Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

JAMBA TU!Si uko peke YAKO?

>> Friday, December 26, 2008

Inasemekana kila kitu kina mahali pake hasa kwa WAHESHIMIWA wenye tabia nzuri.

Binadamu anajifunza tabia nzuri tokea azaliwe na ikibidi ahisicho ni tabia mbaya hawezi kukifanya kwenye umati kama hakilipi ,INGAWA ni machoni mwa jamii yenye watu wenye tabia mbaya wajulikanao kwa ustaarabu wa mazuri.

Kujamba ni muhimu!

Staili ya kujamba na mahali ajambapo mtu inaweza kukuambia TABIA ya mtu ,alivyolelewa MTU na hata UHURU wa MTU kisaikolojia kama sio hata jinsi alivyo MBUNIFU katika MAISHA.

Unaweza kuchagua mpaka MKE kwa kufuatilia anajambaje na anajamba wapi.

Staili ya mtu kuficha kajamba, inaweza kukuambia jinsi gani ni MUONGO au awezavyo kukudanganya hata kwa vitu vya kawaida.

Swali:


  • Kujamba si ni kitu cha kawaida kwa binadamu alaye kuliko hata kuvaa nguo?

  • Unakumbuka mavi na wenzie huanza kunuka kabla ya kunya na labda HUNUKA tokea tumboni?

Na pia...
...UHURU ni kitu cha ajabu!


Kama unataka kupima jinsi gani uko huru, jamba uhisipo si pa kujamba halafu sikilizia kama unaona aibu au unajisikia kuondoka maeneo kwa sababu ya MAFANIKIO ya USHUZI au LA , wakati watu wanajua ni WEWE uliyeachia ushuzi.

Kumbuka lakini...

.....kuna tamaduni , kama hujajamba au kucheua, hujashiba wewe, na ugali utaongezwa!

Na labda...
... ni busara kabla hujaoa au kuolewa ujue staili za kujamba, mahali pa kujamba au tu wajambavyo UKWENI.

Kumbuka lakini..

...labda kujamba haimaanishi KUJAMBA katika HADITHI HII, ingawa tabia fulani za binadamu ni USHUZI!:-(

JAMBA TU, hatusikii wala hatukuoni!

Jamba tu mtoto MZURI, utajisikia AHUENI!

DUH!
Naacha!

SIKU NJEMA!

AU hebu Tutembelee kidogo PARIS kuangalia jinsi WANAFUNZI wa VYUO VIKUU TANZANIA watakavyokuwa wakiandamana Mwakani....




AU ngojea Future MAN , Fleck na Victor Wooten wanisaidie KUfankifai kama sio Kujazzifai ,katika LET ME BE THE ONE.....



Au turudi tu KENYA kwa Safari Sound Band waendeleze CHAKACHA...

13 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 1:27 pm  

Ambiere hata Huku Gonja Maore mtandao upo.
Mkuu hii staili ya kuja....
inahitaji tafakuri, niko ukweni nahisi wataona ninachoandika.
Kesho narejea mjini lakini sina zawadi, kwani watu ndio wanaandaa mashamba hata kishumba hakuna.

Simon Kitururu 1:39 pm  

@Ambiere Kaluse:Basi usijambe, naona hauko peke yako!:-(

:-)

Koero Mkundi 1:56 pm  

Mmm!!! kaka mada zako mbona zina utata?
Mimi hii mada siiwezi.
Japo nimejifunza jambo moja hapo.

Simon Kitururu 2:03 pm  

@Dada Koero: Nawaza tu hapa Dada Koero!Usitishike usiponielewa!Kunauwezekano kabisa niandikacho hakieleweki.

Asante lakini kwa kunitembelea!:-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 1:41 pm  

mimi nimekuelewa. ila nina swali, hivi wewe ukiwa unajamba, unajisikiaje? ukiwa peke yako chumbani, unafyatua tu au?

hivi uliwahi kuwa mbele za watu, unatoa mada, unafundisha nk, watu wote wamekuangalia wewe, harafu li-ushuzi kkubwa linakuja halafu linanuka, huwa unafanyaje? unabana jicho au?


mada hii

Yasinta Ngonyani 3:22 pm  

Sawa kabisa Simon! ila mimi bado sijaelewa haya mambo ya utamaduni-mila . Kwani kuna sehemu nyingine kujamba ni ok, lakini si kucheua.Hapo bado sijaelewa

Mzee wa Changamoto 7:39 pm  

Huku nilipo hawajali kujamba. Ila ukiingiza kidole puani ni balaa. Yaani unaweza kukosa mtu wa kusalimiana nawe kwa kushikana mkono na kama una biashara waweza kosa mnunuzi. Asemavyo da Yasinta ni kweli kuwa yategemea na mahali ulipo.
Kamala naona mada yako ni kiboko. Nimejiweka kwenye nafasi hiyo na kwa hakika unaweza kufunga macho yote. Umenikumbusha mawalimu wangu mkali wa sekondari aliyeingiliwa siafu "ofisi kuu" na kwa hakika ilikuwa mshikemshike kuvumilia na pia haikuwa rahisi kukimbia kwenda kuwatoa huko "ofisini" walikokuwa wameanza "uvamizi"
Fikiria ilikuwaje??!!!!!

John Mwaipopo 2:34 pm  

Hii mada si nyepesi ki hivyo. Hiyo 'kitu' tunafanya wote. Kuna ile ya kawaida ambayo ipo-ipo tu na pengine haitoi harufu sana,

Kuna ile inayokuja baada ya mrundikano wa haja na hakuna choo karibu. Yaani ile inayotokana na kubana-bana ukiwa katika harakati za kutafuta choo.

halafu kuna ya sauti kuu, yaani buuuuuuu!

Kuna ya shiiiiiiiii!

Halafu kuna ya sauti kama filimbi au mluzi.

Kila moja hapo ina stahii yake, hasa kutegemea na pahala ulipo na watu waliokuzunguka, au uliyenaye.

Kubwa katika mada hii ni reflection ya ufanyaji wa tendo hili na matendo mengine. mfano kama utoaji wako wa hiyo shughuli ni wa buuuuu, je inawezekana wewe hauna siri, au unashindwa kutunza siri.

Au yule wa shiiiiii ndio mtunzaji wa siri.

Si hili ni tendo la siri? au?

Christian Bwaya 2:33 pm  

Kazi kweli kweli. Kujamba? Nimecheka sana kusoma maoni ya Mwaipopo.
*********************

Naomba nikuombe Katibu, ufanye juhudi za kuifufua jumuiya yetu mwaka huu unaoanza. Nikuombe ulibebe jukumu hilo tuanze upya. Yaliyopita tuyaache yapite. Tunze upya.

Koero Mkundi 6:48 am  

Habari kaka Kitururu,

Nakutakia heri ya mwaka mpya wa 2009.
Naomba tuendelee kushirikiana kama mwaka uliopita.

Koero Mkundi 6:48 am  

Habari kaka Kitururu,

Nakutakia heri ya mwaka mpya wa 2009.
Naomba tuendelee kushirikiana kama mwaka uliopita.

Mzee wa Changamoto 11:44 pm  

Dah! Mwaipopo "kiazi" kwelikweli. Hahahahahaa

Simon Kitururu 4:59 am  

@Kamala: :-)

@Yasinta: Ulichosema ndio ilivyo kuna sehemu kujipikilisha matusi.
@Mzee wa Changa moto : Sina la kuongezea.
@John: Hahahah !Kwa maelezo yako asiye elewa au kucheka , basi tena!:-)
@Bwaya: ninaahidi kujitahidi niwezavyo.

@Dada Koero: Mimi sijambo, wewe je?Heri ya Mwaka Mpya kwako pia!Tuko pamoja kama mwaka jana tu!

@Kwa wote:Kuna walioruka kusoma msitari huu:

''Kumbuka lakini..

...labda kujamba haimaanishi KUJAMBA katika HADITHI HII, ingawa tabia fulani za binadamu ni USHUZI!:-(''

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP