Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hivi NI TATIZO kwa mwenye PENGO , kujivunia PENGO kwa kuliita pengo MWANYA?

>> Saturday, December 20, 2008

Kama huna, cha kupoteza HUNA.
......Labda pengo ni zuri kama mwanya ikiwa jino hUNA.

Kama huna , ulichonacho ni uwezo wa kuwa na ambacho hUNA,
...ingawa labda ukiwa huna una SUNA.

Tatizo lakujazia ambacho huna,
..kuna wanunuao koroboi ingawa SI KWELI umeme hakUNA.

Mwenye pengo si kweli meno yote hUNA,
.... na waweza kula nyama ingawa kuna wadaioUNA PENGO na mwanya hUNA.

-Mwanya ni nini , kama si ukubwa wa pengo ambapo jino HUNA?

Na....

Mfurahia mwanya labda ni kweli mapengo hana

Na....

Aridhikaye na mapengo,
.... ana meno ya kutafunia kigumu na labda ambacho huna.


-Nini kikuonyeshacho nani kibogoyo ,wakati chako cha kutafuna na meno yako HUNA?


-Kama una mapengo na mwanya, nini huna kama wenye meno watafunavyo cha kujivunia hakUNA?
---------------------_______________-----------------------

Nawaza tu Mkuu!

Tupumzike na NANKO katika LUCKY U


Au tu BASCOM X aje na - Eyes On The Prize

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP