Sukari HUZUNI, kabla ya KULIA!
>> Thursday, December 18, 2008
Kifungua kinywa ni huzuni
...kama chakula NI mwenye huzuni KULIA
Furaha kushoto ukilia ..
...ingawa huzuni si lazima KULIA.
Ingawa kwa furaha......
....unaweza KULIA.
Huzuni ni siri ya utamu wa furaha
...ukiacha KULIA
Utamu wa huzuni,
...chukua muda kabla ya KULIA.
_______________ __________________ _____________
Nawaza tu MKUU!
Swali:
- SI unajua huwezi kuharakisha HUZUNI hata kama UNATAKA au UKO TAYARI kulia?
Au Lord Kitchener aje na - Old Lady Walk Ah Mile
Au tu Lord Kitchener aendeleze tu muziki wa aina ya SOCA katika "kaka roach"...
8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
AMBIERE, E VAVA,
NIMEPITA TENA LEO ALFAJIRI KUKUJULIA HALI.
KAZI NZURI NA IMEJAA UBUNIFU WA HALI YA JUU.
@Ambiere:E vava hi aho!:-)Asante kwa kutonitenga hapa kijiweni!
Simon! kuna watu wanaweza kulia kwa sababu wana furaha, machozi ya furaha. Au nimechemsha?
@Yasinta:Ndio maana nimeandika...:
´´Ingawa kwa furaha......
....unaweza KULIA.''
Kazi nzuri sana. Nimependa tungo yako kaka. Inanitafakarisha. Nitarudi kusema nilichowaza.
@Bwaya:Karibu tena Mkuu na asante kwa kutonitenga!Nashukuru kama imegusa kitu Mkuu!
Haya tena nanukuu. Na safari hii ni kutoka kwa Lucky Dube aliyesema "tears can not bring you joy, but joy can bring you tears. Even though i cry today, i will not hide it. It's for a different reason. JOY" (na hili si watu wa malezi na jinsia zote wanaweza kukubaliana nalo hivyo kama hudhani ni kweli usibishe maana yawezekana ni malezi na jinsia yako vikuaminishivyo hivyo). Lakini ukweli utabaki uleule kuwa ukiona mtu analia usianze kumpa pole. Pengine ahitaji hongera. Na usimpe hongera pia maana yawezekana ahitaji faraja. Kuna haja ya kutafakari kabla hujaamua kutatua tatizo maana si mara zote twawa sahihi katika kuamua juu ya tuonayo, kwani namna tuonavyo .......
@Mzee wa Changamoto: Si utani!
Post a Comment