JAMBA TU!Si uko peke YAKO?
>> Friday, December 26, 2008
Inasemekana kila kitu kina mahali pake hasa kwa WAHESHIMIWA wenye tabia nzuri.
Binadamu anajifunza tabia nzuri tokea azaliwe na ikibidi ahisicho ni tabia mbaya hawezi kukifanya kwenye umati kama hakilipi ,INGAWA ni machoni mwa jamii yenye watu wenye tabia mbaya wajulikanao kwa ustaarabu wa mazuri.
Kujamba ni muhimu!
Staili ya kujamba na mahali ajambapo mtu inaweza kukuambia TABIA ya mtu ,alivyolelewa MTU na hata UHURU wa MTU kisaikolojia kama sio hata jinsi alivyo MBUNIFU katika MAISHA.
Unaweza kuchagua mpaka MKE kwa kufuatilia anajambaje na anajamba wapi.
Staili ya mtu kuficha kajamba, inaweza kukuambia jinsi gani ni MUONGO au awezavyo kukudanganya hata kwa vitu vya kawaida.
Swali:
- Kujamba si ni kitu cha kawaida kwa binadamu alaye kuliko hata kuvaa nguo?
- Unakumbuka mavi na wenzie huanza kunuka kabla ya kunya na labda HUNUKA tokea tumboni?
Na pia...
...UHURU ni kitu cha ajabu!
Kama unataka kupima jinsi gani uko huru, jamba uhisipo si pa kujamba halafu sikilizia kama unaona aibu au unajisikia kuondoka maeneo kwa sababu ya MAFANIKIO ya USHUZI au LA , wakati watu wanajua ni WEWE uliyeachia ushuzi.
Kumbuka lakini...
.....kuna tamaduni , kama hujajamba au kucheua, hujashiba wewe, na ugali utaongezwa!
Na labda...
... ni busara kabla hujaoa au kuolewa ujue staili za kujamba, mahali pa kujamba au tu wajambavyo UKWENI.
Kumbuka lakini..
...labda kujamba haimaanishi KUJAMBA katika HADITHI HII, ingawa tabia fulani za binadamu ni USHUZI!:-(
JAMBA TU, hatusikii wala hatukuoni!
Jamba tu mtoto MZURI, utajisikia AHUENI!
DUH!
Naacha!
SIKU NJEMA!
AU hebu Tutembelee kidogo PARIS kuangalia jinsi WANAFUNZI wa VYUO VIKUU TANZANIA watakavyokuwa wakiandamana Mwakani....
AU ngojea Future MAN , Fleck na Victor Wooten wanisaidie KUfankifai kama sio Kujazzifai ,katika LET ME BE THE ONE.....
Au turudi tu KENYA kwa Safari Sound Band waendeleze CHAKACHA...