TUNAAMBIWA leo ni siku ya UKIMWI wakati;'' WAKATI wowote ni wakati wa CHAI''!
>> Monday, December 01, 2008
Leo ni siku ya UKIMWI!
Lakini juzi na jana, kama tu kesho zina sekunde iwezeshayo yeyote aliye HAI kuukwaa UKIMWI au hata KUISHI na UKIMWI kabla ya kuuawa na ugonjwa kama TB ulioibuka kutokana na mwili kukosa kinga kutokana na vichina vya UKIMWI.
Bado asilimia kubwa hatupimi UKIMWI kutokana na kuogopa kujua ukweli labda tuna UKIMWI!
Sababu kubwa ya watu kuogopa kujulikana wanao MDUDU ni WEWE na MIMI katika vitendo vyetu tuwatendeavyo WAATHIRIKA.
Kutokana na tuwatendeavyo, tufikiriayo au hata tusitishavyo mpaka matamanio kwa tuhisiye ANAO, aliyenao anaweza asikustue anao ili umnyime kitumbua hata kwa ahadi angekula au kushikashika na GLOVU.
Tujikinge wakati wa kufanya NANIHII lakini!
Kikubwa zaidi...
....tujichunguze kama sio sisi tusababishao mpaka KUBWA ZIMA moja likashauri kuwe na SIKU maalumu ya UKIMWI .
Tuchunguze tunawatendeaje tujuao wana UKIMWI ingawa tunajifanya tuna liroho zuri lisababishalo mpaka ndugu wanashindwa kutuambia ukweli kuwa wamedaka MDUDU tena kwenye ajali ya baiskeli au toroli .
LEO NI SIKU ya UKIMWI!
Swali:
- Si wakati wowote ni wakati wa CHAI?
Hebu tusikilize mmoja wa wanaojua wanaongea nini kutokana na uzoefu....
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment