipo tu mawazoni ni, nikiamini;Au ;

  • Naamini kuwa haya ndio maisha na najitahidi kuyakabili niwezavyo kuyaboresha.Nafikiri na wewe unakubaliana nami kuwa maisha ukinuia yanaboresheka!
  • Naamini ni busara kuilinda dunia isitetereke, lakini pia naamini kuwa kuna mambo ya kidunia , yatakayobakia kuwa ya kidunia.Hata binadamu afanyeje dunia itaendelea kuwa na maana ya dunia ikiwa binadamu ataendelea kufikiria kua kuna sehemu bora zaidi mahala pengine ambapo baadhi ya watu wengine hupaita mbinguni.
  • Naamini kuwa masikini wa sasa hivi hawezi kukubali kubaki maskini kinamna walivyo leo wakati wanajua tajiri anaishije na anawaibiaje.Itafika siku atajichukulia chake hata kwa nguvu.Lakini , dunia itabaki kuwa na tajiri na maskini mpaka mwisho wake, ingawa umaskini utakuwa katika tafsiri nyingine si ya sasa ambayo kuna watu wamezidiwa na matoke, wakati wengine wanazidiwa na shughuli zakutupa maganda tu.
  • Naamini tabia ya binadamu itabakia kutafsirika katika makundi ya tabia mbaya na nzuri.Sina uhakika nani atajulikana kuwa anatabia mbaya au nzuri lakini!
Sasa nisikuchoshe sana na barua hii ndefu!Siunajua siku hizi tuna vimobiteli?

Nakutakia kila la heri katika mradi wako wa kuishi!

Ndugu yako katika kuwa hai,
Mawazo.

PS :Wasalimie wanaume na wanawake hapo mradini kwako!
Halafu si unamkumbuka Maiko Jakisoni

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP