Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Inawezekana bado TUNAOMBA MPAKA shenzi MBILI na NAKADHALIKA tatu!

>> Friday, December 05, 2008

Starehe na faraja ya waombaji , waulize waaminio Mungu.

Huachi kuomba ingawa hujapata, na kisiri una dhambi ya kuhisi pamoja na KUOMBA hutapata mpaka ufe INGAWA kwa imani UNAFARIJIKA kwa sababu LABDA ni MAPENZI ya MUNGU.


Labda kitufichiacho siri WAKATI TUNAOMBA, ni staili tu ya UOMBAJI!

Unaweza kuomba hata kwa kusisitizia kuwa huombi mvua zinyeshe ili kuwe na kichaka kwa sababu gesti BEI ghali.

Labda tuna busara, ingawa tunaomba tuepushwe na mabaya wakati umati mzima unajua sie ndio wabaya kwa kujifanya hatuna ubaya kwa kuwa tunatoa SADAKA KANISANI na ijumaa kabla hata hatujaingia msikitini TUNAMSAIDIA MASIKINI WA PESA, aliye tajiri wa roho , kabla ya kutema mate KIDOGO kwa sababu OMBAOMBA ana jipu kidogo maeneo lenye kushamiri USAHA.



Lakini....
....Unaweza kudhani kama tungekuwa nacho labda tusingelazimika kuomba.

Labda...
....kwa sababu MBWA MMOJA hana KIDUDE cha kike na cha kiume katikati ya miguu , kwa hiyo mwenye cha kiume atalazimika kuomba agusishwe cha kike hata kama nia ni mtoto wa kiume.

Lakini bado ....
.....wenye vyote wanaomba kwa sababu hata kama kipo, kunawaonao upungufu wa chao labda kutokana na kukosa utamu wa KUOMBA kwa kuwa hakikuombwa.

Swali:

  • Unajua unaweza kuwa unamuomba kwa kujifanya humuangalii?
  • Unajua inawezekana ulishawahi kuomba MAZIWA kwa kulilia CHUCHU,TITI au NYONYO?


Naacha!

Tulia na ZOUK LOOK- Pleure



Au tupate tu Wreck n EffeCT washauri utingishe TAKO katika RUMP SHAKER

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP