Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUTAHIRI BEI NAFUU TANZANIA!KARIBUNI WATALII!

>> Friday, May 04, 2007

Kuhusu kichwa cha habari hapo natania tu!AU?

Kuna kitu kimoja kimenigusa leo , baada ya kukutana na habari kuwa waanzilishi wa Benji Jump wanadai haki ya kutambulika kuwa wao ni waanzilishi.Baada ya kusoma historia ya benji jump, na hii sehemu ya visiwa vya Pentecoste, Vanuatu kipindi fulani, ndio nilipata kujua jinsi gani watalii walirekodi maswala na jinsi kwa ubunifu wakaiga na kugeuza mila kuwa mchezo.Hili limenifanya nikakumbuka jinsi gani watu wanaweza wakaja kwenu wakaiga chenu halafu wakakifanyia kazi mpaka hawahitaji chenu tena!Huu mchezo wa benji ingawa watu hawa wapasifiki wameuanzisha , sasa hivi wanadai haki yakutambulika tu kuwa waliuanzisha. Ingawa kwao ilikuwa si mchezo , ilikuwa ni kuonyesha ushujaa kabla yakujiunga katika kundi la wakubwa, wakuja walipoustukia wakaukarabati wakaufanya wao.

Sasa.... Kwanini naongea hili?

Jeff Msangi aliongelea jinsi alivyotembelea Busch Gardens-Afrika , akiwa mitaa ya kusini mwa USA, akajikuta yuko nyumbani.Maana wana mbuga yenye wanyama kibao uwajuao wa Afrika Mashariki.Wana mpaka magari yenye namba za Tanzania yakuzungushayo Mbugani. Kwa ujumla wanatengeneza Serengeti yao ambayo wanaiendesha kiufasaha na kuhakikisha inalipa kuliko labda Serengeti itulipavyo wabongo.


Unaweza kuamini hili gari liko mbugani Marekani?

Picha kwa hisani ya Jeff Msangi








Sasa ......
Sisi Watanzania tunaweza kusema kuwa mtu hawezi kukopi Serengeti ikawa na utamu wa serengeti, lakini mimi naamini utamu wakitu unasaikolojia yake.Ndio maana watu wanasomea advertisement, marketing nk . Kisaikolojia mtu anaweza kukubadili mtazamo wako.

Swali:
Unakumbuka kunakipindi ilikuwa bomba kunywa kokakola ya kopo?Sasa unafikiri koka kola ya kopo inautamu tofauti na ya chupa?

Tukirudi katika kutahiri.............

Ndio , tunahitaji kuitangaza nchi yetu ilikuiongezea pesa za kuiendesha bila kutegemea mikopo.Na tunavivutio vingi ambavyo havijulikani bado.Lakini tusiwadharau ambao wanachukua wanyama wetu na kuanzisha mbuga zao.Ni ukweli ukichanganya na mabadiliko ya hali ya hewa(Global warming) , twaweza kujikuta ni sisi tumepungukiwa wanyama na nguvu ya kivutio halafu walioiga wameneemeka mapaka inabidi sisi ndio tutembelee kwao kuona vilivyokuwa vyetu. Halafu tutaanza unajua hawa simba walikuwa wetu!Halafu mpaka tunaanzisha vi-NGO vya kudai kutambulika kuwa sisi ndio tuliokuwa na serengeti halisi.

Okei , labda nimezidisha hapo!Inawezekana hili halitatutokea sisi. Lakini vizazi vyetu vijavyo je?

Swali:
Unafikiri hizi serengeti zianzishwazo ughaibuni zitakufa au zitakuwa kubwa zaidi karne ijayo?Unafikiri jinsi hali ya hewa inavyozidi kutotabirika haiathiri mbuga na vivutio vyetu vingine?


Basi tuendelee kuitangaza vyema nchi yetu na Afrika yetu!Ingawa si lazima kujitangaza kama tangazo langu hapo juu!Umelisahau nini?

Jikumbushe......
KUTAHIRI BEI NAFUU!KARIBUNI WATALII!

Duh!Munishi naye nasikia anataka kuwa raisi!Wewe je?
Endeleza ijumaa naye basi........Duh!Mimi sio mdini kabisaaaaa usinistukie kutokana na injili!:-)




Hivi waandishi wa habari wakimfuata BuDa na kuto mfuata mesaya kama Munishi atakavyo itakuaje?

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Aliko 3:28 pm  

Simon the best selected musical clip so far hahaha i dedicated this tune to bwana maggid,michuzi na wengineo...

Simon Kitururu 4:19 pm  

@Aliko:Asante Mzee!Siunajua tena !Injili!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP