Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Funzo kutokana na Uingereza na Marekani walivyoiba Chagos!

>> Monday, May 28, 2007



Kabla sijasema.
Binadamu unaweza kumpenda panzi kuliko binadamu mwenzako?
Sitanii!Katika baadhi ya nchi naona imefikia kipindi ambacho kitu cha muhimu ni , mbwa wako, wanyama fulani , vipepeo na unaweza ukafungwa kwa kumpiga teke mbwa na kupewa onyo tu ukimpiga mwenzio.

Dondoo:
Hivi unajua USA walikuwa wanataka visiwa vya Aldabra na sababu kubwa waliyotoa kutokichukua kisiwa ilikuwa kuwa pale kuna Kobe wakubwa wanao ishihapo.Jibu walilopata likawa kuwafukuza watu Chagos .



Ukifuatilia mkasa uliowakumba watu wa Chagos, unaweza ukasahau jinsi gani sehemu nyingine kibao zinavyozidi kuibiwa.Kinachofurahisha ni kwamba watu wa Chagos wamefanikiwa kushinda kesi ya kurudishiwa nchi yao, ila tatizo linakuja kwetu wale ambao hatakustukia nchi imeibiwa hatujastukia.

Waingereza na Wamarekani walifanikiwa kuwafukuza wenyeji katika nchi yao kwa kisingizio cha vita baridi dhidi ya USSR. Sasa hivi ukifikiria sana utastukia kuwa hakuna haja ya kufukuza watu kwao, unawachukulia nchi kwa kumiliki bunge lao , miundo mbinu yao na hata akili zao.

Ukiniuliza mimi nitakuambia kuwa , hata kushinda kesi kwa Chagos sasa hivi kunatokana na kupungua kwa umuhimu wa visiwa hivyo kwa Wamarekani na Waingereza.

Nachojua ni kwamba , nchi zetu hasa za Afrika , hazitaachiwa kama maslahi wapatayo kwa kuzimiliki yanazidi nguvu zetu za kujikwamua.Tunaposhindwa kuweza kututumua misuli yetu kufanya nchi nyingine kushindwa kututawala kamwe hatutaachwa kutawaliwa.

Duh!
Samahani, nakumbuka tulipata uhuru miaka kadhaa iliyopita!


Swali:
Hivi wewe ukiwa ndio Mtawala, ukakiri kuwa umetoa uhuru sehemu sehemu ambayo ilikuwa inakufaidisha, unafikiri utakubali kuchangia pesa za kuendesha hiyo sehemu ya uliowaachia ili wajinome bila wewe kuwa na lako ulipatalo hapo?


Je,unafikiri kwanini watawala wa zamani wa nchi za Afrika bado ndio wachangiaji wakubwa wa bajeti za nchi walizosema wamezipa uhuru?
Au unafikiri wanatupenda sana?


Duh !
Siasa kidogo iko mawazoni leo!
Sijapata kamuda kakuandika sana siku kadhaa!

Baadhi ya sehemu niliyopotelea ilikuwa ni hii Photo Sharing and Video Hosting at PhotobucketWorld Village
Picha na Arto Salonen

Baadhi ya wadau wengine niliokuwa nao.......

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aiyekoto mchana

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aiyekooto Usiku

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
BassSoul

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Victor

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Riinah

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aicha

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mandevu:-)

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tompura

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Ghanan Prinsi

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Abdul Senegal

Duh!
Na wengine wote!Tuko pamoja!
Pata Kool and the Gang basi!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP